Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Kama umezaliwa familia masikini, na unampango wa kufanikiwa/kutoboa maisha yaani angalau uwe na nyumba nzuri, Gari, na watoto waishi Maisha poa.
Basi inakupasa utambua baadhi ya Kanuni. Ingawaje Watu wanasema Maisha hayana Formula lakini zipo Formula katika Maisha ambazo ukizifuata unanafasi ya kufanya vizuri.
Ikiwa bado hujaoa na umefikisha umri wa kuoa lakini bado unajitafuta, Maisha yako hayajakaa kwenye Mstari unaoutaka.
Basi Taikon nitakueleza haya;
i. Usioe bila ya kuijenga Imani ya Mkeo kwako.
Wanawake wanaongozwa na Imani kuliko Upendo. Wakati wanaume tunaongozwa na Upendo kuliko Imani. Jenga uaminifu Kwa Mkeo. Akuamini wewe tuu. Sio Mchungaji, sio mganga, sio Rafiki zake, sio Ndugu au wazazi wake. Mfanye mwenza wako akuamini.
Mwanamke akikuamini atakuwa wazi Mbele yako. Ni rahisi kumuelewa kwani hatakuwa MTU wa kujificha ficha, na hata siku akijificha tayari utakuwa umeshamjua.
Zingatia katika kipindi cha mwanzoni unapomchumbia mtoto wa kike atakuwa MTU wa kukuficha vitu vingivingi, hii ni Kwa sababu hakuamini, anajiona hayupo Safe kwako. Anaweza akawa anakupenda na ukawa unampenda lakini asikuamini. Hilo ni kosa. "Mfanye Akuamini"
ii. Jenga Mtazamo wa Mchumba wako uwe Bora dhidi yako.
Ukishajenga Good Attitude Kwa Mwanamke itakusaidia kumuongoza yeye kama Mkeo. Lakini akiwa na bad attitude hutoweza kumuongoza, atakusumbua tuu. Hata umpige haitasaidia. Mwanamke mwenye Good Attitude lazima awe Mama Bora Kwa Watoto wako. Atajua namna ya kukusapoti katika nafasi yake kama MKE.
Kumbuka Imani na Mtizamo vinajengwa, upendo haujengwi, upendo unakuja automatically. Upendo unaojengwa hauwi natural, ni artificial Love ambao mara nyingi haudumu.
iii. Jenga kujiamini kwake na kujitegemea kwake.
Hakikisha Kabla Mwanamke hujamuoa umemfanya ajiamini, kisha mfundishe kujitegemea. Mfundishe kufanya mambo pekeake. Lakini Jambo hili lifanyike mara Baada ya kupitia hatua hizo mbili hapo juu.
Wapo wanaume waoga, wasiojiamini ambao kwao huona Mwanamke akijiamini na kujetegemea wanahisi nafasi Yao itakuwa Hatarini. Huo ni woga wa kijinga, ni dhana potofu.
Ni rahisi kuishi na Mwanamke anayejiamini na kujitegemea kuliko kuishi na Mwanamke tegemezi na asiyejiamini. Kwa nini umhofie Mwanamke, kwamba ili uishi naye basi lazima umfanye asijiamini au asijitegemee? Come on! Hiyo sio nzuri.
Wewe ni mwanaume, Mungu amekupa Akili kubwa mara elfu ya Mwanamke. Kwa nini umhofie Mkeo? Huo unaitwa ukandamizaji na unyanyasaji. Mkeo umhofie ikiwa;
i. Amekuzidi Akili.
ii. Hakuamini
iii. Ana Mtazamo Basi/ bad attitude.
iv. Hakupendi Sana (ingawaje Mwanamke Hana upendo wa dhati 100%)
Mfanye Mkeo ajitegemee kiakili, Kiroho, kihisia na kimwili. Mfanye awe na uchumi Bora. Zingatia Wakati unamfanya ajiamini na kujitegemea sharti wewe uwe zaidi yake. Yaani wewe ndio uwe Role model wake. Sio akuzidi, Noop!
Lakini kama itatokea mazingira ya yeye kukuzidi hasa mambo ya kiuchumi hiyo kwako Isiwe shida. Shida iwe akikuzidi Akili na maarifa.
iv. Jiweke kama Mwanaume.
Jitukuze, jidhihirishe kuwa wewe ni mwanaume, Angalia hata wanyama wa jinsia ya kiume the way wanavyo-act. Muangalie Jogoo, Simba Dume, Bata dume, Beberu n.k. kujitamba ni moja ya Tabia za mwanaume.
