Kikwete aonya Serikali kupuuza ushauri. Ataja madhara yake

Kikwete aonya Serikali kupuuza ushauri. Ataja madhara yake

Kikwete akiwa rais alipokuwa anapewa ushauri ku deal na matatizo ya nchi alikuwa anasema "huo ni upepo tu, utapita".

Leo anatuhubiria umuhimu wa ushauri.

Halafu habari haijatuambia Kikwete aliufanyia kazi vipi ushauri wa Zacharia Hans Poppe?
 
Eti ngano imepanda Bei Kwa Sababu ya Vita ya Ukraine Halafu akaishia hapo?

Hivi Nani aliua mashamba ya ngano kule Manyara ?
Kwa nchi ambazo zinapima hata maelezo ya mtu tu kabla ya kumpa nafasi ya kugombea urais, Kikwete hakutakiwa kuwa rais.

Tatizo Tanzania hatupimi.

Kikwete anaweza kuwa anaelezea kitu, ukaona kafika katikati ya kukielezea, hajamaliza, halafu kumbe mwenzako ndiyo kashamaliza bila conclusion hapo.

Hata hiyo story ya Zacharia Hans Poppe sijui ni muandishi kafanya uzembe hakuandika conclusion ilikuwa vipi, au ni Kikwete mwenyewe hakutoa conclusion alilifanyia kazi vipi hilo suala.

Ila siwezi kushangaa ikiwa Kikwete katoa story nusu bila conclusion halafu kawaacha watu homework, fill in the blanks.

Ana tabia hiyo sana, halafu ni kama yeye mwenyewe haelewi kwamba amesema mambo in unfinished sentences.

Kikwete ana tabia ya kuongea kama vike watu wote wanaweza kuona anafikiria nini kichwani mwake, hivyo hata asipomalizia sentensi, wataelewa tu kwa kuona mawazo yake.

Unashangaa, huyu kapewaje urais?
 
Hivi kweli Bashite waliomweka Uenezi wamefikiria nje ya box,ni mtu mwenye majivuno na hana nidhamu kabisa pia fedha anazotoa takukuru chunguzeni amepewa na chama au ameanza vitisho vyake kwa wafanyabiashara kuwalazimisha wamchangie.mfano eti amempatia gari mwalimu aliyedhulumiwa gari.
Duniani kote makampuni makubwa yanawalipa mabilioni wale wenye mchango Mkubwa kwenye kampuni.

Paulo Makonda anafanya KAZI kubwa sana .
Makonda anastahili kulipwa Hata pesa yote ya chama . Na pia pesa ya Mwenge yote alitakiwa apewe Makonda. Makonda ni Mzalendo halisi. Natamani 2025 ningekua Rais nimteue Makonda kuwa Waziri Mkuu.


CCM inamuhitaji makonda kuliko makonda anavyoihitaji CCM Kwa WAKATI Huu ambao vijana wengi zaidí ni maskini na wanaamini kuwa Dr. Samia yupo Kwa ajili ya kutetea maslahi ya matajiri Wa Chache na familia Zao. Vijana wengi sana Wana Imani na Makonda kuliko MTU yeyote Kwa Sasa ndani ya CCM .
 
Alipokuwa ikulu 2005 to 2015,kulikuwa hakuna Vita ya ukraine wala Israel, na kilimo chetu kilikuwa hovyo, ngsno sukari, nakisi kubwa mpaka kuagiza nje, bei ya mafuta ni kubwa, vigezo vipo vingi, ila Kodi na tozo zinachukua eneo kubwa, taasisi kama ewura,inapata mapato yake kwa kuweka Kodi kwenye kila Lita,
Huyu msoga, alikuja na Sera ya kilimo kwanza, wakaishia kununua magari tu, kilimo Kodi nyingi, mkulima anakufa.
Alipoona ufaulu umepungua shuleni, akaja na u taratibu wake wa kipuuzi na maprofesa wake wa mchongo akashusha pass Mark, ili wafaulu wengi, big result now, matokeo makubwa sasa, siasa ikaingilia utaharamu! Sasa Leo anaongea nini? So pathetic
 
Alipokuwa ikulu 2005 to 2015,kulikuwa hakuna Vita ya ukraine wala Israel, na kilimo chetu kilikuwa hovyo, ngsno sukari, nakisi kubwa mpaka kuagiza nje, bei ya mafuta ni kubwa, vigezo vipo vingi, ila Kodi na tozo zinachukua eneo kubwa, taasisi kama ewura,inapata mapato yake kwa kuweka Kodi kwenye kila Lita,
Huyu msoga, alikuja na Sera ya kilimo kwanza, wakaishia kununua magari tu, kilimo Kodi nyingi, mkulima anakufa.
Alipoona ufaulu umepungua shuleni, akaja na u taratibu wake wa kipuuzi na maprofesa wake wa mchongo akashusha pass Mark, ili wafaulu wengi, big result now, matokeo makubwa sasa, siasa ikaingilia utaharamu! Sasa Leo anaongea nini? So pathetic
Sasa huyu mwenye taaluma ya ufagizi na upangaji wa vitabu ofisini aliyebahatika kuingia ikulu ndiyo hajui kitu abisa . Yeye kaja na mbinu ya mwanafunzi kula uroda na kuzaa huku akiendelea kusoma. Kuondoa mitihani ya darasa la saba na kupunguza miaka ya elimu ya msingi. Pumbavu!
 
Amekerwa sana na uwepo wa Makonda kwenye CC. Concern yake ni too personal.
Hivi kweli Kwa mtu Mwenye akili timamu zile ziara za Makonda za kupanda Punda na watu kufurika kuleta malalamiko hadharani
Kule ni kujenga chama au kukiumbua chama kilicholala!!!

Aibu Kwa chama na Kwa aliye mteua

Alafu watu wenye akili wapo kimya!!!
 
""Ukikosa ushauri mzuri ama ukipata ushauri mzuri ukaupuuza hii nchi itakwenda kusikotakiwa kwenda. Ndio maana makongamano haya ni muhimu sana unachota mawazo,” amesema""

Kwacheo alicho wahi kuwanacho hakuwa na haja ya kuongea maneno kama hayo apo juu.
Makonda alishasemajuzi wastaafu watulie sijui kwanini haeleweki.
Nimekuelewa
Kwa Sasa Makonda ndiyo sauti ya Mama

Nandiyo maana majuzi mama kupitia Makonda alimdhalilisha Mwanamke mwenza
Kwaile kauli
Swali Hilo kamuulize "mamako"

Jambo hili Raisi asipo likemea hadharani no doa la "milele' kwake

Inashangaza UWT wapo kimya
Umoja wa awake Chadema kimya
Hata wanawake na wanaume walio zaliwa na wanawake kimya

Hili neno la dharau Kwa mama lisiachwe lipite hivi hivi ni Tusi kubwa Kwa jamii iliyo staarabika
 
Kwa nchi ambazo zinapima hata maelezo ya mtu tu kabla ya kumpa nafasi ya kugombea urais, Kikwete hakutakiwa kuwa rais.

Tatizo Tanzania hatupimi.

Kikwete anaweza kuwa anaelezea kitu, ukaona kafika katikati ya kukielezea, hajamaliza, halafu kumbe mwenzako ndiyo kashamaliza bila conclusion hapo.

Hata hiyo story ya Zacharia Hans Poppe sijui ni muandishi kafanya uzembe hakuandika conclusion ilikuwa vipi, au ni Kikwete mwenyewe hakutoa conclusion alilifanyia kazi vipi hilo suala.

Ila siwezi kushangaa ikiwa Kikwete katoa story nusu bila conclusion halafu kawaacha watu homework, fill in the blanks.

Ana tabia hiyo sana, halafu ni kama yeye mwenyewe haelewi kwamba amesema mambo in unfinished sentences.

Kikwete ana tabia ya kuongea kama vike watu wote wanaweza kuona anafikiria nini kichwani mwake, hivyo hata asipomalizia sentensi, wataelewa tu kwa kuona mawazo yake.

Unashangaa, huyu kapewaje urais?
Huu mwandiko wa Makonda😀😀😀
 
Eti ngano imepanda Bei Kwa Sababu ya Vita ya Ukraine Halafu akaishia hapo?

Hivi Nani aliua mashamba ya ngano kule Manyara ?
Hivi Tanzania inashindwa kuwatumia wataalamu Wa kilimo Wa ndani wakishirikiana na Majeshi yetu kama JKT na Magereza wakawekeza kwenye kilimo cha ngano na kuachana na mashoga Wa Ukrein na mabwana Zao?
Tanzania ni Kati ya nchi zenye idadi kubwa ya watu Duniani . Watu mil.61 kuishi Kwa kutegemea biashara za kuuza midoli vikorokoro Toka china Huku Chakula kikiwa kinategemewa Toka brazili,Ukraine na Misri ni huzuni kubwa sana .

Paulo Makonda yupo Sahihi.
JK atulie nyumbani kwake. Analifanya taifa hili liendelee kuwa Taifa Tegemezi.
Badala ya wataalamu kufanya Kazi wanashinda kwenye Maukumbi wakiwa Laptop na remote mkononi. Wanagawana pesa za walipa Kodi na mikopo .
Tunataka wasomi vijana wapewe Nafasi na mitaji . Vyama Vya ushirika viundwe upya na visimamiwe na vijana Wa WAKATI Huu. Hawa wazee ndio walioua mashamba yote ya serikali na Vyama Vya ushirika wakajigawia Kwa uroho na ubinafsi Halafu wakawakabidhi wahindi na Waarabu .
JK anatetea biashara zake . Hatumsikii akizungumzia masuala ya kilimo cha ndani, treni ya mwendo Kasi, umeme. Madini , ufugaji, Uvuvi kwenye Bahari kubwa na maziwa Mengi na mito ya kutosha.
Hatumsikii akizungumzia ni vipi bado tunategemea uchumi Wa Tozo na mikopo WAKATI yeye pamoja na Profesor Muhongo WAKATI wanafanya udalali Wa kuuza gesi yetu walituaminisha kuwa uchumi Wa nchi utapanda sana na patakua ña mfuko maalumu Wa kuweka Akiba Kwa ajili ya vizazi vijavyo .
Hayo nimatokeo ya kukithiri kwa rushwa mkuu. Viongozi wanawaza upigajitu sio maendeleo ya nchi.
 
Naweza kumwelewa JK, CC is supposed to be teamwork.
Makonda is uncontrollable, a stray missile.
Na kwamba alitumika na JPM basi also ni missile isiyo aminika.
Hatujasahau Makonda aliwahi kusema Riz anahusika na madawa ya kulevya!!
Tatizo JK ni mtu anakuambia kitu huku anacheka, lakini deep down tayari anafikiria next step.
A stray missile 😅😅 !
Let’s wait and see what is coming next !
Law of the Universe , What goes around comes around !

KARMA Is loading 🙏🙏🙏
 
Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema Serikali ikikosa ushauri mzuri ama ikipuuza nchi itakwenda pasipostahili.

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Novemba 22, 2023 alipokuwa akielezea umuhimu wa makongamano na mikutano katika kuishauri Serikali na Rais, kwenye mkutano wa nne wa Maendeleo ya Biashara na Uchumi ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) ambapo alikuwa mgeni rasmi.

“Ukikosa ushauri mzuri ama ukipata ushauri mzuri ukaupuuza hii nchi itakwenda kusikotakiwa kwenda. Ndio maana makongamano haya ni muhimu sana unachota mawazo,” amesema Kikwete aliyekuwa Rais wa nne wa Tanzania (2005-2015).

Amesema unapokuwa Rais hujui kila kitu lakini unatakiwa kushughulika na kila jambo na kwa sababu huwezi kujua kila kitu inakubidi kutegemea ushauri.

“Wenzako wanakuchagua kwamba unafaa kuwa Rais, lakini utakuwa hujui kila kitu, taaluma yako ni uchumi…lakini ukiwa Serikali na Rais hujui kila kitu. Kwa sababu huwezi kujua kila jambo, lazima utegemee sana ushauri,” amesema.

Amesema ndio maana Rais ana mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, makamishna, wakurugenzi na ofisi binafsi ambayo inawashauri.

Amewataka wasomi hao kutoa ushauri kwa Serikali juu ya mambo mazuri ya kufanya na kile ambacho si kizuri kiachwe na kirekebishwe.

Kikwete amesema uchumi hauwezi kukua bila uwekezaji, na unakuwa mahali ambapo mazingira ya biashara ni rafiki ikiwa vinginevyo wawekezaji wataondoka.

Ametoa mfano wa mfanyabiashara maarufu, marehemu Zacharia Hans Poppe ambaye wakati wa uhai wake alikutana naye nchini Afrika Kusini.

Amesema mfanyabiashara huyo alimweleza amehamishia biashara zake na magari yake yote nchini humo kutokana na mazingira ya biashara kutokaa vizuri nchini.

Amepongeza chuo hicho kwa kuandaa kongamano hilo, lakini akashauri kuangalia uwezekano wakuandaa lingine ambalo litashirikisha taasisi nyingine za elimu za juu.

Kikwete amesema kufanya utafiti ni njia ya kuboresha upeo na maarifa ya kila mtu na itasaidia katika maendeleo ya Taifa.

Bei za mafuta kupanda

Kikwete amesema iwapo bei ya mafuta imepanda katika nchi zinazozalisha ni wazi haiwezi kupungua nchini.

“Namshukuru Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa utashi wa kisiasa ameweka ruzuku ya Sh100 bilioni lakini hii inapunguza kwa senti chache. Wakishaweka ruzuku ya Sh100 bilioni bei ya mafuta inapanda tena.

“Kwa hiyo ndio mazingira tuliyonayo hadi wakimaliza vita (Ukraine na Israel) na kuruhusu mafuta yao kuingia katika soko tutakuwa na nafuu,”amesema.

Kikwete amesema hali hiyo ipo pia kwa mbolea, mafuta ya kula na ngano ambazo wazalishaji wakubwa ndio nchi hizo zinazopigana vita.

Amesema nchi moja tu ni vigumu kutatua, hivyo kunatakiwa kuwe na ushirikiano wa nchi zaidi ya moja.

Amesema hakuna nchi iliyopiga hatua za maendeleo kwa kujifungia yenyewe bila kushirikiana na nchi nyingine.

Aidha, amesema maendeleo ya nchi yoyote ya uchumi huchochewa na matumizi sahihi ya tafiti na ushauri wa kitaalamu, kinyume cha hapo maendeleo ni madogo.

Akizungumza awali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema sasa ni wakati wa kuwa na kozi fupi za wajasiriamali walioko nchini.

“Tumejiwekea malengo ya kuainisha wajasiriamali wale wanaoanza ndani ya mwaka mmoja tuweze kuwakuza baada ya miaka mitatu waweze kuwa wajasiriamali wa kati na hatimaye tutengeneze wafanyabiashara wakubwa na mabilionea,” amesema.

Amesema wao ndio wanaowafundisha wafanyabiashara wanapaswa kuwaonyesha namna ya kutoka walipo, mahali pa kupata mitaji ili waanzishe biashara.

Dk Kijaji amesema yapo machapisho duniani yanayoonyesha kuwa biashara baada ya miaka mitatu hufa, hivyo kuna kazi ambayo wao kama chuo hawajaifanya kikamilifu.

Naye Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Edda Luoga amesema tafiti zitakazokuwa bora zaidi katika kongamano hilo wanatarajia zitachapishwa kwenye majarida, kmtandao wa chuo hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho, Profesa Wineaster Anderson amesema wana mpango wa kupanua huduma zake ili kuwafikia walengwa wengi nchini na mipango hiyo inatazama zaidi visiwa vya Zanzibar, mikoa ya Lindi na Iringa.
Analalamika nchi wazalishaji wa bidhaa wako vitani, mbona hazungumzii kabisa matumizi ya gas kwakuwa alishaigawa kwa maswahiba wake na sasa yeye anafanya biashara ya mafuta, hazungumzii kabisa uwekezaji kwenye kilimo, mafuta ya kula yanaweza kuzalishwa kwa wingi Singida (alizeti), Dodoma (karanga), Kigoma (mawese)
 
Back
Top Bottom