Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

Kikwete Alipata Wapi Madaraka ya Kuanzisha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya ya JMT?

chombo halali kinapatikana kwa njia halali. Chukulia kwa mfano; Rais Kikwete akiamua kesho kuwa anaanzisha Mahakama ya Wanawake - je itakuwa ni halali kwa yeye kufanya hivyo kwa sababu tu anaamini kesi zinazohusiana na wanawake zinahitaji mahakama maalum; na wakatokea wanawake wengi wakamuunga mkono... sisi wengine tutapinga kwa sababu hana madaraka ya kuanzisha mahakama!
Ok mkuu,na njia halali ya kukipata chombo halali ni ipi?shukran.
 
Bunge kwa vile linatunga sheria haliwezi kupitisha sheria ya kufuta Katiba ya sasa! Lakini kwa maajabu Watanzania wamekubali kuwa Bunge lina uwezo huo.
Raisi hana madaraka ya kuanzisha mchakato wa katiba main topic ya thread hii, bunge pia aliwezi kwa madai yako aliyebaki na anaejua njia mbadala ni mwanakijiji mwenyewe yeye ndio much-know, mwee (in mwanakijiji's voice) hata sijui kwenye katiba mpya wewe kama mtanzania unataka nini zaidi ya fujo.

alamsiki me out.
 
Watu wenye akili hawapaswi kukubali uovu na uharamu kwa sababu ya convenience. Ndoa ikifungwa hata kama watu wamekula wali na kufanya harusi kubwa haiendelei kuwa ndoa kama itaonekana haikuwa halali. Uhalali wa ndoa hauji kwa vile watu wamekubaliana kuishi pamoja na kupendana la hasha.

Lakini pia si kweli kuwa it is too little na too late; Mchakato huu haujafika mahali popote ambapo hauwezi kusitishwa na kubadilishwa. Umefika hapa kwa sababu watu wamekubali kucompromise na uongo; wamekubali Rais afanye kitu asicho na madaraka nacho na wamekubali Bunge lipitishe sheria ya kitu ambacho halina uwezo nacho. That to me is the tragedy of immense proportion.

Teh teh teh teh! Zimwi hata likivaa baibui utalijua tu!
Kwe kwe kwe kwe!

You can run but you can not hide!

Mr m.m.mwanakijiji! Teh teh teh teh!

I will keep that to myself! But if you cough up! I will embarrass you! I promise!
 
Una kumbukumbu fupi sana; nani alianzisha mchakato wa Katiba kama siyo Rais Kikwete?

This is interesting indeed!

Mchakato wa Katiba umeanzishwa na vuguvugu la kisiasa nchini ambalo liliwezesha kila mtu kutambua kuwa kuna haja ya kuwepo kwa katiba mpya. Alichokifanya Rais ni kukubali kusimamia mchakato huo, sio kuuanzisha.

Rais hajaamka asubuhi na kusema "tuandike katiba mpya" alichokisema Rais ni "ndio ipo haja ya kuandika katiba mpya". Angeweza kusema hivyo na kuishia hapo bila kuonyesha leadership au akaonyesha leadership kama alivyofanya Kikwete ya kuusimamia mchakato huo.
 
This is interesting indeed!

Mchakato wa Katiba umeanzishwa na vuguvugu la kisiasa nchini ambalo liliwezesha kila mtu kutambua kuwa kuna haja ya kuwepo kwa katiba mpya. Alichokifanya Rais ni kukubali kusimamia mchakato huo, sio kuuanzisha.

Unaandika upya historia; soma tena hotuba yake ya kukaribisha mwaka mpya 2011. Usitengeneze historia mpya. Lakini upande mwingine unakataa huku unakubali.
 
Raisi hana madaraka ya kuanzisha mchakato wa katiba main topic ya thread hii, bunge pia aliwezi kwa madai yako aliyebaki na anaejua njia mbadala ni mwanakijiji mwenyewe yeye ndio much-know, mwee (in mwanakijiji's voice) hata sijui kwenye katiba mpya wewe kama mtanzania unataka nini zaidi ya fujo.

alamsiki me out.

Pole, kama hujui ni vizuri kusema hujui ujulishwe; na kama mtu anajua kitu ni unafiki kujifanya hajui. Wapo wengine ili wasionekane "know much" wanakaa kimya kama hawajui na wakuwaacha wasiojua kufanya wasichojua! Siku njema.
 
