DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Siungi mkono uchawi lakini pia siungi mkono kujichukulia sheria mkononi ikiwa kuna mamlaka za usalama.

Jambo lolote unalolifanya lifanye kwa manufaa yako wewe na familia yako pasi na kuwaaangamiza au kuwaingiza katika matatizo wenzio.
[emoji2956]
 
Wenzake wa kabwe wilaya ya nkasi walijidanganya hivo hivo Ila unaelekea kukata mwezi sasa watu wanazidi kusota rumande na waliokufa waliShazikwa kijjn mambo yanaendelea kama kawa. Walipiga vitisho vingi Ila mwisho wa siku wananchi ndo wanabaki kua wahanga wakubwa.
Na hawa kenge watasota sana.wanajidanganya wanaweza kuiroga serikali 🤣🤣
 
Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.

Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.
Kosa la raia lipo hapo, kilichowapata huwezi kusema ni bahati mbaya, ukichezea moto huwezi kuuomba moto uwe na busara, utakuchoma tu. Mlitaka busara gani? Mpewe mtu mkamuue? Shenzy type
 
Kwanza ni upumbavu kwenda kuvamia kituo Cha polisi. Siwapendi kabisaa police wa tz hasa utendaji kazii wao unahusisha matumizi kidogo mno ya akili lakini raia wamefanya upumbavu mkubwa walilazimisha kupata mkong'onto.
Ni police force na sio police service.
Akili kidogo maguvu mengi
 
Kwahiyo ndugu yako ni mtumishi wa umma nae alishiriki kuvunja kituo cha Polisi ili kumuadhibu mtuhumiwa wake, tupe jina lake tumsaidie
 
Wakuu, hii Nchi ya Ovyo sana, Kuna wajinga wanapopewa nafasi Huwa wanageuka kua Miungu watu.

Jana tarehe 4/10/2023 Kijiji Cha Kazuramimba, Wilayani Uvinza kulitokea vurugu baina ya Polisi na Raia, zilizopelekea Polisi kutumia Silaha za moto, hali hii ilipelekea Raia Kadhaa kufa na wengine kujeruhiwa .

RC, RPC na DC, wakaamua kuzitembelea Hosp zilizopokea majeruhi kimyakimya na kuwaonya kutotoa Taarifa.

Chanzo cha Ugonvi...

Kuna waganga walipelekwa Kijiji huko Kwa Imani za kijadi kwamba wanatafuta wachawi, Kuna mji Mmoja mwenye mji huo akagundulika na Mchawi, Akakimbilia Polisi kishtaki.

Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.

Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.

Polisi wakaanza kutumia Silaha za moto yaan Bunduki kushambulia Raia.

Raia wengi sana wamejuruhiwa, Vijana, Wanawake na watoto na wazee wameumizwa sana.

Polisi wamewakamata watu Kadhaa na majeruhi Kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana, mpaka Sasa Ndugu wanafuta Ndugu zao .

Ni majeruhi wachache tu Tena waloamua kujipeleka Hosp ndio ambao wamejulikana mpaka Sasa ,huku wengine wakiwa hawajulikani.

Polisi wa Kigoma, wanaongoza kuwa na matukio ya "Majeruhi alinyakua Bunduki ya Polisi nakuanza kurushiana risasi ".

Ndugu zangu nawaomba sana Mnisaidie Kupaza sauti,. Ndugu yangu Yuko huko Kikazi, amesombewa humohumo , mpaka Sasa hatuma Taarifa ya uhai au lolote kumhusu yeye.
Dah!...poleni Sana.

Ila raia kuvamia kituo cha polisi na kujaribu kumchukua mtu kutoka hapo kwa nguvu ni kosa na uvunjaji wa sheria

Poleni Sana
 
Wakuu, hii Nchi ya Ovyo sana, Kuna wajinga wanapopewa nafasi Huwa wanageuka kua Miungu watu.

Jana tarehe 4/10/2023 Kijiji Cha Kazuramimba, Wilayani Uvinza kulitokea vurugu baina ya Polisi na Raia, zilizopelekea Polisi kutumia Silaha za moto, hali hii ilipelekea Raia Kadhaa kufa na wengine kujeruhiwa .

RC, RPC na DC, wakaamua kuzitembelea Hosp zilizopokea majeruhi kimyakimya na kuwaonya kutotoa Taarifa.

Chanzo cha Ugonvi...

Kuna waganga walipelekwa Kijiji huko Kwa Imani za kijadi kwamba wanatafuta wachawi, Kuna mji Mmoja mwenye mji huo akagundulika na Mchawi, Akakimbilia Polisi kishtaki.

Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.

Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.

Polisi wakaanza kutumia Silaha za moto yaan Bunduki kushambulia Raia.

Raia wengi sana wamejuruhiwa, Vijana, Wanawake na watoto na wazee wameumizwa sana.

Polisi wamewakamata watu Kadhaa na majeruhi Kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana, mpaka Sasa Ndugu wanafuta Ndugu zao .

Ni majeruhi wachache tu Tena waloamua kujipeleka Hosp ndio ambao wamejulikana mpaka Sasa ,huku wengine wakiwa hawajulikani.

Polisi wa Kigoma, wanaongoza kuwa na matukio ya "Majeruhi alinyakua Bunduki ya Polisi nakuanza kurushiana risasi ".

Ndugu zangu nawaomba sana Mnisaidie Kupaza sauti,. Ndugu yangu Yuko huko Kikazi, amesombewa humohumo, mpaka Sasa hatuma Taarifa ya uhai au lolote kumhusu yeye.
Wamevamia polisi ni haki ya polisi kuwashughulikia, unadhani wangeingia ndani ya kituo na kuchukua silaha za moto si ingekua vita. Mimi nawatetea ndugu zangu askari polisi wamejilinda kwa weledi na kuhakikisha kituo hakiingiliwi na sila haziibiwi.
 
1.Kwa Nini hao waganga wanaleta taharuki Kwa kuwapa watu tuhuma zisizo na uhakika Moja Kwa Moja?

2.Kwa nini Raia wavamie kituo Cha polisi

3.Kwa Nini ndugu yako mgeni ajihusishe kwenye vurugu?am sure angetulia alipofikia asingekamatwa
 
Siempre PT[emoji120]
 
Back
Top Bottom