Kikatiba Rais Samia yuko sahihi kumteua Naibu Waziri Mkuu

acha kulisha watu pumba ni wapi katiba imetamka kutakuwa na naibu waziri mkuu? ujinga nao ni kipaji naona una kipaji
 
So refreshing.

Yaonekana ni cheo ambacho ni Ceremonial!
 
Hakina faida yoyote kwa wananchi ni matumizi mabaya ya kodi . Wizara ya madini nani kapewa? Kwa hiyo nishati imepelekwa ofisi ya waziri mkuu ili kumwongezea presha?
 
Mkuu hoja nyingi zinahoji uhitaji wa nafasi hiyo kwa sasa na sio uhalali, kimsingi sio hoja bali hofu juu ya hatimae ya waziri wetu mkuu, kuna tatizo gani mpk kuwekewa msaidizi? Na msaidizi huyo kwann amekuja sasa ambapo nchi iko kwenye tension ya mkataba wa IGA na bandari zetu? Je, ni kutaka kuwatuliza maaskofu kwa kumweka muumini wao kwenye majukumu mazito ili waweze kupitishia hoja zao kwake kwenda Baraza la mawaziri? Au waziri wetu mkuu hatoi ushirikiano kwa mamlaka kuhusu mambo yanayoendelea na anawekwa pembeni kinamna ili mambo yaende? Mambo ni mengi, maswali ni mengi, hofu ziko pande zote.
 
Siku hizi huweki namba ya simu utapishana na pdf
 
Hana kosa chifu Hangaya🤣🤣🤣
 
Kumbe anaweza kufuta hata cheo cha Waziri Mkuu na kuanzisha kingine hakuna hata wa kuhoji? hii katiba ni mbovu sn na ya hovyo
Hii katiba mbovu tutaisoma na kuelimisha Umma kwa kwa miaka mitatu mfululizo halafu ndio tutaifuta

niombee Ndugu yangu niingie kwny historia ya Kikosi kazi ya kuelimisha Katiba inayoenda kufutwa walau nipate umate mate wa kuzeekea
 
Hapo kwa Biteko wametupatia sana Watanzania. Huyu ni mchapakazi hasa.
 
Ni kweli na Rais Nyerere aliwahi kusema katiba ya tanzania inampa Rais mamlaka za kifalme na kisultani. Mathalani mapema mwaka huu tumeona Jaji wa Mahakama ya Rufaa akiteuliwa kuwa mshauri wa Rais Ikulu. Hapa izingatiwe kwamba serikali ina Wizara nzima ya katiba na sheria na Mwanasheria Mkuu wa serikali! Sasa huyu jaji anayeajiriwa Ikulu kutoa ushauri kwa Rais inakuwaje wakati katiba imetenganisha mihimili ya utawala wa nchi?
 
Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu


Doto Mashaka Biteko - Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.



Prof. Joyce Lazaro Ndalichako - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)



Jenista Joackim Mhagama - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
 
Dah sasa hapa katiba imenajisiwa au imejinajisi yenyewe?
Imenajisiwa maana mteuzi amesoma Katiba kama gazeti wakati Katiba ni sheria inapaswa kusomwa ukizingatia na vifungu vingine ndo maana inaandika "NA KWA KUZINGATIA..."
 
So refreshing.

Yaonekana ni cheo ambacho ni Ceremonial!
Kuwa na Rais na washauri àmbao wanaweza kumgeuza Rais watakavyo ni hatari. Tusubiri Sasa huyu Biteko atakapomaliza Muda wake atalipwa kama DPM au kama Waziri?
 
Hii katiba mbovu tutaisoma na kuelimisha Umma kwa kwa miaka mitatu mfululizo halafu ndio tutaifuta

niombee Ndugu yangu niingie kwny historia ya Kikosi kazi ya kuelimisha Katiba inayoenda kufutwa walau nipate umate mate wa kuzeekea
Upo sahihi 220,000 per day sihaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…