Fasta fasta
JF-Expert Member
- Feb 15, 2011
- 1,125
- 725
Hii sheria ni ya kipuuzi. Ulaya baadhi ya nchi ninazozifahamu wanautaratibu mzuri Sana.Hii ni moja kati ya sheria mbovu na mbaya kuwahi kuwepo katika nchi zote duniani! Utekelezaji wa sheria hii ni kinyume na haki za binadamu.
Kwanini iwe hivyo ilihali ni haki ya mstaafu? Wenye kuitunga hii sheria waliwahi kufanya utafiti wowote na kutaja nchi yoyote duniani inayotumia sheria hii? Kama Kuna nchi hiyo wanaweza kututajia faida na hasara zake Kwa mhusika?
Binafsi siuoni Kama hilo jambo litakuwa na afya Kwa serikali na hata mstaafu badala yake wangewapa wastaafu elimu hata ya kununua hisa kwenye mabenki na hata Amana za serikali Kama wanaona atakitumia kiinua mgongo chake vibaya na siyo kumlipa Kama matone ya drip!
Waziri mweñye dhamana irudishe sheria hii bungeni ikafutwe haraka Sana kwani kuiacha inakwenda kusababisha vifo na hata umaskini Kwa wafanyakazi waliojitoa maisha Yao kuijenga nchi hii Kwa uvumilivu mkubwa wa kulipwa mishahara isiyokidhi mahitaji ya mwezi!
Nimwombe mh. Rais aifute hii sheria ikimpendeza na aache kumsikiliza huyo Jenister Mhagama ambaye Hana Nia njema na wastaafu pamoja na wafanyakazi wa taifa hili kwani ndiye aliyeipeleka sheria hii bungeni kutafuta kick Kwa Magufuli! Namlaani Kwa Imani yangu akaaibike na kupata Kila lililo baya Kwa kuwadhulumu wazee wetu Hawa ambao anawalipa mateso Kwa uzalendo wao wa nchi Yao!
Kila mwananchi akifikisha miaka 60 anakula pension yake. Wameweka kiwango kidogo Cha kuchangia anzia ukiwa kijana kuanzia miaka22.
Yaani hakuna Cha mfanyakazi waserikali au dalali au bodaboda. Wote wanachangia huu mfuko na wanapata pension yao na kila mwezi wanakula posho Safi.
Ndiyo maana wazee ndiyo wanatunza familia za vijana wao. Na wanapesa.
Na ushauri.