BIN NUN
JF-Expert Member
- May 23, 2014
- 3,477
- 7,085
Mpaka leo hii, hiki cheo kiliwahi kushikiliwa na watu 2 tuu tena kwa sababu maalumu sana na nyeti, na zenye maslahi mapana kwa taifa.Jamani jamani mbona watu ni waongo hivi? Unabuni kutoka kichwani na kuandika kama ni tukio la ukweli? Salim alishika lini huu wadhifa? Ni Mrema pekee aliyewahi kushika.
1. Dr. Salim Ahmed Salim.
Salim alipewa cheo hiki 1986 mpaka 1990, kwasababu aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja enzi za Mwalimu Nyerere (Baada ya Kifo cha Sokoine), hivyo baada ya Rais Mwinyi kuingia akaona ni Busara Waziri Mkuu wake aliyemteua Joseph Sinde Warioba awe na Naibu ambaye ni Salim.
2. Augustino Lyatonga Mrema
Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema alitumia ujuzi wake kama KACHERO WA USALAMA WA TAIFA, kudadisi na kukamata wezi na wala rushwa katika kila wizara ya Serikali aliyogundua mambo si shwari.
Hali hiyo ikawaudhi baadhi ya mawaziri wenzake serikalini. Wakamwambia "MREMA USIVUKE MIPAKA YAKO, Wewe ni waziri kama sisi na huwezi kuingilia mambo ya ndani kwenye wizara zetu bila kujadiliana nasi kwanza." Mrema anasema alikomaa nao, na ndipo Rais Mwinyi akagundua dhamira yake njema.
Rais Mwinyi mnamo mwaka 1992 akamuongezea cheo kipya Mrema. Akamteua kuwa NAIBU WAZIRI MKUU.
1993, Mrema alipopewa Unaibu Waziri Mkuu anasema "wenzangu walianza kuniogopa na kuniheshimu. Hata kama wanaenda sehemu walikuwa wanalazimika kusimama kwanza ili kupisha msafara wenye ving'ora wa Naibu Waziri Mkuu."
Akiwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu alishughulika na kila aina ya ubadhirifu, wizi na magendo kwa kadri alivyopata taarifa. Akawa waziri maarufu sana kwa wananchi mijini na Vijijini.
"Rais Mwinyi kila akirudi kutoka mikoani alikua akiniita na kuniambia Mrema nimetoka kwenye ziara, wananchi wanakusalimia sana. Unafanya kazi nzuri," alinisimulia Mzee Mrema katika mahojiano hayo ya MSUMARI WA MOTO.
Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu Mrema zama hizo za uwaziri wake wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu ilikua ni kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi kwa nguvu za wananchi ili kuimarisha ulinzi lakini pia "Tajirika na Mrema" - UTOAJI WA ZAWADI KWA WATU WANAOFICHUA WAHALIFU.