DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

DOKEZO Kijiji cha Kazuramimba (Uvinza, Kigoma): Mauaji yaliyofanywa 4/10/2023 ninayekemea kwa nguvu zote, Majeruhi wako wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kigoma ina wakimbizi wengi....

Tunajuaje kuwa hao WAVAMIZI wa hicho KITUO si MAGAIDI ?!!!

Je hawakuwa na lengo la KUPORA SILAHA ZA MOTO ?!??![emoji15][emoji15]
 
Endelea kushabikia matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.

Kwani kuna hasara gani kuwaelimisha na kuratibu uondoshwwji wa changamoto zao?

Wachawi ndo walituletea Mwenge wa Uhuru na ndiyo wanaotuwekea viongozi madarakani ujue


Wapi nimeshabikia?

Polisi wametumia nguvu kwa wananchi ambao wamevamia kituo cha Polisi kumsaka mtuhumiwa alieenda kujisalimisha kwa hao Polisi. Ubaya uko wapi hapa?

Kwani hao wananchi walitegemea reaction ipi kutoka kwa walinzi wa Amani / Polisi nyakati za fujo / uvunjifu wa Amani?

Hao wananchi hawajui kwamba vita yoyote ile ni maandalizi na mipango madhubuti kabla na sio malalamiko baada?

Sasa unaingia vita dhidi ya Uchawi na wachawi wa kiAfrika kirahisi namna hii kwa kutegemea huruma ya yule yule anaelipwa na kuongozwa na huyo huyo anaekuroga?
 
Serikali ikikuuliza leta ushahidi ya kwamba huyu amekuzuia usiendelee.
Utapeleka ushahidi gani ili achukuliwe hatua.
Serikali yetu haiamini katika masuala ya uchawi ila watendaji wake huenda wakawa wanaaamini uchawi.
serikali sindio watu wenyewe sasa. Utasemaje serikali haiamini uchawi wakati walozi wanaalikwa White house kumzindika mkulu
 
Kituoni kuna watuhumiwa wengi ...

Tunajuaje hawakuwa na lengo la kuwatorosha na watuhumiwa wengine?!!! [emoji15][emoji15]

Mob psychology [emoji45][emoji45]
 
Endelea kushabikia matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.

Kwani kuna hasara gani kuwaelimisha na kuratibu uondoshwwji wa changamoto zao?

Wachawi ndo walituletea Mwenge wa Uhuru na ndiyo wanaotuwekea viongozi madarakani ujue
Na wewe unahitaji kupigwa mpaka akili yako ikukae sawa. Hii nchi bado kuna wajinga wengi sana kumbe.
 
Wakuu, hii Nchi ya Ovyo sana, Kuna wajinga wanapopewa nafasi Huwa wanageuka kua Miungu watu.

Jana tarehe 4/10/2023 Kijiji Cha Kazuramimba, Wilayani Uvinza kulitokea vurugu baina ya Polisi na Raia, zilizopelekea Polisi kutumia Silaha za moto, hali hii ilipelekea Raia Kadhaa kufa na wengine kujeruhiwa .

RC, RPC na DC, wakaamua kuzitembelea Hosp zilizopokea majeruhi kimyakimya na kuwaonya kutotoa Taarifa.

Chanzo cha Ugonvi...

Kuna waganga walipelekwa Kijiji huko Kwa Imani za kijadi kwamba wanatafuta wachawi, Kuna mji Mmoja mwenye mji huo akagundulika na Mchawi, Akakimbilia Polisi kishtaki.

Polisi wakamficha hapo na Raia wakamfata hukohuko.

Kukosekana Kwa Busara baina ya Polisi na Raia,. Fuji zikatokea na kituo Cha Polisi hiko kikavunjwa.

Polisi wakaanza kutumia Silaha za moto yaan Bunduki kushambulia Raia.

