Kikao Cha Kamati Kuu, kwenye Habari ya Maridhiano, Mbowe akiri alifanya kosa kubwa

Kikao Cha Kamati Kuu, kwenye Habari ya Maridhiano, Mbowe akiri alifanya kosa kubwa

Ni kweli unayoyasema kuwa watanzania ni waoga wa kupigania haki.
Lakini ufahamu kuwa ni aheri tungebakia katika mazingira tale yale ya kabla ya maridhiano bandia.

Wakati ule licha ya watanzania kukosa ujasiri kupigania haki zao, lakini CHADEMA na ACT, walifanikiwa kuifanya Dunia nzima kufahamu kuwa Tanzania na watanzania wapo kwenye utawala gandamizi. ile ilikuwa ni hatua kubwa sana na muhimu. Ni kutokana na mazingira hayo, kulikuwa na pressure kubwa ya kimataifa ambayo ilifikia mpaka Samia kulazimika kumtoa Mbowe kutoka gerezani. Kutokana na ugandamizaji, jamii ya kimataifa ilisitisha misaada kadhaa kwa Tanzania. Mataifa mengi rafiki yalisitisha misaada kwa Tanzania. Msaada wa MCC ulifutwa, msaada wa jumuia ya Madola ulifutwa. Msaada wa kibajeti kutoka jumuiia ya Ulaya, ulipunguzwa sana.

Mazingira hayo magumu ndiyo yaliyomlazimisha Samia kutafuta maridhiano bandia. Akayatumia maridhiano hayo bandia kujitangaza kimataifa. Na CHADEMA ikatumika kama shahidi wa Samia kuwa utawala wake unaheshimu demokrasia na haki za binadamu.

Bila ya maridhiano yale, kibano cha jumuia ya kimataifa kingeendelea na hata kuongezeka, hali ambayo ingeweza kuwalazimisha watawala dhalimu kusalimu amri.

Leo kuna kazi kubwa kurudi kwa jumuia ya kimataifa mliyoiaminisha kuwa mambo ni mazuri, halafu ukawaambie mambo siyo hivyo. Unaweza kupuuzwa.
Mbowe anafanya kazi kubwa sn kupambana na haya mashetani kwa mbinu zote
 
Mimi nashangaa watu kudai kuwa Mbowe aondoke lakini viongozi wengine wabaki! Hivi ni mawazo gani mapya unategemea kutoka kwa watu ambao wameshirikiana nae siku zote? Wanakuwa kama wale waliotegemea CCM itabadilika kwa sababu kiongozi wake mkuu amebadilika. Wanasahau kuwa CCM ni taasisi na kwenye suala la kushika dola kwa namna yeyote ile wote wanaimbq nyimbo moja.

Aidha, ukiona mpinzani wako anakuambia kuwa utamshinda ukimuondoa kapteni wako wa sasa ujue kuna tatizo. Chadema ime perform beyond expectations ukizingatia madhila iliyopitia.

Ni Mbowe na viongozi wenzake ndio wamekiwezesha kubaki imara. Kwenye hilo anatakiwa ashukuriwe, sio kubezwa.

Amandla...
 
Mwenyekiti Mbowe, kwa kiasi kikubwa, bila ya kuwahusisha viongozi wenzake na wanachama, ndiye aliyeingia kwenye maridhiano bandia na Samia. Na ni yeye, ndiye mara nyingi aliwashawishi wanachama na viongozi wenzake kuwa maridhiano yalikuwa na faida na dhamira njema.

Leo kila mmoja ana uhakika kuwa maridhiano yale na 4Rs ulikuwa ni utapeli wa hali ya juu kwenye siasa.

Mariadhiano ulikuwa ni mchezo wa mfugaji wa kuku wa kienyeji anayetafuta kuku wa kumchinja, kuku yupo nje, anamrushia mtama ndani ya chumba, kuku aliyekosa ung'amuzi, anaamini kuwa anapendwa sana ndiyo maana amepewa chakula ndani ya nyumba, anaingia ndani, kisha mfugaji anafunga mlango, anamkamata na kwenda kumchinja. Maskini kuku huyu mjinga, siku aliyoamini sasa anapendwa na kuthaminiwa sana, kumbe ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa uhai wake. Anauawa bila kelele, bila hata kuku wenzake waliopo nje kusikia, bila ya kuwa na uwezo hata wa kukimbia.

Mazingira ni magumu sasa kuliko hata wakati kabla ya maridhiano haya bandia. Mwaka 2019, walipora tu uchaguzi, lakini hakuna waliotekwa wala kuuawa wala kuumizwa. Uchaguzi wa mwaka huu, wamepora uchaguzi, wameua na kuwaumiza wote walioonesha dalili ya kutaka kuzuia uporwaji wa uchaguzi.
Mbowe alifanya upuuzi mkubwa sana. Ngoja alipe gharama za upuuzi aliofanya.
 
Wameanza uongo. Watakubaliana waseme wao ndio washindi ccm imewaibia kura. Kisha wataenda ubalozi wa marekani na umoja wa ulaya kutoa taarifa ya uongo na wao balozi watajidai ni kweli vibaraka wao ndio washindi. Tutegemea sugu akiwa na mawani makubwa ya giza chain shingoni na suruali mbano kupewa yeye kuongoza ujumbe ubalozi wa marekan.🇺🇲😆
 
Unamlaumu Samia wakati waliofanya hayo mnawajua
Mjinga wewe...

Wewe kumbe hata hujui kuwa Waziri wa TAMISEMI ni Bi. Samia Suluhu Hassan...!

Na hata hujui kuwa TAMISEMI ndiyo iliyoandaa, kuratibu na kusimamia kila hatua ya ubaya na uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi huu wote..!

Utaachaje kumng'ong'a na kmshutumu bibi huyu tena Mzanzibari kwa uchafu na uharibifu aliwafanyia Watanganyika...?

Na obvious, kwa jinsi ulivyo bado mjinga, bila shaka moyoni mwako umeshaanza kubisha kuwa waziri wa TAMISEMI si Bi. Samia Suluhu Hassan bali ni Mohamed Mchengerwa, mkwilima wake aliye na kifua kipana kwa mama mkwe wake...!!

Shauri lako, kama bado unaamini hivi, basi endelea kuishi na ujinga wako huo.................!!!
 
Kufa kila mtu atakufa, hata wanaofanyiwa ubaya nao watakufa. Kwahiyo suala la kifo lisitumike kuwatisha baadhi ya watu.
Ukiwaua wenzako unategemea uishi milele..? Mwisho wa maisha yote ni ubatili mtupu
 
Back
Top Bottom