Kikwete aonya Serikali kupuuza ushauri. Ataja madhara yake

Kikwete akiwa rais alipokuwa anapewa ushauri ku deal na matatizo ya nchi alikuwa anasema "huo ni upepo tu, utapita".

Leo anatuhubiria umuhimu wa ushauri.

Halafu habari haijatuambia Kikwete aliufanyia kazi vipi ushauri wa Zacharia Hans Poppe?
 
Eti ngano imepanda Bei Kwa Sababu ya Vita ya Ukraine Halafu akaishia hapo?

Hivi Nani aliua mashamba ya ngano kule Manyara ?
Kwa nchi ambazo zinapima hata maelezo ya mtu tu kabla ya kumpa nafasi ya kugombea urais, Kikwete hakutakiwa kuwa rais.

Tatizo Tanzania hatupimi.

Kikwete anaweza kuwa anaelezea kitu, ukaona kafika katikati ya kukielezea, hajamaliza, halafu kumbe mwenzako ndiyo kashamaliza bila conclusion hapo.

Hata hiyo story ya Zacharia Hans Poppe sijui ni muandishi kafanya uzembe hakuandika conclusion ilikuwa vipi, au ni Kikwete mwenyewe hakutoa conclusion alilifanyia kazi vipi hilo suala.

Ila siwezi kushangaa ikiwa Kikwete katoa story nusu bila conclusion halafu kawaacha watu homework, fill in the blanks.

Ana tabia hiyo sana, halafu ni kama yeye mwenyewe haelewi kwamba amesema mambo in unfinished sentences.

Kikwete ana tabia ya kuongea kama vike watu wote wanaweza kuona anafikiria nini kichwani mwake, hivyo hata asipomalizia sentensi, wataelewa tu kwa kuona mawazo yake.

Unashangaa, huyu kapewaje urais?
 
Duniani kote makampuni makubwa yanawalipa mabilioni wale wenye mchango Mkubwa kwenye kampuni.

Paulo Makonda anafanya KAZI kubwa sana .
Makonda anastahili kulipwa Hata pesa yote ya chama . Na pia pesa ya Mwenge yote alitakiwa apewe Makonda. Makonda ni Mzalendo halisi. Natamani 2025 ningekua Rais nimteue Makonda kuwa Waziri Mkuu.


CCM inamuhitaji makonda kuliko makonda anavyoihitaji CCM Kwa WAKATI Huu ambao vijana wengi zaidí ni maskini na wanaamini kuwa Dr. Samia yupo Kwa ajili ya kutetea maslahi ya matajiri Wa Chache na familia Zao. Vijana wengi sana Wana Imani na Makonda kuliko MTU yeyote Kwa Sasa ndani ya CCM .
 
Alipokuwa ikulu 2005 to 2015,kulikuwa hakuna Vita ya ukraine wala Israel, na kilimo chetu kilikuwa hovyo, ngsno sukari, nakisi kubwa mpaka kuagiza nje, bei ya mafuta ni kubwa, vigezo vipo vingi, ila Kodi na tozo zinachukua eneo kubwa, taasisi kama ewura,inapata mapato yake kwa kuweka Kodi kwenye kila Lita,
Huyu msoga, alikuja na Sera ya kilimo kwanza, wakaishia kununua magari tu, kilimo Kodi nyingi, mkulima anakufa.
Alipoona ufaulu umepungua shuleni, akaja na u taratibu wake wa kipuuzi na maprofesa wake wa mchongo akashusha pass Mark, ili wafaulu wengi, big result now, matokeo makubwa sasa, siasa ikaingilia utaharamu! Sasa Leo anaongea nini? So pathetic
 
Sasa huyu mwenye taaluma ya ufagizi na upangaji wa vitabu ofisini aliyebahatika kuingia ikulu ndiyo hajui kitu abisa . Yeye kaja na mbinu ya mwanafunzi kula uroda na kuzaa huku akiendelea kusoma. Kuondoa mitihani ya darasa la saba na kupunguza miaka ya elimu ya msingi. Pumbavu!
 
Amekerwa sana na uwepo wa Makonda kwenye CC. Concern yake ni too personal.
Hivi kweli Kwa mtu Mwenye akili timamu zile ziara za Makonda za kupanda Punda na watu kufurika kuleta malalamiko hadharani
Kule ni kujenga chama au kukiumbua chama kilicholala!!!

Aibu Kwa chama na Kwa aliye mteua

Alafu watu wenye akili wapo kimya!!!
 
Nimekuelewa
Kwa Sasa Makonda ndiyo sauti ya Mama

Nandiyo maana majuzi mama kupitia Makonda alimdhalilisha Mwanamke mwenza
Kwaile kauli
Swali Hilo kamuulize "mamako"

Jambo hili Raisi asipo likemea hadharani no doa la "milele' kwake

Inashangaza UWT wapo kimya
Umoja wa awake Chadema kimya
Hata wanawake na wanaume walio zaliwa na wanawake kimya

Hili neno la dharau Kwa mama lisiachwe lipite hivi hivi ni Tusi kubwa Kwa jamii iliyo staarabika
 
Huu mwandiko wa Makonda😀😀😀
 
Hayo nimatokeo ya kukithiri kwa rushwa mkuu. Viongozi wanawaza upigajitu sio maendeleo ya nchi.
 
A stray missile 😅😅 !
Let’s wait and see what is coming next !
Law of the Universe , What goes around comes around !

KARMA Is loading 🙏🙏🙏
 
Analalamika nchi wazalishaji wa bidhaa wako vitani, mbona hazungumzii kabisa matumizi ya gas kwakuwa alishaigawa kwa maswahiba wake na sasa yeye anafanya biashara ya mafuta, hazungumzii kabisa uwekezaji kwenye kilimo, mafuta ya kula yanaweza kuzalishwa kwa wingi Singida (alizeti), Dodoma (karanga), Kigoma (mawese)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…