Raia wengi sana wamejuruhiwa, Vijana, Wanawake na watoto na wazee wameumizwa sana.

Polisi wamewakamata watu Kadhaa na majeruhi Kadhaa na kuwapeleka kusikojulikana, mpaka Sasa Ndugu wanafuta Ndugu zao .

Ni majeruhi wachache tu Tena waloamua kujipeleka Hosp ndio ambao wamejulikana mpaka Sasa ,huku wengine wakiwa hawajulikani.

Polisi wa Kigoma, wanaongoza kuwa na matukio ya "Majeruhi alinyakua Bunduki ya Polisi nakuanza kurushiana risasi ".

Ndugu zangu nawaomba sana Mnisaidie Kupaza sauti,. Ndugu yangu Yuko huko Kikazi, amesombewa humohumo , mpaka Sasa hatuma Taarifa ya uhai au lolote kumhusu yeye.
Mnataka serikali ishirikiane na walozi kuendesha nchi? Wahalifu huwa hawapatikani kwa ramli.
 
Kwenye mambo ya kijinga kama hayo nawaunga mkono polisi, kuna wakati kumuuwa mwehu kiburi ndio sululu ya mgogoro.
Hauwezekani kikundi cha wajinga kiende kuvamia kituo cha polisi kwa hoja za kumtaka raia mwenzao wakamfanye wanachotaka wao.
Kazi ya jeshi la Polisi ni kulinda raia na Mali zao, na hawawalindi raia hao dhidi ya wanyama bali dhidi ya binadamu wenzao wajinga.
Waambieni watu wa Kazuramimba waache upumbavu wa kuvamia vituo vya polisi, tena wakijitoa ufahamu itaundwa kanda maalum ya Kazuramimba, huwezi kuwavamia polisi halafu wakuache uwaumize wakat silaha zipo.
Polisi fanyeni kazi yenu msipndwe vichwani na washirikina, tena kamateni hao waganga wote swekeni ndani iwe fundisho. Hizi ramli zao zimepingwa hata na dini zote.
 
Nisaidie hiko chuo nimehangaika sana kukipata nataka kwa dhati kabisa kuwa mchawi
Kwa taarifa yako UCHAWI si dili....

Si dili....

Utawaachia vizazi vyako LAANA....

Ziko kafara za damu....

Ukifa...huko nyuma ni laana ,balaa na mikosi....

Hakika uchawi ni LAANA....

Bora huyajui hayo MAMBO....
 
serikali sindio watu wenyewe sasa. Utasemaje serikali haiamini uchawi wakati walozi wanaalikwa White house kumzindika mkulu
Hivi uliwahi.kusikia katika nchi ya Tanzania mtu amehukumiwa mahakani sababu ya uchawi.
Binafsi sijapata kusikia labda kama unajua unifahamishe.

Hata kama serikali inaamini uchawi ni ushahidi gani utatumika kama kithibitisho cha kumkamata mtu akiwa mchawi.
Mwisho kabisa kuwa mchawi sio shida wala dhambi.
Je unautumia uchawi huo katika masuala yapi au kwa manufaa gani.
 
Raia kuvamia kituo cha polisi ni kosa kubwa sana.
Smg hapo unafungulia (blast) unaminya trigger hadi ziishe
 
Mahakama zipo ...

Mpelekeni mahakamani kwa hizo tuhuma za "yasiyoonekana"....

Ni kweli uchawi upo....ni sayansi ya "gizani"....

Unashinikizaje polisi wakupe mtuhumiwa ?!!![emoji15][emoji15]

Raia wajibu wetu si kutii sheria zetu wenyewe?!!! [emoji15][emoji15]

UNAVAMIAJE KITUO CHA POLISI???? [emoji15]
Kuna watu Wana ujinga mwingi sana kichwani. Yaani wanafanya nakosa ya wazi sana ambayo hata kuchomoka kwenye mkono wa sheria ni ngumu.
 
Back
Top Bottom