Kikokotoo(Mafao): Rais Samia anastahili pongezi kwa hili

Kikokotoo(Mafao): Rais Samia anastahili pongezi kwa hili

... hivi pensheni ya kila mwezi ni % ngapi ya mshahara mtumishi aliostaafia wakuu? Au kuna fomula tofauti? Kama ipo, naomba kuijua ndugu zanguni.
Naongezea maswali: sio kwamba asilimia 33.3 mkupuo, halafu asilimia 66.6 unagawa kwa miaka 12.5 ndipo unapata ya kila mwezi? Au ndio kuna formula ya kubakiza kwao?
 
Naongezea maswali: sio kwamba asilimia 33.3 mkupuo, halafu asilimia 66.6 unagawa kwa miaka 12.5 ndipo unapata ya kila mwezi? Au ndio kuna formula ya kubakiza kwao?
... na je, baada ya hiyo miaka 12.5 kama mstaafu angali hai fungu lake linakuwa limeisha halipwi tena? Kama ataendelea kulipwa, why 12.5 years? Sio kuchuriana huku?
 
Siyo kwamba utapewa kila mwezi. Wanakupatia kila baada ya miezi 6 baada ya kuzungushwa huku ukiwa na kisukari kikali na homa kali. Ukichukua miaka 2 tu tayari unaenda kaburini
[emoji45][emoji45][emoji45][emoji45]inauma sana. Mtu apewe mzigo wake apange mikakati yake ya maisha.

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Huu ndio upuuzi ambao wanasiasa wanasababisha kwenye hii nchi. Kuweka matabaka kwenye jamii.

Wao ( Mbunge, Mkuu wa mkoa na bosi ) wao haiwahusu ila wafanyakazi ambao ni tabaka linalotawaliwa.

Ni wazi sasa hakuna wa kuwasemea wasio na sauti. Shame on you politicians!
Waambie wabunge na wao wachuku 33% alafu zinazobaki wapewe kwa mwezi uone hiyo vita itatokea

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la nchi hii mambo ya muhimu tunaona ni ya wanasiasa na hayatuhusu. Ukimwambia mfanyakazi kuhusu katiba mpya anasema haimuhusu hiyo inawahusu wanasiasa. Sasa matokeo yake ndio haya wanasiasa wanapitisha mambo ambayo yana gusa haki za wafanyakazi bila wafanyakazi wenyewe hasa kushirikishwa kwenye maamuzi yanayowagusa. Laiti kungekuwa na katiba nzuri nina hakika hili lisingepitishwa. Haiwezekani mbunge apewe pesa yake yote kwa mkupuo asilimia 100% halafu mfanyakazi apangiwe tena sio kwa hiyari yake mkupuo wa 33% zilizobaki apewe kidogo kidogo tena sio zote.

Kwa kweli sio haki kabisa kwa wavuja jasho wa nchi hii. Lakini je ni nani wa kuwatetea wavuja jasho wa nchi hii? Jibu ni hakuna wa kuwatetea zaidi ya wafanyakazi wenyewe kuamua kujitetea. Ni hili lianzie la kuweka watu wenye kujali matatizo yao kwenye uongozi wa vyama vya wafanyakazi kuanzia ngazi za chini kabisa mpaka ngazi ya taifa. Vinginevyo itokee tu hisani ya baadhi ya wanasiasa na mawakili wa haki za binadamu wajitolee tu kama msaada kuwatetea wafanyakazi katika hili kupitia njia ya mahakama ili serikali ilazimishwe kubadilisha sheria hii.

Ni ukweli kabisa mara nyingi aliyeshiba hamjali mwenye njaa kwa hiyo wafanyakazi wasitegemee kabisa kuwa huo mfumo wa malipo utabadilika bila kuunganisha nguvu kupitia vyama vya wafanyakazi. Kama wanasiasa wangekuwa na nia njema kwa mfanyakazi basi wangerudisha ule mfumo wa zamani ambao mfanyakazi alikuwa anapewa asilimia 75 kwa mkupuo halafu asilimia 25 kidogo kidogo.

