Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Incredible and very intelligent question:

a. Kwanza na zaidi kabisa walitakiwa kuangalia Katiba ya sasa inasemaje kuhusiana na kuandika Katiba Mpya.
b. Kwa vile Katiba ya sasa hairuhusu kuandika Katiba Mpya (chini ya Ibara ya 98) basi walitakiwa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa (hasa kwa watu wanaosema wanafuata utawala wa Katiba na Sheria)
c. Katika mabadiliko hayo ya Katiba walitakiwa kuweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya kama ulivyo utaratibu wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa.

Kutoka hayo matatu ndio tungezungumzia kuandika Katiba Mpya.

Sasa hivi wote hawa wanaweza kuitwa wahaini tu!

Kama kuna wanaolalamikia katiba hii tuliyonayo kwamba ni batili (kutokana na ulivyosema), basi hiyo ibara ya 98 aina maana. Kwa hiyo vile vile alivyoamua Nyerere (kama Rais) kuandika katiba tuliyo nayo (ambayo inalalamikiwa) ndivyo alivyoamua Kikwete (Rais) kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Tumekwishafika mbali na mchakato, kama malalamiko yatatatokea mbeleni ni kawaida yetu.
 
Wanajamvi hebu tujikumbushe kidogo tulitokea wapi na tunaelekea wapi;

1.Tarehe 20 Desemba mwaka 2010 wakati Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika alipowasilisha bungeni hoja binafsi ya mabadiliko ya katiba mpya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alisema kuwa haiwezekani kuandikwa upya na badala yake kinachowezekana ni kuifanyia marekebisho iliyopo. Jaji Werema ambaye ndiye mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya kisheria aliweka msimamo wake huo katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande.

2. Aliyekuwa Waziri wa Sheria wakati huo, Celina Kombaine, akimuunga mkono mwanasheria mkuu, naye alidai kutokuwepo na umuhimu wa kuwepo katiba mpya na kwamba Serikali inaridhika na utaratibu uliopo wa kuifanyia katiba hiyo marekebisho ya mara kwa mara pindi umuhimu wa kufanya hivyo unapokuwapo. Alisema hayo mara baada ya kuhudhuria kikao cha baraza jipya la mawaziri kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na kuongeza kwamba wale wanaodai katiba mpya ni watu wa barabarani wasiokuwa na uelewa juu ya masuala hayo.

Nimetoa mifano hii miwili kwa lengo moja tu kuonesha kwamba kabla ya mswada binafsi wa Mbunge wa Ubungo kuwasilishwa bungeni, hakuna ushahidi wowote unaoonesha kwamba upatikanaji wa katiba mpya uliwahi kuwa sera, ilani au ajenda ya chama tawala wala serikali yake. Kwa ufupi ni kwamba madai yoyote kuhusu katiba mpya kama kawaida yalipuuzwa na kubezwa kila yalipotolewa na wananchi wema walioweza kuona dira ya wapi tunakotoka na wapi tunataka kufika.

Kama mlivyoshuhudia hapo juu kauli hizo mbili zilitolewa kwenye viwanja vya Ikulu na vilitolewa baada ya ama shughuli au vikao rasmi vilivyosimamiwa na Raisi Jakaya Kikwete. Si hayo tu, miongoni wa ama waliohudhuria au waliotoa kauli hizo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Sheria na Jaji Mkuu wa Mahakama nchini. Pamoja na hayo, matamko haya yalitolewa wakati ambapo msimamo wa chama tawala, CCM, ulijulikana kuhusu swala zima la katiba mpya.

Swali linalojitokeza hapa kama anavyodokeza Mwanakijiji ni je, Kikwete alipata wapi madaraka ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba mpya ya JMT? Kama aliamua kama Raisi, kipengele gani cha katiba ya nchi kilimruhusu? Kama aliamua kama Mwenyekiti wa CCM, maamuzi ya kikao gani yalimruhusu? Kama aliamua kama Mkuu wa serikali, je Baraza la Mawaziri lilishirikishwa? Okay, wapo watakaodai kama Raisi hahitaji ruhusa, kama ni hivyo huu mchakato ni haramu!

Hii nchi haiendeshwi kidikteta, ni nchi ya kidemokrasia inayoendeshwa kulingana na matakwa ya katiba iliyopo ambayo yeye kama Raisi aliapa kuilinda na kuitetea. Katiba ya nchi si jambo dogo, katiba ni sheria mama na ni katiba hiyo hiyo ndiyo inampa mamlaka Raisi pamoja na serikali anayoisimamia. Kuuacha mchakato wa katiba mikononi mwa mtu ambaye kwa kiwango chochote kile ameonesha udhaifu mkubwa katika kusimamia mambo ya msingi bila kuyumba ni kujitafutia balaa.

