Kikokotoo(Mafao): Rais Samia anastahili pongezi kwa hili

Kikokotoo(Mafao): Rais Samia anastahili pongezi kwa hili

Huu ndio upuuzi wenyewe. Ulipwe 33% alafu nyingine ulipwe kwa mwezi. Sasa kama mtu una uwekezaji wako unategemea pesa ya uhakika ndio umefeli , serikali iache kufanya raia wategemezi.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
Siyo kwamba utapewa kila mwezi. Wanakupatia kila baada ya miezi 6 baada ya kuzungushwa huku ukiwa na kisukari kikali na homa kali. Ukichukua miaka 2 tu tayari unaenda kaburini
 
Mimi naona wangetoa uhuru kwa wastaafu kuchagua aina ya kikokotoo wakipendacho baada ya kustaafu. Mfano mstaafu anayetaka kupewa hela zake zote, apewe! Na yule anayetaka kupewa hiyo 33% kwanza, apewe! Mtu asipangiwe matumizi ya hela yake.

Hii mambo ya kulazimisha kulipana hela pungufu, ni upuuzi. Mbona hao Wabunge hicho kikokotoo hakiwahusu? Au wao wanajiona wana uwezo mkubwa wa kutunza pesa kuliko wastaafu wengine?

Serikali iache mambo ya wizi kwa wastaafu.
 
Siyo kwamba utapewa kila mwezi. Wanakupatia kila baada ya miezi 6 baada ya kuzungushwa huku ukiwa na kisukari kikali na homa kali. Ukichukua miaka 2 tu tayari unaenda kaburini
Ndilo lengo Lao, wengi hawatachukua hata hiyo 33% ya pili na watakufa kabla!
Pesa za wastaafu wao wanajengea madaraja na hawana nia ya kuzirudisha.

Kikokotoo hiki, kiwahusu, wabunge pia na vigogo wote!
Ili tuamini Sisi sote ni binadamu ni Sawa na Africa ni umoja!
 
Siyo kwamba utapewa kila mwezi. Wanakupatia kila baada ya miezi 6 baada ya kuzungushwa huku ukiwa na kisukari kikali na homa kali. Ukichukua miaka 2 tu tayari unaenda kaburini
Hapa tz mambo ni shaghala baghala
Hela ya mstaafu anayokatwa pindi akiwa kazini anapangiwa namna ya kuipata
So far hao workers association wenyewe hawaja staafu thus y
Mtu anarudi kijiji hizo gharama za nenda ruudi zitabebwa na nani
 
Haki yakwangu halafu matumizi ananipangia mwingine hivi Ni vioja hili zoezi litadumu kwa muda mfupi tu baada ya hapo watarudisha utaratibu wa mwanzo mpe mtu chake afe nacho mwenyewe sio kumtunzia kwani mliambiwa wahusika hawajui kutunza hela zao?
 
Hii ni moja kati ya sheria mbovu na mbaya kuwahi kuwepo katika nchi zote duniani! Utekelezaji wa sheria hii ni kinyume na haki za binadamu.
Kwanini iwe hivyo ilihali ni haki ya mstaafu? Wenye kuitunga hii sheria waliwahi kufanya utafiti wowote na kutaja nchi yoyote duniani inayotumia sheria hii? Kama Kuna nchi hiyo wanaweza kututajia faida na hasara zake Kwa mhusika?
Binafsi siuoni Kama hilo jambo litakuwa na afya Kwa serikali na hata mstaafu badala yake wangewapa wastaafu elimu hata ya kununua hisa kwenye mabenki na hata Amana za serikali Kama wanaona atakitumia kiinua mgongo chake vibaya na siyo kumlipa Kama matone ya drip!
Waziri mweñye dhamana irudishe sheria hii bungeni ikafutwe haraka Sana kwani kuiacha inakwenda kusababisha vifo na hata umaskini Kwa wafanyakazi waliojitoa maisha Yao kuijenga nchi hii Kwa uvumilivu mkubwa wa kulipwa mishahara isiyokidhi mahitaji ya mwezi!
Nimwombe mh. Rais aifute hii sheria ikimpendeza na aache kumsikiliza huyo Jenister Mhagama ambaye Hana Nia njema na wastaafu pamoja na wafanyakazi wa taifa hili kwani ndiye aliyeipeleka sheria hii bungeni kutafuta kick Kwa Magufuli! Namlaani Kwa Imani yangu akaaibike na kupata Kila lililo baya Kwa kuwadhulumu wazee wetu Hawa ambao anawalipa mateso Kwa uzalendo wao wa nchi Yao!
 
Sasa kama mmetaka tozo za daraja la kigamboni zishuke mlitegemea wafanyaje🤣
 
Huu ndio upuuzi ambao wanasiasa wanasababisha kwenye hii nchi. Kuweka matabaka kwenye jamii.

Wao ( Mbunge, Mkuu wa mkoa na bosi ) wao haiwahusu ila wafanyakazi ambao ni tabaka linalotawaliwa.

Ni wazi sasa hakuna wa kuwasemea wasio na sauti. Shame on you politicians!
 
Dah, 'mwamba' amejua kutuachia mateso......

Jamaa zangu fulani hivi kimyaaa hapa, ila mama akipokea tuzo na kuzindua miradi utawasikia, 'r.i.p jpm!'
 
Kwa hiyo mstaafu akifariki ule mwaka wa kwanza.....serikali inatia kibindoni 67% ya pesa ya marehemu mstaafu huku watoto wake wakiambulia vumbi, sijawahi kuona serikali ya hovyo kama hii inayotolea udenda hadi pesa za wazee........
 
Back
Top Bottom