Ni kweli unayoyasema kuwa watanzania ni waoga wa kupigania haki.
Lakini ufahamu kuwa ni aheri tungebakia katika mazingira tale yale ya kabla ya maridhiano bandia.
Wakati ule licha ya watanzania kukosa ujasiri kupigania haki zao, lakini CHADEMA na ACT, walifanikiwa kuifanya Dunia nzima kufahamu kuwa Tanzania na watanzania wapo kwenye utawala gandamizi. ile ilikuwa ni hatua kubwa sana na muhimu. Ni kutokana na mazingira hayo, kulikuwa na pressure kubwa ya kimataifa ambayo ilifikia mpaka Samia kulazimika kumtoa Mbowe kutoka gerezani. Kutokana na ugandamizaji, jamii ya kimataifa ilisitisha misaada kadhaa kwa Tanzania. Mataifa mengi rafiki yalisitisha misaada kwa Tanzania. Msaada wa MCC ulifutwa, msaada wa jumuia ya Madola ulifutwa. Msaada wa kibajeti kutoka jumuiia ya Ulaya, ulipunguzwa sana.
Mazingira hayo magumu ndiyo yaliyomlazimisha Samia kutafuta maridhiano bandia. Akayatumia maridhiano hayo bandia kujitangaza kimataifa. Na CHADEMA ikatumika kama shahidi wa Samia kuwa utawala wake unaheshimu demokrasia na haki za binadamu.
Bila ya maridhiano yale, kibano cha jumuia ya kimataifa kingeendelea na hata kuongezeka, hali ambayo ingeweza kuwalazimisha watawala dhalimu kusalimu amri.
Leo kuna kazi kubwa kurudi kwa jumuia ya kimataifa mliyoiaminisha kuwa mambo ni mazuri, halafu ukawaambie mambo siyo hivyo. Unaweza kupuuzwa.
..kwani jumuiya ya kimataifa hawaoni kinachoendelea?
..binafsi nadhani kuendelea kumlaumu Mbowe ni jitihada za kukwepa kukabiliana na Samia na Ccm yake.
..Kikatiba Samia ndiye Waziri wa Tamisemi kwasababu wizara hiyo iko chini ya Ofisi ya Raisi. Mchengerwa na Naibu Waziri tu ktk wizara hiyo.
..Sasa uchaguzi umevurugwa na Tamisemi kwanini hatumlalamikii Samia na serikali badala yake tunamshutumu Mbowe?
..Hivi kutenda haki ktk chaguzi zetu kunahitaji maridhiano? Je, Mbowe alimshikia bastola Samia ili akitekeleza falsafa yake ya 4R?Mbowe anahusika vipi na maamuzi ya Bunge la Ccm kupuuza maoni ya wadau kuhusu kuunda Tume Huru ya uchaguzi?