Mfano wa udhaifu ninaouongelea ni kama huu wa sintofahamu uliojitokeza sasa wa kutoweza kutoa maamuzi mara moja kuhusu mswada uliopitishwa na Bunge uliogubikwa na utata. Raisi alitakiwa awe anafuatilia kwa makini sana huu mjadala mzito ndani na nje ya Bunge hata kama angekuwa hayupo nchini. Wakati mwingine msimamo wa Raisi hutakiwa kutolewa mapema hata kabla ya mswada kumfikia kama ataukubali au la kulingana na hoja zinavyotolewa bungeni.

Hapana, kwa mtindo huu hatufiki na kama hatukujifunza kwa majirani zetu Kenya nguvu ya Umma ulipokataa rasimu iliyofikishwa kwao kwa njia ya kura ya maoni, basi hatuna tofauti na mbuni. Katiba ni ya wananchi na wao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho kama wataafiki kitakacholetwa mbele yao au wataikataa...naomba kunukuu sehemu ya utangulizikatika misingi ya katiba yetu ya sasa inavyotamka;
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Inaweza kutarajiwa, kwamba,sote, tutakubaliana na Ibara mojawapo inayobainisha wazi kwamba "serikali itapata mamlaka na madaraka ya utawala kutoka kwa wananchi".
Hata kama hakuna Ibara mahususi katika Katiba ya sasa juu ya mwongozo wa namna ya kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba,mchakato huu unapata uhalali wake-pamoja na hoja ya kwanza hapo juu- kutokana na ukweli mwingine kwamba si kila kitu kinachoanzishwa na kutekelezwa-ikiwemo mchakato wa katiba mpya-lazima kiwe kiwe kina uhalali wa kisheria katika maandishi.Wakati mwingine,busara na hekima huweza kutumika kutafsiri mazingira na mahitaji ya nyakati.Wanazuoni nguli wa sheria wanatujuza kwamba Katiba ya sasa si halali kwa kuwa haina uhalali wa kisiasa(kukiuka msingi wa kidemokrasia).Tunapojaribu kuupa mchakato wa kundika katiba uhalali wa kisiasa,sasa hoja mpya ya mchakato kukosa uhalali wa kisheria inaibuka!Hata kama tutakubaliana kwamba mchakato wa sasa umekosa uhalali wa kisheria,tutapaswa kuunga mkono,kwa kuwa,kwa sasa mchakato una uhalali wa kisiasa-kama masuala mengine yakiachwa kama yalivyo-ambayo ndiyo msingi mkuu na tunu muhimu za dhana za demokrasia.Na kama hata mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba unalalamikiwa kutekwa na Chama Tawala,tunaweza kutarajia watunga sheria hawa hawa,wanaoingiza vifungu visivyoingia akilini -kikiwemo kile kinachoweka ukomo wa uhai wa shughuli za Tume ya Katiba-tungeweza kuwatarajia kupitisha Marekebisho ya Katiba ya sasa ambayo yangeweza kuruhusu mabadiliko ya sheria?.
Mwisho,kama dhana ya Demokrasia hujumuisha,pamoja na mambo mengine,utawala wa sheria,na kama dai kwamba mara zote demokrasia ni utawala wa sheria lakini utawala wa sheria -zikiwemo sheria mbalimbali-si lazima utambue,uakisi na ulinde misingi na tunu za demokrasia mara zote ni sahihi,basi mchakato wa sasa wa Katiba Mpya ni sahihi.
 
Wanajamvi hebu tujikumbushe kidogo tulitokea wapi na tunaelekea wapi;

Nimetoa mifano hii miwili kwa lengo moja tu kuonesha kwamba kabla ya mswada binafsi wa Mbunge wa Ubungo kuwasilishwa bungeni, hakuna ushahidi wowote unaoonesha kwamba upatikanaji wa katiba mpya uliwahi kuwa sera, ilani au ajenda ya chama tawala wala serikali yake. Kwa ufupi ni kwamba madai yoyote kuhusu katiba mpya kama kawaida yalipuuzwa na kubezwa kila yalipotolewa na wananchi wema walioweza kuona dira ya wapi tunakotoka na wapi tunataka kufika.