Ok mkuu,na njia halali ya kukipata chombo halali ni ipi?shukran.

Ni ile iliyowekwa kihalali na vyombo halali. So far njia pekee halali ni ya kubadilisha Katiba ya sasa au orodha ya mambo ya Muungano vyote vimeelezwa ndani ya Katiba ya sasa Article 98. Kuandika Katiba Mpya hakuna utaratibu wa Kikatiba wametunga tu sheria isiyokubaliana na Katiba ya sasa.
 
Upinzani kama inamaanisha kupinga kila jambo zuri na baya litendwalo na serikali basi Mzee Mwanakijiji umeshinda katika hili. Sikuwahi kukuona ukiunga mkono hata move +or- moja ya serikali.
 
Last edited by a moderator:
Ni ile iliyowekwa kihalali na vyom
bo halali. So far njia pekee halali ni ya kubadilisha Katiba ya sasa au orodha ya mambo ya Muungano vyote vimeelezwa ndani ya Katiba ya sasa Article 98. Kuandika Katiba Mpya hakuna utaratibu wa Kikatiba wametunga tu sheria isiyokubaliana na Katiba ya sasa.

Bado hujatusaidia kutujuza njia halali

mwanakijij,tunasubiri ufafanuz Wako,pia ushakuwa mzee sass,acha lugha za matus,usizeeke vibaya mm
 
Hili ni swali ambalo jibu lake liko wazi; kuwa Rais Kikwete hakuwa na madaraka hayo. Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa kwa vile Rais kaamua kufanya kitu basi kitu hicho ni halali.

Mimi na baadhi yetu tumekataa kuutambua mchakato huu wa Katiba Mpya kwa sababu ni haramu; haukuanzishwa na chommbo halali na hata hivi sasa matatito tunayoyaona na yatakayotokea mbeleni (kwenye Bunge la Katiba na Kura ya Maoni) itakuwa ni mwendelezo tu wa kosa hili kubwa.

HUU NI MCHAKATO HARAMU. Sikiliza HOJA MARIDHAWA

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=115504&stc=1&d=1381127129[/JFMP3]

Sasa hapa MM kama hali halisi ndiyo hivyo ni nani mwenye makosa, ni yeye au ni sisi wananchi? Kama hakuwa na mamlaka hayo na hajatulazimisha ni sisi wenyewe tumeridhia, ina maana Kikwete naye ametoa mawazo yake kama mwananchi wa kawaida tu na ikapelekea watu wakayakubali sawa tu kama vile ambavyo ningeweza kutoa mawazo yangu mimi au wewe na yakakubalika na kufanyiwa kazi. After all, pamoja na kwamba mimi si mtaalamu sana wa mambo ya sheria na wala sijawahi kuisoma kwa kina sana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi nadhani uhuru wa kutoa mawazo, yakakubaliwa au yakakataliwa ni haki ya uraia. Hivyo siku tukikuchagua wewe tuseme kuwa Rais wa JMT ujue kuwa tunakuvika mamlaka ya ziada tu na haki zako zingineza msingi kama mwananchi wa kawaida zinaendelea kuwepo kama ilivyokuwa awali. Mimi niko pessimistic kwamba huu mchakato ningeweza kuuanzisha hata mimi na uka-take-off na kuwa kama ulivyo sasa hivi. Watu tunapowapa madaraka fulani tusijisahau hadi tukafikia hatua ya kuwanyang'anya haki zao za msingi wanazostahili kuendelea kuwa nazo kama raia wa kawaida
 
By JF-MBUNGE
Mkuu kaka anashindwa kuelewa kuwa some times illegal things can be appropriate,but an issue is appropriate for what?


Oh boy; what kind of logic is this?

Simple kaka, mwizi akikufyatua risasi kukutoa maisha yako na we una silaa ukammaliza! is it legal kuua? will it not be appropriate action for ur life? I think u should learn to view in different views rather than view according 2ur view.
 