Wakati mfanyakazi anaenda kutaabika uzeeni kutokana na malipo kiduchu kwa mkupuo walioihujumu hiyo mifuko kwa njia moja au nyingine wapo bado maofisini na wengine wapo mitaani wanatanua badala ya kuwajibishwa na hata kuwa ndani ya kuta za gereza. Hiyo mifuko imejenga majengo mengi na vitega uchumi vingi ambayo havirudishi faida kwa mfanyakazi mstaafu japo yametumia fedha zake nyingi kuwekeza. Wakati mwingine nafikiria hayo majengo kwa nini yasipigwe mnada tu hata kwa nusu hasara halafu pesa zirudishwe kwenye mfuko zikalipe wale wazee wanaozungushwa nenda rudi nenda rudi na vibahasha vyao vya kaki vilivyochakaa wakidai mafao yao? Kwa uchungu sana nasema ipo siku kama nchi tutavuna laana kwa kuwatesa watu waliojenga hii nchi kwa machozi, jasho na damu halafu tunawalipa dhuluma pale wanapofika umri wa kudai mafao yao. Na mbaya zaidi watu wanaosababisha hiyo dhuluma wamehudumiwa na hao wazee kwa njia mbali mbali kuanzia mashuleni, vyuoni, mahospitalini, mabarabarani, n.k.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Huu ndio upuuzi ambao wanasiasa wanasababisha kwenye hii nchi. Kuweka matabaka kwenye jamii.

Wao ( Mbunge, Mkuu wa mkoa na bosi ) wao haiwahusu ila wafanyakazi ambao ni tabaka linalotawaliwa.

Ni wazi sasa hakuna wa kuwasemea wasio na sauti. Shame on you politicians!
Hao ulowataja sio waajiriwa wa kudumu
 
..Lakini je ni nani wa kuwatetea wavuja jasho wa nchi hii? Jibu ni hakuna wa kuwatetea zaidi ya wafanyakazi wenyewe kuamua kujitetea. Ni hili lianzie la kuweka watu wenye kujali matatizo yao kwenye uongozi wa vyama vya wafanyakazi kuanzia ngazi za chini kabisa mpaka ngazi ya taifa..
Vyama vya wafanyakazi hakuna kitu..
Kuna mdau kasema vilishageuka CHAWA wa watawala hivyo kazi yao ni kuunga mkono kila jambo!

Tatizo kubwa awamu hii linaanzia bungeni. Kumekuwa na watu wa aina moja tu, so hakuna wa kuhoji. Watawala watapitisha kila wanachotaka hata kama hakina maslahi kwa wananchi
 
Jana, statement toka Ikulu ilieleza kuwa Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya mafao ya Pensheni, kama ilivyoombwa na chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) siku ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi, 2022), ambapo sasa amekubali ombi la kupandisha malipo ya mafao, kutoka 25% iliyokataliwa na wadau hadi 33.3%.

Ametaka TUCTA, wizara ya fedha na Chama cha Waajiri (ATE), kuendelea kushirikiana ili kukamilisha taratibu za malipo ya mkupuo huo wa asilimia 33.3% badala ya 25% iliyokataliwa mwaka 2018.

Kanuni za Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, ziliweka kikokotoo kimoja cha asilimia 25 ambacho kiliweka usawa kwa wastaafu wote kupata mafao yenye fomula moja, tofauti na awali kulipokuwa na fomula mbili.

Kikokotoo kipya kwenye kanuni kilikuwa ni asilimia 25 kwa mafao ya mkupuo na asilimia 75 inayobaki kulipwa kama pensheni ya mwezi kwa kila mwezi hadi mwanachama atakapofariki dunia.

Hata hivyo, katika kikokotoo hicho, umri wa kuishi ulikadiriwa kuwa ni miaka 12.5, ikiwa ni umri uliokadiriwa kuwa mwanachama ataishi baada ya kustaafu.

Kwa mujibu wa kikokotoo cha NSSF ambacho kimekuwapo kwenye kanuni za shirika hilo tangu mwaka 2014, mwanachama anapostaafu analipwa asilimia 25 ya mafao ya mkupuo na kilichobaki kinalipwa kama mshahara wa kila mwezi.

Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, imetaja jumla ya mafao saba ambayo ni manne ya muda mfupi (fao la upotevu wa ajira, fao la ugonjwa, fao la uzazi na mkopo wa nyumba) na matatu ya muda mrefu ambayo ni pensheni ya uzeeni, fao la ulemavu na fao la warithi.

Kwa hili, niseme Rais Samia na serikali yake wanastahili pongezi.
Pongezi kubwa kwa mama kazi yake inaonekana
 
Dah, 'mwamba' amejua kutuachia mateso......