Kama mlivyoshuhudia hapo juu kauli hizo mbili zilitolewa kwenye viwanja vya Ikulu na vilitolewa baada ya ama shughuli au vikao rasmi vilivyosimamiwa na Raisi Jakaya Kikwete. Si hayo tu, miongoni wa ama waliohudhuria au waliotoa kauli hizo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Sheria na Jaji Mkuu wa Mahakama nchini. Pamoja na hayo, matamko haya yalitolewa wakati ambapo msimamo wa chama tawala, CCM, ulijulikana kuhusu swala zima la katiba mpya.

Swali linalojitokeza hapa kama anavyodokeza Mwanakijiji ni je, Kikwete alipata wapi madaraka ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba mpya ya JMT? Kama aliamua kama Raisi, kipengele gani cha katiba ya nchi kilimruhusu? Kama aliamua kama Mwenyekiti wa CCM, maamuzi ya kikao gani yalimruhusu? Kama aliamua kama Mkuu wa serikali, je Baraza la Mawaziri lilishirikishwa? Okay, wapo watakaodai kama Raisi hahitaji ruhusa, kama ni hivyo huu mchakato ni haramu!

Hii nchi haiendeshwi kidikteta, ni nchi ya kidemokrasia inayoendeshwa kulingana na matakwa ya katiba iliyopo ambayo yeye kama Raisi aliapa kuilinda na kuitetea. Katiba ya nchi si jambo dogo, katiba ni sheria mama na ni katiba hiyo hiyo ndiyo inampa mamlaka Raisi pamoja na serikali anayoisimamia. Kuuacha mchakato wa katiba mikononi mwa mtu ambaye kwa kiwango chochote kile ameonesha udhaifu mkubwa katika kusimamia mambo ya msingi bila kuyumba ni kujitafutia balaa.

Mfano wa udhaifu ninaouongelea ni kama huu wa sintofahamu uliojitokeza sasa wa kutoweza kutoa maamuzi mara moja kuhusu mswada uliopitishwa na Bunge uliogubikwa na utata. Raisi alitakiwa awe anafuatilia kwa makini sana huu mjadala mzito ndani na nje ya Bunge hata kama angekuwa hayupo nchini. Wakati mwingine msimamo wa Raisi hutakiwa kutolewa mapema hata kabla ya mswada kumfikia kama ataukubali au la kulingana na hoja zinavyotolewa bungeni.

Hapana, kwa mtindo huu hatufiki na kama hatukujifunza kwa majirani zetu Kenya nguvu ya Umma ulipokataa rasimu iliyofikishwa kwao kwa njia ya kura ya maoni, basi hatuna tofauti na mbuni. Katiba ni ya wananchi na wao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho kama wataafiki kitakacholetwa mbele yao au wataikataa...naomba kunukuu sehemu ya utangulizikatika misingi ya katiba yetu ya sasa inavyotamka;

Mungu ibariki Tanzania.

Katiba tuliyonayo ni ya mlengo wa chama kimoja. Tafakari.
 
HAJA ya kubadilisha katiba na kuwa na yenye taasisi huru (NEC, Polisi, TAKUKURU etc) ilikuwepo siku nyingi, na ilifikia kileleni wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010. Ili kukidhi hiyo HAJA, HOJA ya mchakato wa katiba mpya ikapelekwa bungeni.Kama HOJA ya katiba mpya haitakidhi HAJA ya wananchi, basi tutakuwa tumepoteza muda tu. Ndiyo maana bila makubaliano ya wengi (vyama vyote vikubwa) ni bure kwa CCM kudhani itapatikana katiba ya kikwao. Katiba ni kwa ajili ya wananchi, na sio wananchi kwa ajili ya katiba. Kwa umoja wao, wananchi wakitaka kubadilisha katiba wanaweza. Wapo juu ya katiba.
 
Incredible and very intelligent question:

a. Kwanza na zaidi kabisa walitakiwa kuangalia Katiba ya sasa inasemaje kuhusiana na kuandika Katiba Mpya.
b. Kwa vile Katiba ya sasa hairuhusu kuandika Katiba Mpya (chini ya Ibara ya 98) basi walitakiwa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa (hasa kwa watu wanaosema wanafuata utawala wa Katiba na Sheria)
c. Katika mabadiliko hayo ya Katiba walitakiwa kuweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya kama ulivyo utaratibu wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa.

Kutoka hayo matatu ndio tungezungumzia kuandika Katiba Mpya.

