Kikao Cha Kamati Kuu, kwenye Habari ya Maridhiano, Mbowe akiri alifanya kosa kubwa

Mwenyekiti Mbowe, kwa kiasi kikubwa, bila ya kuwahusisha viongozi wenzake na wanachama, ndiye aliyeingia kwenye maridhiano bandia na Samia. Na ni yeye, ndiye mara nyingi aliwashawishi wanachama na viongozi wenzake kuwa maridhiano yalikuwa na faida na dhamira njema.

Leo kila mmoja ana uhakika kuwa maridhiano yale na 4Rs ulikuwa ni utapeli wa hali ya juu kwenye siasa.

Mariadhiano ulikuwa ni mchezo wa mfugaji wa kuku wa kienyeji anayetafuta kuku wa kumchinja, kuku yupo nje, anamrushia mtama ndani ya chumba, kuku mjinga anaamini kuwa anapendwa sana ndiyo maana amepewa chakula ndani ya nyumba, anaingia ndani, kisha mfugaji anafunga mlango, anamkamata na kwenda kumchinja. Maskini kuku huyu mjinga, siku aliyoamini sasa anapendwa na kuthaminiwa sana, kumbe ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa uhai wake. Anauawa bila kelele, bila hata kuku wenzake waliopo nje kusikia, bila ya kuwa na uwezo hata wa kukimbia.

Mazingira ni magumu sasa kuliko hata wakati kabla ya maridhiano haya bandia. Mwaka 2019, walipora tu uchaguzi, lakini hakuna waliotekwa wala kuuawa wala kuumizwa. Uchaguzi wa mwaka huu, wamepora uchaguzi, wameua na kuwaumiza wote walioonesha dalili ya kutaka kuzuia uporwaji wa uchaguzi.
Hongera zimwendee mwenyekiti CHADEME Dodoma kwa kuyaibishabma ccm na polisi wao.

Hongera nyingi zimqendee Lissu kwa kusimama kishujaaa kuyakataa maridhiano ndani na nje.

Hongera Lema ulisema hadhaeani kywa mwenyekiti awe amakini na hayo maridhiano.

Note: dawa ya ccm ni fimbo kama ile Ndugai aliyomtandika mpinzani wake hadi kuzimia😅
 
Polepole tutaelewana mbowe ndo msaliti mkubwa wa chawa na wapenda mabadiliko wote
 
Walimuonya watu hakusikia, including lissu. Is why watu wanamtaka aende out
Chadema tunaumizana wenyewe tu.....naungana na Lissu aliyesema tulifanya makosa makubwa kuweka Imani yetu kwa huyu mama...sasa Chatu ameshatumeza nusu, kitakachosaidia ni mabadiliko ya haraka....
 
Hii mifano mingine,kwahiyo unataka kusema mjinga hapo ni nani...
 
Unamlaumu Samia wakati waliofanya hayo mnawajua
Mbona hela zetu za kodi zikitumika kwenye miradi mnamshukuru Samia kwa kutoa fedha hizo huku mkijua siyo kweli? Sasa kwanini asilaumiwe pia kwa makosa ya watendaji wake?
 
Hakuna kosa lolote watu wameikataa chadema kwa vitendo
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Lema ameshakisaliti chama! Kweli lema ni mtu wa kukosa hata mtaa mmoja Arusha kati ya mitaa 154?? Kilichonichekesha CCM na umburura wao, kuna mtaa mwenyekiti kapata kura 1,200 lakini waliojiandikisha walikuwa 300 sasa anayedanganywa hapa ni Samia au CHADEMA??
 
Tutajie mtaa huo?Bila huo ushahidi utakuwa mzushi tu.Wewe ndio umeleta hayo madai kawa hiyo burden of proof itakuwa juu yako.
 
Mwenyekiti Mbowe, kwa kiasi kikubwa, bila ya kuwahusisha viongozi wenzake na wanachama, ndiye aliyeingia kwenye maridhiano bandia na Samia. Na ni yeye, ndiye mara nyingi aliwashawishi wanachama na viongozi wenzake kuwa maridhiano yalikuwa na faida na dhamira njema.

Leo kila mmoja ana uhakika kuwa maridhiano yale na 4Rs ulikuwa ni utapeli wa hali ya juu kwenye siasa.

Mariadhiano ulikuwa ni mchezo wa mfugaji wa kuku wa kienyeji anayetafuta kuku wa kumchinja, kuku yupo nje, anamrushia mtama ndani ya chumba, kuku mjinga anaamini kuwa anapendwa sana ndiyo maana amepewa chakula ndani ya nyumba, anaingia ndani, kisha mfugaji anafunga mlango, anamkamata na kwenda kumchinja. Maskini kuku huyu mjinga, siku aliyoamini sasa anapendwa na kuthaminiwa sana, kumbe ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa uhai wake. Anauawa bila kelele, bila hata kuku wenzake waliopo nje kusikia, bila ya kuwa na uwezo hata wa kukimbia.

Mazingira ni magumu sasa kuliko hata wakati kabla ya maridhiano haya bandia. Mwaka 2019, walipora tu uchaguzi, lakini hakuna waliotekwa wala kuuawa wala kuumizwa. Uchaguzi wa mwaka huu, wamepora uchaguzi, wameua na kuwaumiza wote walioonesha dalili ya kutaka kuzuia uporwaji wa uchaguzi.
Mbowe anatakiwa aondoke kwenye hyo nafas kuepusha chadema kuendelea kudidimia
 
Mariadhiano ulikuwa ni mchezo wa mfugaji wa kuku wa kienyeji anayetafuta kuku wa kumchinja, kuku yupo nje
 
Back
Top Bottom