Kikao cha Dkt. John Magufuli, Tundu Lissu, Dkt. Hussein Mwinyi na Maalim Seif Sharif Hamad ni muhimu kabla ya utangazaji matokeo

Kikao cha Dkt. John Magufuli, Tundu Lissu, Dkt. Hussein Mwinyi na Maalim Seif Sharif Hamad ni muhimu kabla ya utangazaji matokeo

Ninavyoona mimi inasikitisha mno uchaguzi huu unasikitisha wapendwa Tuombe Mungu sana atuepushe na dhahama maana mhemko ni mkubwa mno
 
WanaJF,Salaam!

Ninapendekeza kifanyike kikao cha haraka kitakachowakutanisha wagombea wenye nguvu kwa upande wa Zanzibar na Tanganyika ikiwezekana hata wasiokuwa na nguvu wahusishwe.

Kikao hicho kiwe na uwezo wa kuwajenga kisaikolojia, kuwaangaliza na kuwataka kuheshimu katiba ya nchi, utashi wa wapigakura, na utayari wa kukubali matokeo ya uchaguzi. Aidha, kikao hicho kwa kiasi kikubwa kinaweza kuratibiwa na uongozi wa Kanisa la Waadiventista Wasabato kwa kuwa huwa hawana upande wowote - lakini pia balozi zetu na asasi za kiraia zaweza kushirikishwa.

Kwa mtazamo wangu sioni haja kabisa ya mabomu kutumika katika uchaguzi na utangazaji matokeo, sioni haja ya risasi kutumika, sioni haja ya tume kusafisha wagombea kwa dodoki, sioni haja ya maandamano, wala sioni haja ya wagombea kuhasimiana. Naona haja ya mgombea kukiri kushindwa na kupongeza aliyeshinda kihalali.

Tanzania ni moja na hatuwezi kupata Tanzania nyingine ikiwa itavurugika, Zanzibar ni moja na hatuwezi kupata nyingine ikiwa itavurugika.

Nawatakia uchaguzi mwema 2020
Msakila Mussa Kabende
Mwanaccm
Kigoma - Tanzania
25 Oktoba, 2020
Hakuna kikao ,wizi wa kura hautakubalika ,tume watangaze matokeo ya kweli ,wakileta za kubumba bumba imekula kwao!!
 
Umeshakosea unaposema wagombea wenye nguvu wakutane unamaana nani ananguvu kumzidi Magu au unataka kikao kimpe mgombea wako nguvu. Hakuna ujinga kama huo kufanyika, wabashiri wa mambo ya kisiasa wanasema Lisu atapata kura asilimia chini ya 10.
 
Back
Top Bottom