Kikao Kamati Kuu ya CCM Kimeitaka Serikali Kuwachukulia Hatua Haraka Waliotajwa ripoti ya CAG na TAKUKURU

Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
WATAPANDA KIZIMBANI AU VYEO?
 
Kwani Kuna mtu karajea na rpoti ya CAG?
Mkuu wa nchi atoe presidential decree hao wote waliotajwa kuhusika katika ubdhirifu wa mabilioni ya walipa kodi wafungwe maisha , this is very possible kama sheria ya kuwashughulikia ina mapungufu haswa waliotajwa kwenye repoti ya CAG ....
 
Iko hivi bosi. Serikali yetu inaongozwa na mifumo, sera, sheria, taratibu etc katika utendaji kazi na hatimaye repoti. Linapokuja suala la ukaguzi kinachoangakia je kama ni sera, sheria, utaratibu, mifumo ya kimaamuzi ilifuatwa. Chukulia tu mfano kwenye taasisi fulani unakuta mtia sahihi ya malipo fulani kikomo chake ni mil 50, ikizidi hapo labda anatakiwa atie sahihi mkuu wa taasisi na huo unaweza kuwa utaratibu upo, ila unakuta alitia sahihi huyo asiyeruhusiwa na CAG akija atasema utaratibu haukufuatwa. Mfano mwingine, unakuta labda serikali imepeleka hela kwa ajili ya ujenzi wa kitu fulani halafu wakabadili matumizi bila kikao cha bodi husika maana yake CAG akija hapo atasema kuna matumizi mabaya ya hela bil 5 etc. Wakati mwingine wakaguzi wanaomba documenti labda zimepotea au wahusika hawakuleta receipt na CAG asipoipata hiyo receipt tayari hiyo ni hela inahesabika haijulikani ilipo. Kwa ujumla serikalini kuna vitu vingi, tusikimbilie kulaumu
Kwanini doc zipotee?? Kuna watumishi waliajiriwa kwa kazi hiyo ya kupoteza doc? aacha kutetea uhozo.
 
Na iende kuwa hivyo kwa wote waliohusika bila kulindana kwa matamko yasio na tija. Otherwise upigaji uendelee tuu !!
 
Namba 3, nimeipenda kuna baadhi ya wakubwa ambao hawamsadii vzr Namba1, badala yake vyeo na nafasi zao wanazitumia kuwaonea waliochini kabisa! hii sio Sawa.
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
Nchi ili kuinyoosha inahitajika kiongozi mwenye uthubutu wa Sokoine ama JPM ili kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma. Angalizo tu ni kuwa tusimuangalie JPM katika upande wa mapungufu yake, bali kile alichokisimamia kwa haki.

Kuorodhesha madudu ni kitu kimoja, lakini kuwachukulia wahusika hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafailisi mali walizozichuma kwa njia za kifisadi ni njia nyingine. Kwani hili litakuwa ni funzo nzuri kwa wengine wenye tamaa ya ufisadi.

Kupiga kelele tu bila kuchukua hatua zinazo onekana, ni sawa kuzidi kulikarabati kaburi la marehemu kwa nakshi za thamani, huku ukiiacha familia yake ikifa kwa kiu na njaa.
 
Asante kwa taarifa
====
Ukichimama nchale ,ukikimbia nchale!!!
 
Kumbe Chama na Serikali boss ni yule yule,ni sawasawa na pande mbili ya shiling.Tutasubiri Sana kupata mrejesho wa hatua zitakazochukuliwa.ni kitu kimoja hizi taasisi.wanatuperemba wa tz
 
CCM ni kimbilio la Majizi na ni CHAKA lao la kujificha.
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
😂😂😂😂. Kwa hiyo samia kaitaka serikali kueachukulia hatua mafisadi 😂😂😂😂😂! Aisee hichi ni kituko cha mwaka….Samia kaitisha kikao cha kamati kuu kuitaka serikali kuwachukulia hatua walio husika au kutajwa na CAG kwa ubadhilifu wa mali!

Kupata vichekesho hivi bonyeza #Tanzania…..😂😂😂
 
Tunasubiri tuone !!
 
😂😂😂🇹🇿🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom