Muda mwingine muwe mnaona aibu kukomenti upimbi
Hasara ya miaka 9 ya ATCL
Hasara ya miaka 7 ya NHIF
Hasara ya miaka 7 TTCL
Hasara ya miaka 7 ya Mchechu
Hasara ya miaka 6 ya Makamba
Hasara ya miaka 7 ya Tanesco
Weka Bandari hapo
Hasara ya Manyanga
Msitufanye Watanzania kuwa wajinga..Ukichukua hasara ya mashirika yote ya Umma kwa Miaka 10 inaweza kuwa sawa na nusu ya Deni la Taifa au hata zaidi yake.....
Muwe mnaona aibu enyi Wazalendo Uchwara..
Ni kweli kabisa Kama tukisimamia Mali zetu na mashirika yetu Vizuri Hatukua na sababu ya kuomba misaada ya Miswaki na dawa za Meno za mia Tano kutoka Kwa taifa ovu kama Marekani na Washirika wake.
Watanzania tuamke Sasa kuwakataa Mafisadi na Washirika wao.
Rais Ana mamlaka makubwa sana. Ateue watu makini kutoka Hata Vyama vya Upinzani. Mchawi mpe Mwana amlee.
CCM itadumu Kwa kulijenga taifa. Lakini Kwa Hali ya Sasa CCM inakula taifa na kulibomoa. Ni mchwa ndani ya nguzo ya MTU. Ni balaa tupu.
Oooh , TANU yajenga nchi , TANU Oooh TANU yajenga nchi. Tuliimba zamani hizo tukiwa wanafunzi Wa Shule ya Msingi na chipkizi .
Kwa Sasa ni CCM yabomoa nchi na kugawana Fito.
Tangu lini kampuni ya Simu ya Serikali inapata hasara. Hata kibanda Cha Mpesa kama MTU anamtakia mzuri hapati hasara bia Wizi.
Hasara ni matokeo ya Wizi na ufisadi.
Viwanda vya sementi eti vilipata hasara . Mameneja Badala ya kufungwa au kufukuzwa KAZI walihamishiwa wizarani na wengine kwenye Bodi na wengine kuwa Wakurugenzi . WEZI wakazawadiwa vyeo. WEZI wanatabia ya kuwa na mtandao Mkubwa kutokana na kutumia vibaya pesa za umma kuwahonga walioko juu na kuwakirimu wanapotembelewa nao ndio Maana Hata kamati za Bunge zinakua dhaifu kutokana na Rushwa.
Akija waziri au katibu Wa wizara Fulani kutembelea na kukagua shirika au mradi Fulani anapokelewa na zawadi kibao . Kama ni MTU anayependa uzinzi basi ataandaliwa na wanawake Wa kutosha . Hapo ni kubebana tu Hata akiona madudu na ufisadi akiondoka anakumbuka starehe alizokula kwenye ziara na SIO vinginevyo. Utasikia Nakuja Mbeya niandalie Mwanamke Wa kinyakyusa siajwahi kula mnyakyusa. Akienda Moshi mchaga ,akiendaa Kagera Mhaya. Anatengeneza safari za kijinga kijinga kutafuta pesa na starehe.Mashirika yanakufa ,anapata pesa anafanya starehe anajijenga na familia yake.
Hapa pia tutakubaliana wazi kuwa Hata Kukimbiza Mwenge ni kichaka Cha kumaliza pesa za umma Kisha watu kwenda kuomba Misaada ya miswaki.
Mwenge ukipita nchi nzima ukimulika Kila Sehemu lakini Halmashauri nyingi ni Wizi mtupu. Miradi mingi ni ubabaishaji na Wizi mtupu. Mwenge unamulika nini Sasa. Mwenge kama Mkurugenzi hajaandaa fungu la wakimbiza Mwenge basi atakaguliwa na kuibuliwa madudu na kuchaguliwa kuwa hafai kuendelea na KAZI.
Tuachane na Mwenge Wa Kila mwaka unaipa taifa hasara Kubwa. Hizi ni Zama za wapigaji na SIO Wazalendo . Enzi hizo mwange ulikimbizwa na Wazalendo Kwa gaharama ndogo sana.Mkuu Wa Wilaya alikua anapanda gari moja na wakuu Wa Idara mbalimbali Wilayani lakini kwa Sasa Wilaya moja inaweza ikatoa magari 40 ya Kukimbiza Mwenge . Yatatolewa Kila mkuu Wa Idara na gari lake na mengine ya KUKODISHA . Kwa Sasa gharama za kuwagharamikia wakimbiza Mwenge nchi nzima ni kubwa sana . Zinatosha Kununua miswaki na dawa za meno Kwa watoto mashuleni bila kutegemea Misaada ya mabeberu wenye agenda zao mbovu.
Mwenge uwekwe kwenye Nakumbusho na ukimbizwe Kila baada ya miaka Kumi ikiingia Awamu nyingine au Rais mwingine na SIO Kila mwaka .