Kikokotoo(Mafao): Rais Samia anastahili pongezi kwa hili

Hii sheria ni ya kipuuzi. Ulaya baadhi ya nchi ninazozifahamu wanautaratibu mzuri Sana.

Kila mwananchi akifikisha miaka 60 anakula pension yake. Wameweka kiwango kidogo Cha kuchangia anzia ukiwa kijana kuanzia miaka22.

Yaani hakuna Cha mfanyakazi waserikali au dalali au bodaboda. Wote wanachangia huu mfuko na wanapata pension yao na kila mwezi wanakula posho Safi.

Ndiyo maana wazee ndiyo wanatunza familia za vijana wao. Na wanapesa.

Na ushauri.
 
Ya Ulaya huku kwa wacheza singeli hayatekelezeki!
 
Naomba kujuzwa:-
Mfanyakazi wa mkataba private sector anachangia kule NSSF.
Ikitokea 1) asipewe mkataba mpya au 2) kufukuzwa kazi kabla ya kufika miaka 60 say ajira imekoma either kwa kufukuzwa au kutoongezewa muda wa mkataba akiwa bado janki about 32 years, je anaruhusiwa ku claim pesa yake apo nssf immediately au itabidi asubiri hadi afikishe miaka60?!
 
Naichukia hii serikali , Mungu atende tena achukue na huyu
 
Ukweli ni kwamba mifuko ime kopwa na serikali na serikali haiwezi kulipa Hilo Deni la trilion 14. Hivyo wanatumia huu ujanja kwa kuwaumiza watu.
Lini vyama vya wafanyakazi walikaa na ATE na serikali wakakubaliana huu ujinga?
Lkn pia mifuko imejiingiza kwenye biashara ya REAL ESTATE ambayo pay back period yake ni miaka mingi isitoshe magorofa mengi ya NSSF, PSPF SIJUI PSSSF hayana wapangaji na yamejengwa kwa mapesa mengi Sana. Lkn pia ubadhirifu. Imagine Kuna mkurugenzi mmoja kila jumamosi liwake au inyeshe alikua anakwenda uingereza kuangalia mechi za premier league.
Yaani yeye mechi za NEW CASTLE , ARSENAL NA MABINGWA LIVERPOOL anazionaga LIVE.
 
Ya Ulaya huku kwa wacheza singeli hayatekelezeki!
Tatizo ni panya. Inawezekana kabisa tukipata katiba mpya. Hela Kama hii haihitaji msukosuko Mara kukopa Mara kuiba Mara matumizi ya office na vikao. Hili linatakiwa liingie kwenye katiba.

Itafutwe chombo Kama bunge lisimamie hao wafanyakazi. Mfanyakazi akivurunda haiwezi kuwa Siri lazima litabumburuka tu hata Kama ni Rais kakopa lazima wabunge watahoji. Na wao si watakuwemo.
 
Itafutwe chombo Kama bunge lisimamie hao wafanyakazi. Mfanyakazi akivurunda haiwezi kuwa Siri lazima litabumburuka tu hata Kama ni Rais kakopa lazima wabunge watahoji. Na wao si watakuwemo
Bunge gani?
Hili hili la Tulia?!!!
 
Issue kubwa nadhani serikali itakua haipeleki michango huko kwenye mifuko ndo maana wanawekea watu vikwazo kwamba upewe 33% kwanza kubadilisha tu kile kikokotoo cha zamani na kuleta hiki kipwa kuna hela nyingi sana mtumishi anapunjwa...
 
Huyu akimaliza miaka mitano anakusanya jasho lake lote na nyongeza juuu...





Huyu baada ya miaka 60 akistaafu anapewa 33/% na zingine atapewa kidogo kidogo....
 
Bunge gani?
Hili hili la Tulia?!!!
Hapana. Kama katiba mpya ikipatikana. Lazima wabunge wa upinzani watakuwepo. Hili tumwachie Tulia na Msukuma.

Yaani wazee wanatesa ndiyo wenye pesa huko acha kabisa. Ukipokea pension na mkeo na kila mwezi account Zinacheka miaka 💯 lazima uione mjomba.
 
Lakini wabunge wakimaliza miaka mitano wanapewa 200m yote...ila uliesota miaka 60 kuitumikia serikali unakula 33% kwa style hii hakuwezi kua na uwajibikaji serikalini hata siku moja
piga chinu ccm
 
Mwizi ndiye anayepanga. Ni mwendo wa maumivu
 
Shame on us wananchi. We failed big kuendelea kutawaliwa na CCM mpaka sasa.
 
Ufafanuzi kwa wanaujua madhara au faida zake tafadhali. Kwa maelezo hayo tuu haitoshi kujua mataafu anafaidika au anapunjwa kwa kiasi gani. Weka nyama nyama na supu tuweze kuelewa, kwa mwenye uelewa wa kutosha. Hesabu ya ulinganifu inahusika hapo
Faida ni chache hasa ni ongezeko la posho ya kila mwezi. hasara ni nyingi mfano mtmishi akifa mapema kila kitu kinaishia hapo. Mtumishi aliyejiandaa akiwa kazini na anataka kukuza mtaji wake na hela ya mkupuo atapungukiwa mtaji. Mfano mtumishi alitamani kukuza mradi wake wa kilimo kwa kununua mashine kama trekta na mashine za uchakataji ataweza kushindwa kufanya hivyo.
Kwa walevi na wazembe inaweza kuwa na manufaa
 
Tanzania fedha inayokopesheka haraka haraka ni ya mifuko ya hifadhi ya jamii. Serikali inaitumia ovyo ovyo zaidi ya inavyotumia fedha za wahisani.
 
Pensheni ya Kila Mwezi nayo kaongeza kwa Asilimia 17 Hongera sana Mama

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…