Sasa hivi wote hawa wanaweza kuitwa wahaini tu!
Mkuu mwanakijiji pengine huko sawa na malalamiko yako, lakini tunaomba mwongozo wako wa mawazo hiwapo hayo madai yako ya mchakato hayapo sawa na endapo yatarekebishwa.

Je kwa mtazamo wako binafsi unataka hiyo katiba irekebishwe wapi kwa upande wako; ukiangalia the governance accountability, haki za raia kwa sasa na uonevu huko wapi in short wewe kwako matatizo ya katiba yako wapi na yarekebishwe vipi hayo ni maswali ambayo mtanzania wakaida pia anatakiwa haya ongelee kwa upande wake ni wapi wewe unaona katiba inamatatizo kiserikali na kwa upande wa haki zetu wananchi, mfano kama ndio ungepewa muda wa kuongelea matatizo ya katiba ni yepi hasa kwako.

Maana we kila saa katiba this katiba that, tuelimishe tukuelewe katiba mpya inaulizama gani na vipengele gani vya haki zetu kwa sisi watanzania tulio hoehae unaona vimezibwa na tunaonewa hili tukuelewe na haki zenyewe tuzidai vipi ambapo kwa sasa tumenyimwa unavyoona.

Wewe unataka nini hasa kwenye hii katiba mpya unayo idai kila kukicha ukiwa kama mtanzania na haki zako ni kipi unacho demand hayo ndio maswali hata jamaa mnaotaka wapelekewe huko vijijini pia wanatakiwa wayajibu na ni wapi wamekwazika na hizo haki ambazo zimenyimwa kwenye katiba ya sasa na usawa upatikane vipi?.

Mwanakijiji na wenzako nyie ndio mnae enda kutuondela haki zetu matatizo yaliyopo kwa sasa ni kwa sababu ya wabunge ya CCM and them going unchallenged thus far due to social ignorance sasa mnawapa fursa ya kufuta haki zetu. Katiba aikuwa na matatizo zaidi ya nguvu za sehemu kadhaa, i hate CDM for this.
 
HAJA ya kubadilisha katiba na kuwa na yenye taasisi huru (NEC, Polisi, TAKUKURU etc) ilikuwepo siku nyingi, na ilifikia kileleni wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010. Ili kukidhi hiyo HAJA, HOJA ya mchakato wa katiba mpya ikapelekwa bungeni.Kama HOJA ya katiba mpya haitakidhi HAJA ya wananchi, basi tutakuwa tumepoteza muda tu. Ndiyo maana bila makubaliano ya wengi (vyama vyote vikubwa) ni bure kwa CCM kudhani itapatikana katiba ya kikwao. Katiba ni kwa ajili ya wananchi, na sio wananchi kwa ajili ya katiba. Kwa umoja wao, wananchi wakitaka kubadilisha katiba wanaweza. Wapo juu ya katiba.
Nakubalina na hoja ya kuwa kuna umuhimu wa vyombo huru and independent hili kuweka sawa checks, lakini source ya matatizo hayo ni katiba mpya au kupunguza nguvu ambazo kwa sasa ni overlapping decision making from one government body especially the presidency.

Kwa upande wako katiba mpya itatue vipi hili swala, na kwa sasa wananchi wanaonewa vipi in general mpaka wapewe katiba mpya?
 
Tuchukulie kuwa ni swali la kitoto lijibu basi; maana hata mtoto akiuliza swali anapewa jibu. Ukiona mtu mzima anashindwa kujibu swali la mtoto ni kwa sababu mtoto kauliza swali gumu. Wewe unaamini Kikwete (Rais wa Tanzania) ana madaraka ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Kwanza kaa chini ujiulize ni nini maana ya madaraka. Nadhani hicho ndicho unachoshindwa kuelewa, maana ya neno madaraka.

Rais asingekuwa na madaraka ya kusimamia (sio kuanzisha, kwa sababu Kikwete hajaanzisha mchakato wa katiba mpya - hapo napo kajifunze ni nani au nini kilichoanzisha mchakato wa katiba mpya) mchakato wa katiba mpya, basi tusingekuwa hapa tulipo.

Katiba is a political-legal agenda na ukiifikiria kimahakama tu lazima upotoke, hasahasa kama huna nia njema kama ulivyo wewe.
 
Anatabia mbaya sana huyo Mwanakijiji binafsi i hate him to bits kwa upotoshaji wake if only people could see him him for what he is.
 
Anatabia mbaya sana huyo Mwanakijiji binafsi i hate him to bits kwa upotoshaji wake if only people could see him him for what he is.

