Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mwenyekiti Mbowe, kwa kiasi kikubwa, bila ya kuwahusisha viongozi wenzake na wanachama, ndiye aliyeingia kwenye maridhiano bandia na Samia. Na ni yeye, ndiye mara nyingi aliwashawishi wanachama na viongozi wenzake kuwa maridhiano yalikuwa na faida na dhamira njema.
Leo kila mmoja ana uhakika kuwa maridhiano yale na 4Rs ulikuwa ni utapeli wa hali ya juu kwenye siasa.
Mariadhiano ulikuwa ni mchezo wa mfugaji wa kuku wa kienyeji anayetafuta kuku wa kumchinja, kuku yupo nje, anamrushia mtama ndani ya chumba, kuku aliyekosa ung'amuzi, anaamini kuwa anapendwa sana ndiyo maana amepewa chakula ndani ya nyumba, anaingia ndani, kisha mfugaji anafunga mlango, anamkamata na kwenda kumchinja. Maskini kuku huyu mjinga, siku aliyoamini sasa anapendwa na kuthaminiwa sana, kumbe ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa uhai wake. Anauawa bila kelele, bila hata kuku wenzake waliopo nje kusikia, bila ya kuwa na uwezo hata wa kukimbia.
Mazingira ni magumu sasa kuliko hata wakati kabla ya maridhiano haya bandia. Mwaka 2019, walipora tu uchaguzi, lakini hakuna waliotekwa wala kuuawa wala kuumizwa. Uchaguzi wa mwaka huu, wamepora uchaguzi, wameua na kuwaumiza wote walioonesha dalili ya kutaka kuzuia uporwaji wa uchaguzi.