Nakubali kuwa mimi ni kiraka,nimeziba nafasi iliyokua wazi ila sio mchepuko coz mimi ndie njia pekee anayopita mume wangu kipenzi.Tunaishi maisha yetu hatuigizi.Kama ni mwanamke, wewe ni kiraka tu. Mchepuko. Kama ni mwanaume, wewe ni buzi tu. Coward. Huna sababu ya kuigiza maisha wanayoishi wanandoa halali. Badala ya kuwaza future na umoja na familia wewe unawaza ubinafsi na mali
Mkuu samahani kidogo.Ndoa kwangu naichukulia kama jambo la kiroho zaidi, najua wenzangu mna mitazamo yenu tofauti ndio maana mnaichukulia ndoa kama issue flani tu!.
Sioni sababu kwanini uogope kutoa mali kwa familia ambayo tayari una damu yako [watoto] hata kama mali hiyo ulipewa na mama yako mzazi bila kuwepo mumeo.
▪ Hakuna mama anayeweza kasirika akiambiwa na binti yake ile nyumba uliyonipa nimeitoa kwa wajukuu zako, hayupo!.
Kwenye ndoa tunazungumzia muunganiko wa wawili kuwa mwili mmoja, sasa kwanini kanisani mjiite "mwili mmoja" wakati vichwani mwenu mali zenu hamtaki ziwe za familia? Utapeli.
Hapa kuna tatizo kwenye mindset, na nakubaliana na prida 100% watoto wa kike wengi mnazitaka ndoa kama maonesho, muitwe wake za watu, mheshimiwe na jamii iliyowazunguka, lakini kiuhalisia hamjitoi 100% kwa ajili ya hizo ndoa zenu.
Kwa hii mentality yenu, basi nina hakika wale kataa ndoa wataendelea kusimamia misimamo yao, nyie mnaingia kwenye ndoa na mindset ya kitapeli, ya kibinafsi kuficha mali zenu.
Bora muolewe na hizo mali zenu wallah ndoa zenu zitadumu, na mtazitumikia kwa 100%
Hamna kitu napenda kama kuona denoo G na binti kiziwi kwenye mijadala.Hasa ambayo hawakubaliani..😃Kwaheri Denoo, leo hautanikausha maji 😂
Asante sana kwa huu ufafanuzi mkuu.🙏Mali za kabla ya ndoa hazigawanywi lakini kuna kitu wengi hawakijui. Hili mali hizo zisiletwe kwenye mgao zinatakiwa kuwa vile vile kama ambavyo zilikua wakati mnafunga ndoa. Mfano nimejenga nyumba kabla ya kumalizia kupiga rangi nikafunga ndoa. Masuala mengine kama rangi, tiles, ukuta nikamalizia nikiwa ndoani. Hapo kwenye divorce settlement hiyo nyumba italetwa kwenye mgao kwa sababu imeongezeka thamani nikiwa ndoani.
Niwe na duka, kampuni, kiwanda n.k mali husika inatakiwa ibaki vile vile ili isiletwe kwenye mgao. Ukiiongezea thamani mtu kiwanda ukaongeza ukubwa wa uzalishaji au kampuni ukafungua matawi mengine. Mali inaletwa kwenye mgao.
McKenzie Scott akiolewa na Bezos wakati ambao Amazon tayari ishaanzishwa na walibyotalakiana McKenzie akapata mgao wake kwa sababu Amazon ilikua kubwa tofouti na wakati wanafunga ndoa
Uko sahihi kabisa mkuu,nakubaliana na wewe kwa yote ulosema hapa ila kuishi upweke nalo ni tatizo ndo mana nikashauri kuishi na mwenza kwa style itakayosaidia kuepuka changamoto hizo.Tunakataa ndoa sio kwa sababu ya mgao wa mali tu, tunakataa ndoa kwa sababu mfumo wa mzima ukiufanyia tathmini na maisha ya sasa unaona hakuna faida iliyobaki kwa ajiri ya mwanaume uko kwenye ndoa.
Modern marriage demand traditional sacrifices from men, while removing nearly every traditiinal benefit that once came with it
-mwanaume anatakiwa kuprovide lakini asiwe na mamlaka juu ya mwanamke(mnaita uswa aa kijinsia)
-ndoa za kisasa ni presha na stress kwa mwanaume, sio amani
-risk to reward ratio haiingii akilini. Nitumie maisha yangu yote kutafuta hela, kujenga himaya yangu na future yangu only to lose half of it through one emotional decision. Tottaly bullshit.
-mwanaume anatakiwa kujitoa wakati wanawake wanaambiwa wajipe kipaumbele wenyewe.
Zaidi ya mgao wa mali zipo sababu nyingi sana za wanaume kuachana na suala ndoa.
kukataa ndoa na kukataa mahusiano ni jambo linaloelekeana. mtu anayetakiwa kutiliwa mashaka ni yule anayekataa kujihusisha na mahusiano/ndoa moja kwa moja.Yawezekana faida za ndoa zikawepo chache tu ila hii ya kufa bila msaada ni kufilisika kwa hoja ndani ya ya hiyo taasisi ya ndoa
Kunikamata kweli kanikamata coz nampenda sana Mr. wangu na kweli kaleta furaha maishani mwangu na kweli nilikua mpweke kama unavyohisi na kweli natamani kweli kufunga ndoa na kuvaa shela na siku hiyo wangenikoma ila kwa ufafanuzi wa kisheria aliutoa mkuu Natafuta Ajira sidhani kama nitafunga ndoa.Jamaa kajua kukukamata yaani sogea tukae lakini unaamani na furaha hivyo siku mkifunga ndoa sijui itakuwaje inaonekana ulikuwa mpweke sana.
Na ni vyema kipindi hiki cha ujana wenu mkitumie kwanza kujenga maisha yenu,mu enjoy life,mpate muda wa kukosea na kujifunza,mkue kwa namna zote ndio suala la kuishi na mwenza lifuatie.Vijana wa 20s tukisema tunakataa ndoa ni kama mzaha tu, bado pilika za maisha hazijakolea vizuri, bado hata hatuujui upweke vizuri.
Naona leo kidogo umerudi kwenye uhalisia, the other day ulikuwa kwenye mihemko ya hatari!.Mkuu samahani kidogo.
NItafurahi ikitambulika kwamba miimi sina minndset ya kutaka ndoa kama maonesho.Yaani kuolewa tu ili na wewe uitwe Mrs fulani.Sikumbuki ni wapi nimesema hivyo mkuu.
Nakumbuka nilisema watu wanatakiwa kuishi pamoja kwa sababu ya mapenzi tu.Wapendane na kuendana na sio kwa sababu nyingine yeyote ile.
Mali za wote zinapaswa kunufaisha wanafamilia wote ila sio sawa kusema tuolewe na mali kisa kuchukua tahadhari ya kutodhulumiwa iwapo ndoa itavunjika.
Jana tulielewana lakini!Hamna kitu napenda kama kuona denoo G na binti kiziwi kwenye mijadala.Hasa ambayo hawakubaliani..😃
May be!.😃😃
I was calm muda wote mkuu.
Ujue maandishi nayo yanaweza kusound ndivyo sivyo