Watu wameshaanza kumshtukia, ndio maana mgomo wake wa simu ulifeli.
 
chombo halali kinapatikana kwa njia halali. Chukulia kwa mfano; Rais Kikwete akiamua kesho kuwa anaanzisha Mahakama ya Wanawake - je itakuwa ni halali kwa yeye kufanya hivyo kwa sababu tu anaamini kesi zinazohusiana na wanawake zinahitaji mahakama maalum; na wakatokea wanawake wengi wakamuunga mkono... sisi wengine tutapinga kwa sababu hana madaraka ya kuanzisha mahakama!

umejichekesha chekesha ovyo utafikiri si mtu mzima hakuna hoja yoyote yenye mashiko ulotoa inayoonyesha uharamu wa mchakato wa katiba mpya na umeongea kichele inaonesha hujiamini toa hoja zenye mashiko ueleweke hata kule kwa ilunga.uliongea porojo tu we mzee pumzika siasa zimekutupa mkono
 
Nadhani alifuata ushauri wa Dr.W.Slaa, kuwa akichukuwa nchi ndani ya siku 90 atakuwa kaishaandika katiba mpya.

Kwa hiyo JK KJ Kumbe aliogopa akaamua kufuata huo ushauri?
 
Last edited by a moderator:
Pasco naomba urejee nada yako hiyo na unioneshe nilipokubeza kwani ukosoaji wangu wa mchakato huu haujaanza baada ya mswada kuletwa bungeni bali ulianza pale Kikwete alipotangaza tu nia ya kutaka kuanzisha mchakato huu. So nioneshe nilipokubeza ili nikuuombe radhi.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, debates zote zina pande mbili tuu, for or against!, nilipouanzisha ule mjadala, nilisema kwenye mchakato wa katiba, Chadema did a wrong move, took a wrong step, hivyo kwa kutousimamisha, they'll have either to live with it, or suffer the consequences!, watu wa for ni wale waliokubaliana na mimi, watu wa against ni wale waliopingana na mimi. Wewe ulikuwa against na kusisitiza Chadema did the right thing and the right move!.

Hiki kinachoendelea sasa ni matokeo tuu!, na kwenye huu mchakato wa Katiba, as of now, its too little too late!.

Nilisisitiza, if you can't get what you want, just take what you get!", japo "katiba bora" is what we want, na tunachopewa ni "bora katiba!", bora kwanza, tuipokee tuu hii "bora katiba!" kwa sababu something is better than nothing!, tukiikataa, katiba hii hii iliyopo ndio itaendelea!, haya ni maji, tumeisha yavulia nguo, hatuna budi kuyaoga!.

Pasco.
 
Incredible and very intelligent question:

a. Kwanza na zaidi kabisa walitakiwa kuangalia Katiba ya sasa inasemaje kuhusiana na kuandika Katiba Mpya.
b. Kwa vile Katiba ya sasa hairuhusu kuandika Katiba Mpya (chini ya Ibara ya 98) basi walitakiwa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa (hasa kwa watu wanaosema wanafuata utawala wa Katiba na Sheria)
c. Katika mabadiliko hayo ya Katiba walitakiwa kuweka utaratibu wa kuandika Katiba Mpya kama ulivyo utaratibu wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa.

Kutoka hayo matatu ndio tungezungumzia kuandika Katiba Mpya.

Sasa hivi wote hawa wanaweza kuitwa wahaini tu!
Mkuu Mzee Mwanakijiji, sometimes "The end, justifies the means!", tukiangalia mchakato wa kupatikana jii katiba ya JMT ya 1977 na huu unaondelea sasa, we are 100 times better off!, as of now, its too little too late!,
Tuendeleze mchakato tupate katiba katiba mpya, hata kama sio "katiba bora!. bali ni "bora katiba!".
Pasco.
 
Kaka too direct kutaka kifungu maalumu kinacho lipa bunge mamlaka ya kutunga sheria ya katiba mpya.Anyway, ninavyoelewa mie katiba ni mwongozo, nakubaliana na wewe kuwa hakuna specific kifungu katika katiba kinalipa bunge uwezo wa kutunga katiba mpya..Lkn bunge ni chombo cha kisheria kinachotunga sheria za nchi yetu nahakuna chombo kingine kinachofanya kazi hiyo.

Hii ni reasoning isiyo sahihi. Kama Katiba haijatoa madaraka kwa Bunge au kwa mtu yeyote mwingine kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya - wakati katiba ya sasa bado ina nguvu na hakujafanyika mapinduzi ambayo yameisuspend the current constitution, huku kuandika Katiba Mpya kunatoka kwenye madaraka gani? Nadhani watu hawaelewi maana ya "madaraka". Madaraka ni ule uwezo ambao mtu au taasisi inapewa kuweza kufanya mambo fulani yaliyo chini au ndani ya uwezo huo na bila ya uwezo huo mtu au chombo hicho hakiwezi kufanya.

Kwa mfano, watu wote hawawezi kufungisha ndoa hata kama wanaweza kusema maneno ya ndoa na hata kuvaa nguo za mashehe, wachungaji au mapadre. Kwanini? Kwa sababu hawana madaraka ya kufanya hivyo. Lakini pia siyo kila mwenye madaraka ya kufungisha ndoa anaweza kufungisha ndoa yoyote isipokuwa kama ana madaraka mahsusi. Padre hawezi kwenda kwa Waislamu na kufungisha ndoa Kiislamu halafu ndoa ikawa halali!

Katiba yetu ya sasa haina ibara ya kuandika Katiba Mpya; HAKUNA. Sasa Bunge haliwezi kutunga sheria ya kitu ambacho halina uwezo nacho! Bunge kwa vile linatunga sheria haliwezi kupitisha sheria ya kufuta Katiba ya sasa! Lakini kwa maajabu Watanzania wamekubali kuwa Bunge lina uwezo huo.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, sometimes "The end, justifies the means!", tukiangalia mchakato wa kupatikana jii katiba ya JMT ya 1977 na huu unaondelea sasa, we are 100 times better off!, as of now, its too little too late!,
Tuendeleze mchakato tupate katiba katiba mpya, hata kama sio "katiba bora!. bali ni "bora katiba!".
Pasco.

Watu wenye akili hawapaswi kukubali uovu na uharamu kwa sababu ya convenience. Ndoa ikifungwa hata kama watu wamekula wali na kufanya harusi kubwa haiendelei kuwa ndoa kama itaonekana haikuwa halali. Uhalali wa ndoa hauji kwa vile watu wamekubaliana kuishi pamoja na kupendana la hasha.

Lakini pia si kweli kuwa it is too little na too late; Mchakato huu haujafika mahali popote ambapo hauwezi kusitishwa na kubadilishwa. Umefika hapa kwa sababu watu wamekubali kucompromise na uongo; wamekubali Rais afanye kitu asicho na madaraka nacho na wamekubali Bunge lipitishe sheria ya kitu ambacho halina uwezo nacho. That to me is the tragedy of immense proportion.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, debates zote zina pande mbili tuu, for or against!, nilipouanzisha ule mjadala, nilisema kwenye mchakato wa katiba, Chadema did a wrong move, took a wrong step, hivyo kwa kutousimamisha, they'll have either to live with it, or suffer the consequences!, watu wa for ni wale waliokubaliana na mimi, watu wa against ni wale waliopingana na mimi. Wewe ulikuwa against na kusisitiza Chadema did the right thing and the right move!.

Hiki sicho ulichosema hapo juu; umenituhumu kuwa nilikubeza kana kwamba nilidharau mchango wako na kukufanya uonekane mjinga. Kumbe nilikuwa na maoni tofauti na wewe tu na yalitolewa kwa heshima yote. Maoni yako yale yalikuwa na makosa wakati ule kama ambavyo bado yameendelea kuwa na makosa. Hii si kubeza.
 
Anatabia mbaya sana huyo Mwanakijiji binafsi i hate him to bits kwa upotoshaji wake if only people could see him him for what he is.

Njoo tujadiliane live unioneshe huo upotoshaji wangu; if you dare. Lakini kama kuchukia tu well; inakula wewe mwenyewe. I love you to pieces.
 
Kwanza kaa chini ujiulize ni nini maana ya madaraka. Nadhani hicho ndicho unachoshindwa kuelewa, maana ya neno madaraka.

Rais asingekuwa na madaraka ya kusimamia (sio kuanzisha, kwa sababu Kikwete hajaanzisha mchakato wa katiba mpya - hapo napo kajifunze ni nani au nini kilichoanzisha mchakato wa katiba mpya) mchakato wa katiba mpya, basi tusingekuwa hapa tulipo.

Katiba is a political-legal agenda na ukiifikiria kimahakama tu lazima upotoke, hasahasa kama huna nia njema kama ulivyo wewe.

Una kumbukumbu fupi sana; nani alianzisha mchakato wa Katiba kama siyo Rais Kikwete?
 
Back
Top Bottom