Kijana wangu hataki kuonywa akikosea, ananuna haongei na mtu hata siku 3

Unambwatiza? Kwa umri huo unatakiwa uwe na staa unavomuonya kama ukiwa kimbau mbau ipo siku atakulamba makofi
Well said, wazazi wa kiafrika wanaunyang'au flani hivi wa kutokuwa na mipaka na kujua jinsi ya kuhandle mambo.

Kijana kwa umri aliofika TESTOSTERONE iko juu sana.Anatafuta uhuru wa kila kitu mpaka utawala😄😄😄.Ndio maana jamii ya simba mnyama, matoto madume yakibalehe yanafukuzwa kwenye himaya.Himaya huwa ni kiongozi au uongizi mmoja tu.

Kijana wako amefika level ambayo kwa asilimia kadhaa anatambua kuwa kuna vitu huna cha kumfanya ukitoa kumlipia ada na kumfadhili connection atakapomaliza chuo.

Na hili huwa wazazi wengi wanakwepa kulikubali kuwa, malezi na uzazi ni jambo la wajibu na lina ukomo😄😄😄 huwezi kijimilikisha maisha ya kiumbe mwingine.Umetumika vyakutosha kubali umetumia resource zako vya kutosha kuwakuza hao madogo ila at somepoint mamlaka yako yanaanza kushift kutoka kwako kwenda kwake ili aje ajitegemee.

Cha kukushauri ni kua anza kumtreat kama mtu mzima.Ukiletewa mashtaka yapokee kisha tafuta muda au nafasi mtoke wote mwenda hata sehemu gaurage,site, bar au kokote ambapo men issues zinafanyika mtoe kwenye hayo mazingira ya kikekike, kisha kwa utaratibu msomee mashtaka na umpe nafasi ya kujitetea baadae akimaliza mpe CODE ZA KIUME.Akifata sawa asipofata mpe muda, kuna vitu mtu anajifunza kwa vitendo.Tusitake kuwalinda sana majunior tunawanyima nafasi za kukosea na kujifunza vizuri.


Trust me mapokeo yake hapo yatakuwa ya utofauti sana. Ila ukianza kumfokea mbele ya wadogo zake au wanawake.Hapo lazima atareact na anahaki hata kama kakosea, wewe umeshindwa kumheshimisha.

Hawa madogo wanavitu vingi tunatakiwa kuwaelewesha kwa upole na hekima.


#Learning is a process!!
 
Kamaliza first year. Huyo ana mambo matatu.

1. Betting
2. Forex trading
3. Kujichua.

Anaweza kuwa anafanya yote matatu.
 
ana nyota ya trump, chuma kingine waluozaliwa 25 dec - 20 jan hawa ni mbuzi balaa lao sio la kitanganyika.
 
Hongera mzazi kwa kujionesha wewe ni …

Kwanza inakuwaje mtoto wa kumzaa wewe mwenyewe na bado yupo kwenye himaya yako anakuninia.TUKITUMIA ALILI SANA ITAONEKANA WEWE NDIO MWENYE KOSA

Nisiwe mwongo pia,fimbo,makonde,njaa,na vyote vinavyohusiana na adhabu ni ELIMU.Achana na scenario ya mtoto hapigwi,KITAKURAMBA.
 
Baba mtu fuata ushauri huu kijana ameshakua huyo mpe mke ndo dawa yake kubwa umri huo matamanio hua juu sanaa sasa ili kumtuliza mpe mke ata kama utamsaidia kila kitu wewe mwenyewe
 
Mkunjeni angali mbichi, acheni kulidekeza, myosheni mapena, la sivyo atanyoshwa na walimwengu...


Cc: Mahondaw
 
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.
wakati wa kumkunja ushaa pita, ukitaka kumpika kubali kutafuta sufulia kubwa ili atoshe.
Nyie ndiyo ambao mwanao akigombezwa na mtu mwingine mnanuna na ugomvi juu
Haya yamekukuta nawewe.
Pole
Sisi wengine tulikunjwa angali wa bichi, mzazi akifoka tunajua ni kunyenyekea tu euther unakosa au hauna
Kikubwa ni mzazi amekufokea
 
Wewe ni kampuni gani ? Yani kabila gani? Nikuambie jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…