JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Sasa huu ni upuuzi,anayetoa maagizo kwa serikali ndio huyo huyo mkuu wa serikali sasa anajipa maagizo?Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:
1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.
Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
Kwanini asitekeleze kwanza harafu aende kwenye chama kutoa taarifa?