Upinzani tu usingekuwa sababu ya kufanya kitu kikubwa na nyeti hivi. Kumbuka alishinda na kuapa kulinda na kuhifadhi Katiba anayotaka kuibadilisha. Nafikiri factor ya Zanzibar ilikuwa msingi mkubwa wa mchakato huu. Zanzibar kwa Katiba yao walishakinzana na Katiba ya Muungano. Hakuna njia ingine isipokuwa kutengeneza Katiba mpya ili kuondoa msigano huu.
​Kwani CCM bara na visiwani hawakuliona hilo!? Tuseme JK ndiye Think tank wa CCM!?
 
​Kwani CCM bara na visiwani hawakuliona hilo!? Tuseme JK ndiye Think tank wa CCM!?

Mimi nakubaliana na MM kuwa utaratibu wa kikatiba kuhusu mchakato umekosewa. Ulitakiwa upitie ibara ya 98 ya Katiba. Lakini Rais Kikwete hakuwa na uwezo wa kuanzisha mchakato huo kuanzia ibara ya 98! Alipaswa aanze kwenye vikao halali vya CCM. Na wana-CCM wengi (mie simo) wanalijua hilo lakini kwa unafiki wao wameshindwa kumwambia Mwenyekiti badala yake wamekalia kuuvuruga mchakato batili.

Wakati ule akina Malecela walipokubaliana bungeni kuanzisha serikali ya Tanganyika Nyerere aliwaambia 'serikali ya Tanganyika haikuwa sehemu ya sera za CCM, chama tawala na hivyo hawawezi kuanzisha sera hiyo bungeni. Walipaswa kuileta chamani kwanza, ijadiliwe, ikubaliwe, ndio ipelekwe bungeni kama muswada wa sheria'. Ndivyo ilivyo kwa kuandika katiba mpya - sio sera ya CCM - na Kikwete hawezi kuianzisha juu kwa juu bila maamuzi ya vikao halali vyo CCM! Sasa udhaifu wa CCM kama chama ndio umetufikisha hapa. Wanafiki. Wangemshauri Mwenyekiti kuhusu utaratibu. Katiba mpya sio sera ya CCM hivyo basi tujadili kwanza kwenye chama, tukikubaliana, tuiagize serikali ipate ushauri wa kisheria wa namna ya kuandiaka katiba mpya. Hapo sasa Mwanasheria Mkuu angeitwa na kuulizwa - tufanyeje? Bila shaka angejielekeza kwenye ibara ya 98.

Najua Kikwete anatafuta 'legacy' lakini inavyoelekea he might go down in history, not only as the worst President ever, but also as worst CCM Chairman. Amewabambikia CCM sera feki ya katiba mpya - hawajui cha kufanya - kila mmoja na lwake. Isitishe kaibambikia nchi mchakato feki wa kuandika katiba mpya. Hotuba zake zote yeye ni kung'ang'ania kuteua misururu ya watu tu! "oho Kama Nyerere aliteua kwa nini na mimi nisiteue'!!!
 
Unaandika upya historia; soma tena hotuba yake ya kukaribisha mwaka mpya 2011. Usitengeneze historia mpya. Lakini upande mwingine unakataa huku unakubali.

Simple question. Nikisema "Kimsingi katiba Mpya ni hoja ya wapinzani", nitakuwa nadanganya?
 
Simple question. Nikisema "Kimsingi katiba Mpya ni hoja ya wapinzani", nitakuwa nadanganya?
​Hujaniuliza mimi, lakini naweza kujibu kuwa imo ndani ya manifesto za vyama vya upinzani na siyo ndani ya manifesto ya CCM!
 
​Hujaniuliza mimi, lakini naweza kujibu kuwa imo ndani ya manifesto za vyama vya upinzani na siyo ndani ya manifesto ya CCM!

Jibu lako ni sahihi lakini halijalenga swali. Swali ni je, nitakuwa nadanganya? Lengo langu ni kuderive jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyoanza, maana kuna wapotoshaji wanaanza kusema kuwa Kikwete ndiye aliyeuanzisha huu mchakato which is a gross misleading piece of information.
 
hahaha hii akili au matope

dk 9:04 unajichekesha unacheka mwenywe

neno haramu umerudia kama mara mia

hujanukuu hata kifungu kimoja cha katiba

this is ridiculous!

Eti katiba haina sehemu ya kubadilisha katiba bali kurekebisha

khaaaaa

Ha ha haaa, ingefaa umnyooshee na kidole kileeeeeee....!!! ha ha haa
 
Back
Top Bottom