Lakini mpaka unajitamba uwe na Sababu za kufanya hivyo. Kujitamba na majigambo Kwa Mwanamke au Mkeo huhesabika kama dalili ya kujiamini.
v. Jenga UMOJA na USHIRIKIANO na mwenza wako.
Tayari anakuamini.
Tayari anamtazamo chanya juu yako na Maisha Kwa ujumla.
Tayari anajiamini na kujitegemea.
Tayari anakuona wewe ni Baba na mume kwake. Automatically UMOJA na USHIRIKIANO utakuwa dhahiri katika familia yenu.
Hata kama haumuamini Mkeo lakini usionyeshe kutokumuamini. Hiyo husababisha na kuondoa Imani yake juu yako.
Sishauri wanaume muwaamini wake zenu lakini ninajaribu kueleza kuwa Waonyesheni mnawaamini. Na ili Mwanamke ajue unamuamini basi lazima umfanye ajiamini na kujitegemea, kisha umshirikishe mipango yako na hatua zinazofuata.
Mwanamke Kwa kumfanyia hivi anajiona unampenda, lakini pia anaona unandoto naye.
Zingatia: Kabla hujafanya haya lazima uthibitishe kuwa huyo Mwanamke ndiye sahihi. Sio uokote Makahaba WA mjini alafu ufanye huo upuuzi wako. Utakwama!
Huwezi fanikiwa kwenye Maisha yako ikiwa wewe na Mkeo hampo pamoja. Ili familia yako ifanikiwe lazima wewe kama Baba ujenge UMOJA na USHIRIKIANO na Mkeo ili baadaye Watoto waige Kutoka kwenu huo UMOJA na USHIRIKIANO.
Sio uwaambie Watoto wawe wamoja na washirikiane ilhali Watoto hawajawahi kuona huo UMOJA na USHIRIKIANO kwenu(wewe na Mkeo).
Epuka mambo ya Familia ya Kwenu na familia ya Mkeo. Ubinafsi wa kupendelea kwenu au mkeo kupendelea Kwao huo ndio utakaowakwamisha pakubwa. Kitendo cha Mkeo kusema Wazazi wake ni Bora zaidi kuliko wewe tayari kinatafsiri kuwa hiyo familia yenu imeshashindwa.
Kitendo cha wewe(mume) kusema Wazazi wako ni Bora kuliko mkeo au wazazi wa Mkeo tayari umeshatangaza hapo hakuna Familia. Mmeshindwa Kabla hamjaanza. Kamwe hamtotoboa.
Ni suala la muda tuu. Unaweza kujiona unapata Maendeleo lakini nakuhakikishia kuna siku inakuja utapiga mzinga ambao utakuacha mdogo wazi. Kila ulichokitafuta kitaanza Kupotea tena Mbele ya macho yako. Hayo ni matunda ya kutokuwa na UMOJA na USHIRIKIANO.
Hakikisha wewe na Mkeo (ninyi kama familia) kila kitu kinaenda Kwa Haki. Ubinafsi usionekane mahali popote pale. Kama vile Mkeo anavyotaka uwe MTU mkubwa na ufanikiwe ndivyo hivyohivyo na wewe unapaswa umsapoti Mkeo afanikiwe.
Kwa maana Mafanikio yenu ndio Mafanikio ya familia na watoto na wajukuu zenu. Msioneane Wivu na vijicho. Hii Tabia tunayo Sana WANAUME.
Mkeo akipanda cheo au akipata kazi, unapatwa na hofu. Woga wa nini. Kwamba utachapiwa? Kwamba atakuachia?😊😊 Kuachwa kupo tuu. Mkeo anaweza kukuacha hata kama ni mama WA nyumbani.
Elewa kuwa Mwanamke atakudharau endapo utaacha na kushindwa kuwa Mwanaume. Elewa kuwa Mwanamke hawezi mdharau Baba yake kama vile kijana asivyoweza kumdharau Mama yake.
Taikon nimemaliza.
SABATO NJEMA.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

- Kuwa mwenye Akili,
- Kuwa na mbinu elfuelfu mbadala za kukabiliana na matatizo.
- Kuwa Msafi na mtanashati, jua kuvaa vizuri kulingana na maumbile yako, umri wako na hadhi yako. Usikubali kuwa mchafu mchafu au usiye na Swaga.
- ongea Kwa madoido ya kiume.