Jamaa zangu fulani hivi kimyaaa hapa, ila mama akipokea tuzo na kuzindua miradi utawasikia, 'r.i.p jpm!'
Kila mtu ana mema yake na mabaya yake ila jambo hili la kupangiana pensheni uileje aloo linawatesa sana wafanyakazi toka wakiwa makazini
 
Baada ya serikali kusitisha tangazo la kikokotoo mwaka 2018 sasa wamekuja na kikokotoo kipya baada ya mashauriano na waajiri.

ATE na vyama vya wafanyakazi ambapo mstaafu katika mifuko yote atalipwa asilimia 33 tu kama malipo ya mkupuo. Wale tuliokuwa tumejipanga kuchukua michango yote kwa mkupuo tujiandae.

Kwan hiki kikokotoo kinaanza lini?
 
Ufafanuzi kwa wanaujua madhara au faida zake tafadhali. Kwa maelezo hayo tuu haitoshi kujua mataafu anafaidika au anapunjwa kwa kiasi gani. Weka nyama nyama na supu tuweze kuelewa, kwa mwenye uelewa wa kutosha. Hesabu ya ulinganifu inahusika hapo
Pension ukichukua kubwa ya mkupuo monthly Pension inakuwa ndogo

Mfano ilipokuwa asilimia 50 mkupuo monthly Pension wafanyakazi walipata asilimia 25 ya mshahara wa kuondoka

Wale wa NSSF waliopewa mkupuo asilimia 25 monthly Pension walikuwa wakipata asilimia 72 ya mshahara wao wa kuondoka

Vyama vya wafanyakazi hopeless walipigana mkupuo mkubwa upande wakati monthly Pension inashuka ilitakiwa wapigania mkupuo ushuke ili mfanyakazi apokee at least hadi asilimia 80 ya pesa ya mshahara wa kuondokea kustaafu

Kudai asilimia kubwa ya mkupuo uwe mkubwa ni janga kwa wastaafu. Mbeleni wataishi kwa shida mno kwa vi monthly Pension vidogo
 
Jana, statement toka Ikulu ilieleza kuwa Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya mafao ya Pensheni, kama ilivyoombwa na chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) siku ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi, 2022), ambapo sasa amekubali ombi la kupandisha malipo ya mafao, kutoka 25% iliyokataliwa na wadau hadi 33.3%.

Ametaka TUCTA, wizara ya fedha na Chama cha Waajiri (ATE), kuendelea kushirikiana ili kukamilisha taratibu za malipo ya mkupuo huo wa asilimia 33.3% badala ya 25% iliyokataliwa mwaka 2018.

Kanuni za Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, ziliweka kikokotoo kimoja cha asilimia 25 ambacho kiliweka usawa kwa wastaafu wote kupata mafao yenye fomula moja, tofauti na awali kulipokuwa na fomula mbili.

Kikokotoo kipya kwenye kanuni kilikuwa ni asilimia 25 kwa mafao ya mkupuo na asilimia 75 inayobaki kulipwa kama pensheni ya mwezi kwa kila mwezi hadi mwanachama atakapofariki dunia.

Hata hivyo, katika kikokotoo hicho, umri wa kuishi ulikadiriwa kuwa ni miaka 12.5, ikiwa ni umri uliokadiriwa kuwa mwanachama ataishi baada ya kustaafu.

Kwa mujibu wa kikokotoo cha NSSF ambacho kimekuwapo kwenye kanuni za shirika hilo tangu mwaka 2014, mwanachama anapostaafu analipwa asilimia 25 ya mafao ya mkupuo na kilichobaki kinalipwa kama mshahara wa kila mwezi.

Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2018, imetaja jumla ya mafao saba ambayo ni manne ya muda mfupi (fao la upotevu wa ajira, fao la ugonjwa, fao la uzazi na mkopo wa nyumba) na matatu ya muda mrefu ambayo ni pensheni ya uzeeni, fao la ulemavu na fao la warithi.

Kwa hili, niseme Rais Samia na serikali yake wanastahili pongezi.
Fao la kujitoa mbona halijarejeshwa watu watoe hela zao kila mtu afe na chake??
 
Mibunge ya CCM iliyotunisha matumbo kama vyura kule bungeni na mimacho yao mkiubwa kama ya bundi ndiyo iliyosababisha U.SENGE huu usiovumilika kwa watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom