Kikwete atetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

Kikwete atetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 akihoji, "Hivi ni kweli kwamba, sheria zetu zinazohusu uchaguzi ni mbaya sana kiasi kwamba haziwezi kusimamia mchakato wa uchaguzi mwaka huu?"
Ameyasema hayo leo Juni 21 katika ufungufu wa Kongamano la kitaifa la Sheria jijini Dar es Salaam.
View attachment 3377661
Huyu yeye kashiba
 
Chawa mpumbavu tu wewe utaishia kulamba viatu vya watawala,na utakufa na kuzikwa na ujinga wako
relax bas gentleaman,
mihemko na makasiriko ni ya nini sasa aisee lofa ambae hutakufa na werevu wako wa kuropoka?
 
B
Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 akihoji, "Hivi ni kweli kwamba, sheria zetu zinazohusu uchaguzi ni mbaya sana kiasi kwamba haziwezi kusimamia mchakato wa uchaguzi mwaka huu?"
Ameyasema hayo leo Juni 21 katika ufungufu wa Kongamano la kitaifa la Sheria jijini Dar es Salaam.
View attachment 3377661
Huyu mzee mshenzi sana. Kama walifanya maboresho ikawaje kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana 2024 Novemba wagombea wa Chadema zaidi ya 12000 walienguliwa?

Anasema Wakurugenzi sio wasimamizi hao Maofisa Waandamizi wana tofauti gani na hao Wakurugenzi?

Kwa nini Tume isiajili vijana wakawa Watumishi wake w kudumu? Ilihali kuna Watanzania wengi vijana hawana ajira?

Huyu mzee ameshiriki sana kulififisha hili Taifa. Na hajui tu ipo siku atajutia upuuzi anaowafanyia Watanzania kwa tamaa zake. Hapo linajipdndekeza ili Ridhiwani baadae aje kuwa Rais.
 
Chadema wamewaeleza wananchi jinsi mfumo huu wa uchaguzi pamoja na marekebisho yake, bado hautatenda haki.Mwenyekiti. wa tume,watuumishi wa umma wote hao ni wameajiriwa na rais ambaye ni mgombea.Cdm wamefunua macho wananchi kutotenda haki kwa mfumo uliopo.Watu wengi wanahoji kwa mini serikali ya ccm haikubali maoni ya kubadili huu mfumo ukawa wazi kwa wote.?Ni kipi kinachozuia?Hilo ndo mungejadili Taifa lijue.
 
Screenshot_2025-06-21-14-50-25-1.png
 
Hataishi Milele. Ataviacha vyote
Tena siku akiviacha vyote naomba raisi alieko madarakani awazilie kama walivofanya serikali ya Hechilema kwa Lungu, tuone hao wanafunzi na walimu wa kuwajaza mkapa kama watawapata, Maana sidhani kama Kuna mtu ataenda!
 
Uchaguzi wa 2020 nilifika mapema saa tatu na nusu kituoni kupiga kura, nilishangazwa na uwepo wa wapigakura wachache kituoni lakini maboksi ya kupigia kura karibu yote yalikuwa yamajaa karatasi za kura.

Nilimuuliza askari aliyekuwepo pale lindoni, mbona kama fréquence ya wapigakura kama ndogo? Jamaa akajibu kwa mkato tu, watu wameamka mapema wamekuja kupiga kura, wamemaliza kazi hiyo wanaendelea na shughuli zao....

Matokeo yalipotoka ilokuwa dhahiri kuwa kulikuwa na mpango wa kuiba kura kwa kuipendelea CCM dhidi ya upinzani, kwa jinsi Rais wakati huo John Pombe Magufuli alivyofanya kazi inayopigiwa mifano hadi siku ya leo ....Sikuona kabisa sababu ya CCM na vyombo vya Dola kupanga njama za ushindi wa kishindo.

Kikwete anashangaa na kujiaminisha kuwa mambo yako sawa... Kama kweli hivyo ndivyo basi huo uchaguzi uendelee tu ili tupate matokeo yatakayoonyesha nani yuko sahihi kati ya wanaotaka Reforms zifanyike tena kabla ya uchaguzi na wale wanaodai reforms zimeishafanyika.
 
Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 akihoji, "Hivi ni kweli kwamba, sheria zetu zinazohusu uchaguzi ni mbaya sana kiasi kwamba haziwezi kusimamia mchakato wa uchaguzi mwaka huu?"
Ameyasema hayo leo Juni 21 katika ufungufu wa Kongamano la kitaifa la Sheria jijini Dar es Salaam.
View attachment 3377661

PUBLIC BAR ASSOCIATION CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI MGENI RASMI RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
1750508691535.jpeg

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali nchini, msomi Bavoo Junus, amesema kuwa Kongamano la Kitaifa la Sheria litafanyika kesho Jumamosi, Juni 21, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali amesema hayo leo Juni 20, 2025, jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, na kongamano hili linaandaliwa na Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (Public Bar Association).

“Moja kati ya malengo ya kuanzishwa kwa Chama cha Mawakili wa Serikali ni kuwaunganisha mawakili wa serikali wanaotoka katika maeneo mbalimbali, kuwaleta pamoja ili kuweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sheria, lakini pia lengo lingine la msingi la kuanzishwa kwa chama ni kukifanya chama kiwe jukwaa la kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi kwa sababu serikali inawajibika kwa wananchi, kwa maana hiyo sisi ni mawakili wa wananchi,” amesema Junus.

Aidha, ameongeza kuwa Chama cha Mawakili (Public Bar Association ) kina jukumu la kutoa elimu katika masuala mbalimbali ya kisheria, hususan katika mambo yanayogusa maslahi mapana ya taifa.

Sasa katika kutekeleza jukumu la kutoa elimu kwa umma, na kwa kuzingatia tunaenda katika uchaguzi mkuu, chama kimeandaa kongamano ambalo lengo lake kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi mkuu
 
PUBLIC BAR ASSOCIATION CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI MGENI RASMI RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
View attachment 3377780
Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali nchini, msomi Bavoo Junus, amesema kuwa Kongamano la Kitaifa la Sheria litafanyika kesho Jumamosi, Juni 21, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali amesema hayo leo Juni 20, 2025, jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, na kongamano hili linaandaliwa na Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (Public Bar Association).

“Moja kati ya malengo ya kuanzishwa kwa Chama cha Mawakili wa Serikali ni kuwaunganisha mawakili wa serikali wanaotoka katika maeneo mbalimbali, kuwaleta pamoja ili kuweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sheria, lakini pia lengo lingine la msingi la kuanzishwa kwa chama ni kukifanya chama kiwe jukwaa la kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi kwa sababu serikali inawajibika kwa wananchi, kwa maana hiyo sisi ni mawakili wa wananchi,” amesema Junus.

Aidha, ameongeza kuwa Chama cha Mawakili (Public Bar Association ) kina jukumu la kutoa elimu katika masuala mbalimbali ya kisheria, hususan katika mambo yanayogusa maslahi mapana ya taifa.

Sasa katika kutekeleza jukumu la kutoa elimu kwa umma, na kwa kuzingatia tunaenda katika uchaguzi mkuu, chama kimeandaa kongamano ambalo lengo lake kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi

"TUMETAPAKAA NCHI NZIMA, TUNAELEKEA OKTOBA 2025 HIVYO TUMEJIANDAA KUTOA ELIMU "....

View: https://m.youtube.com/watch?v=nclLbxW74YY
Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania, msomi Bavoo Junus akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Junus na kufafanua chama cha mawakili wa serikali (Public Bar Association) wanachama ni wale walio katika utumishi wa umma yaani serikalini na taasisi za umma na idadi yao wapo zaidi ya 5,000.

Chama sasa kinakuwa jukwaa kwa kutoa elimu kwa umma, hivyo Public Bar Association inazingatia tunaelekea October 2025 ni wakati muafaka sisi kama chama cha mawakili kutoa elimu sahihi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025

 
Kikwete ameuliza swali la msingi. Hivi wale wanao haribu uchaguzi wanafanya hivyo kwa sababu sheria na Katiba zilizopo zinawaruhusu au wanazikiuka? Mtu anapomuengua mgombea ambae ni mwanasheria kwa kudai kuwa hajui kuandika na kusoma anafanya hivyo kwa sababu sheria zinamtaka kufanya hivyo? Na kama akifanya hivyo anakiuka sheria na Katiba zilizopo anapata wapi ubavu wa kufanya hivyo?

Kwa mtazamo wangu binafsi, maboresho yanayotakiwa ni yale ya kumfanya mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuogopa kufanya hivyo. Kwa mfano, kama patakuwa na kipengele kuwa ikithibitika kuwa kura zisizo halali zimehesabiwa katika kituo cha kupigia kura, msimamizi wa kituo hicho atashtakiwa binafsi na akipatikana na hatia atatumikia kifungo. Hii itahusu kura zilizoingizwa kwenye maboksi kabla ya muda, kura za kughushi, kura zisizoendana na idadi ya waliojiandikisha kupiga kura n.k. Mgombea awe na haki ya kudai kura zihesabiwe tena kwa uwazi kama hajaridhika na matokeo. Chama chochote cha kisiasa kilicho sajiliwa kiwe na haki ya kufungua hayo mashtaka kwenye Mahakama maalum ya wazi ambayo itawajibika kusikiliza hayo mashtaka na kutolea uamuzi kabla ya matokeo kutangazwa na kuthibitishwa. Atakaeshindwa atakuwa na haki ya kukata rufaa. Haki ya wagombea kushuhudia kura zikihesabiwa na kuchukua kumbukumbu (video n.k.) izingatiwe.

Hivyo hivyo kwa msimamizi yeyote wa uchaguzi ambae atathibitishwa kuwa hakuwatendea haki wagombea ( kuwaengua kwa sababu za kijinga, kutokuwepo ofisini wakati wa kupokea fomu za uchaguzi n.k.). Msimamizi wa uchaguzi atakiwe kuthibitisha kuwa fomu zimejazwa kwa usahihi siku moja kabla ya siku ya mwisho ya kuzirejesha na kama kuna mapungufu kuyaainisha kwa maandishi ili mgombea aweze kurekebisha kabla ya dirisha kufungwa.

Nadhani wasimamizi corrupt wakichukuliwa hatua kama criminals, imani itaanza kurudi katika mfumo mzima wa uchaguzi.

Amandla...
 
Kikwete hana hadhi tena ya mstaafu mwenye busara, ni mhuni kama wahuni wengine
Huyu ni zaidi ya muhuni.
Huyu ndiye adui mkubwa sasa hivi wa nchi hii. Ni muhimu watu wamtambue hivyo.

Kwa vile anaendelea na uhujumu wa taifa hili, moja ya njia za kujisafisha baada ya kuondoa uchafu uliopo sasa huyu inabidi aondolewe hadhi na heshima zote za kuwahi kuwa kiongozi wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom