Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

- Kama CC ya CCM itashindwa kumzuia Lowassa asigombee kama ilivyofanya mara mbili kwa Mzee wetu JSM ambaye hatujawahi kuelezwa kosa lake ni nini hasa;
- Kama UwT nao watashindwa kuwashawishi CCM kuliondoa mapema jina la mlafi huyu kama walivyomwacha JMK akampa UwaziriMkuu wa NCHI yetu;
- Kama vyombo vya habari navyo vitajiingiza kwenye kampeni chafu dhidi ya wagombea wengine SAFI ili kumsaidia Lowasa kama walivyofanya akina Salva mwaka 2005;
- Kama KATIBA MPYA haitakuwa na MIIKO na SIFA nzito za KIONGOZI MKUU wa TAIFA hili;

TANZANIA kama TAIFA baada ya 2015 iko mashakani.
 
August, nakuomba uamini sio kweli watetezi wote wa Lowassa humu wamelipwa!. Just amini hivyo!.
Mimi Pasco (wa jf) ni mmoja wa watetezi wa Lowassa ateuliwe kuwa mgombea wa CCM nikiwa sina chama wala sijapewa senti tano ya mtu awaye yote!.

Nature ya mwanadamu inadictate kuwa lazima kuna motive inakudrive kufanya uamini kitu/mtu bila malipo yeyote. Only logical proposition labda kama alivyosema mtoahabari unaweza kuwa ni big fan wa Mh. WILLIAM HAGUE. Wewe uliyepo nje hujui huku bongo tumechoka kiasi gani na huyu mtu.
 

Wrong thinking. We have to remain positive on others unless propelled by positive and constructive evidence to think otherwise.

Hii dhana ya kila anayefikiria tofauti KAHONGWA au kuna kitu ndo inafanya Tanzania haiendelei. Tumejifungia kwenye BOX. Vipi ukiambiwa kuna kitu najua ambacho sitaki kusema kwa hao mnaoona wanafaa ambacho ni kibaya kuliko mabaya mnayozungumzia ya EL?.

Anyway, acha sisi tuendelee kufunga mikanda kwenye ELairline.
 
The boss, unazungumzia laana mara ngapi?. Hii iliyopo haitoshi?!. Ndio maana tunataka ukombozi na ukombozi huo ni kwa kupitia kwake!.

Najaribu sana kukuelewa Pasco kupitia post zako mbalimbali. Mwshowe, nafikiri unamaanisha kuwa kupitia kwake, itakuwa rahisi kwa upinzani kuchukua uongozi i.e. kama akichaguliwa kuwa mgombea urais wa CCM. Kwa maneno mengine, si yeye atakayeleta ukombozi huo moja kwa moja, ila unaombea na unashabikia ili CCM wafanye kosa la kumruhusu yeye kuwa mgombea.
 

LOL ahahaha Umenichekesha.
 


haki ya nani mkuu una ujasiri balaa.......nakushauri walau uwe na parachuti pembeni maana.....!!!!
 
haki ya nani mkuu una ujasiri balaa.......nakushauri walau uwe na parachuti pembeni maana.....!!!!

Edson,
Haki ya nani nimecheka balaa mpaka naulizwa na my waifu nacheka nini! ahahahaha yaani una mambo?

Vipi lakini usharudi Bongo?. Sio ujasiri ndugu yangu, Ninaaamini hivyo. Lowassa ndie anafaa.

Karibu basi hata economy class ya ELairline!
 

Hii post namba 763 inamaliza propaganda zote za kina Fair Play, Pasco na wenzao. Mbona hawaijibu, na wanajifanya hawajaiona? Lowasa ana uthubutu , ( au Kama Mwakyembe alivyosema, "UJASIRI WA KIFISADI") wa Kifisadi.....sasa kama huo ndo akina Pasco mnautetea basi mko sahihi. Basi na mpigieni debe huyo "Jasiri" wenu ili nchi hii igeuke Mexico nyingine. Maana hapa Lowasa akipita, ni kwamba nchii hii haitatawalika , kwa vile makundi yaliyopo yote yatajianzishia "empire" zao ndani ya nchi hii, na mwisho tutawaliwe kwa "Cartels" za walevi hawa wa madaraka, kama zilivyo DRUG Cartels za Mexico. God Forbid!
 
Wee Chief, usitake kutuharibia kampeni ya mgombea wetu, Lowassa msafi, mtakatifu!

Wewe hushangai Mzee Mwanakijiji hachangii thread hii?. Ameelewa soma na kujikalia kimya, waelewa wameelewa tunasimamia wapi, ndio maana na sisitiza ukombozi wa kweli wa nchi hii utapatikana kupitia kwake!.

CCM siku zote inashinda chaguzi mbalimbali kwa sababu inapendwa sana!, sio kwa kutake advantage ya ignorance yetu sisi Watanzania hivyo CCM hata wakisimamisha jiwe tuu litapita, sembuse Lowassa!.

Sasa baada ya kulielewa somo, tuungane, tumsafishe Lowassa, tumpake mafuta ang'are na kumeremeta, tumpulizie na manukato anukie vizuri, apendeke na kuongeza mvuto, CCM wamsimamishe awe mgombea wao!.
 
Mkuu Nyumbu hii tuliiona na tuliijibu, Lowassa ndiye atachaguliwa na ataigeuza nchi hii ya Tanzania kuwa ni nchi ya ahadi, nchi ya maziwa na asali!
 

Hewala, nimekuelewa.
 
Hewala, nimekuelewa.

Kumbe mna akili hivyo sasa kwanini toka zamani hamjiungi na ELairline?

Kauli mbiu hapa JF ELairline for 2015! hiyo ndo inatakiwa iwe salamu yetu humu watu wa EL hapa JF.
Pasco ukiiona ipo sawa basi tui endorse ianze kutumika. Kabla ya kuandika chochote tunaanza na hilo.
 

Hili bandiko ni matusi kwa baadhi yetu. Nitalitafuta na kulirejesha baada ya uchaguzi mkuu 2015 kama nitakuwa hai.
 
Pasco and company ya watetezi wa Lowassa,hatupingia au kutomtaka kwetu EL kuongooza nchi yetu si kwa sababu ya Richmond scum na hata sasa wanaomshabikia au kumchukia Lowassa sababu ya Richmond labda hawamfahamu vizuri.BTW sisi wengine kwa kuitakia mema nchi hii na kuiepusha janga(Lowassa) lingine kubwa ni ripoti ya mwalimu Nyerere kuhusu Lowassa na ukwasi aliovuna kwa kipindi kifupi akiwa mtumishi wa umma.Haya mengine ya kulawiti wanaume wenzie na wizi na ufisadi mwingine baada ya kuwa waziri mkuu ni muendelezo tu wa nia yake ovu juu ya nchi hii na uthibitisho wa dhahiri kwa walio-doubt ripoti ya Mwalimu au wale wasiomfahamu EL kwa undani.
 

Kwani wewe huwezi kupima au kuona au kuelewa na kutoa mtazamo wako mpaka umtegemee MWALIMU(rip)?
MIE MAWAZO TEGEMEZI SIYAPENDI KABISA
 
The problem we are having is that; every body thinks that old people a wise and a true leaders. But be assured that is not applicable here in Tanzania and never will.

For CCM none who is mentioned is clean so for the next president i don't see anybody. they are all thieves and liars.

For the seak for of the new nation we are having so many educated young Boy and Girls, and i think we should take this opportunity and become true and patriotic leaders by claiming back our country from this traitors.

Am tied of all these people mention above because i know surely what they deserve is to stay behind bar at Keko period and all their properties taken.
 

Mkuu Keil,
Nakubaliana na wewe kwamba uwazi katika siasa na mahali pengine ni kitu muhimu sana. Lowassa na viongozi wenzake wameshindwa kabisa kusema vyanzo vya utajiri wao usio na idadi , ndio sababu mpaka sasa hawajakabidhi tamko la mali zao kwa sekretarieti ya maadili ya umma, kwa kuwa hazitamkiki/hazina maelezo timilifu namna zilivyopatikana.


Sipati picha hii Kamati Kuu ambayo Mwalimu aliagiza iitwe kwa gharama zake kwa ajili ya "KUMTETEA" (if any, at all) mtu ambaye hana imani naye hata tone, ingetoka na maazimio gani katika kikao hicho. Hatujaambiwa pia ni kwanini huyu 'Rais' mtarajiwa hakuhudhuria kikao hicho cha ana kwa ana na Mwalimu pale Msasani. Pasco tupe jibu, hope unafahamu.

...Kwa utetezi wangu kwa Lowassa bora tugombane tuu kwa sasa akishateuliwa tutapatana tuu!.
Mkuu Pasco,
Katiba inakuruhusu kuwa na msimamo huo, na uko sahihi. Unaweza kutupa mwanga kidogo kuhusu hoja za Kasori juu ya mgombea wetu mtarajiwa? Kwa nini hakwenda Msasani 'Kusafishwa' alipoitwa? Aliomba msaada wa Nyerere kusafishwa, je juhidi hizi zilifia wapi?

...SMU nakuhakikishia asilimia 100% kwa 100% utetezi wangu kwa EL ni kwa maslahi ya taifa!. Sina maslahi binafsi yoyote na sijapokea hata senti tano ya yeyote!
Mh. I smell something here. Hujaahidiwa kuteuliwa kweli?

- Kama CC ya CCM itashindwa kumzuia Lowassa asigombee kama ilivyofanya mara mbili kwa Mzee wetu JSM ambaye hatujawahi kuelezwa kosa lake ni nini hasa;..
WC,
Wewe ni mkongwe sana hapa JF, ina maana mpaka leo hujajua kwa nini JSM alienguliwa katika kugombea urais? Mbona tumeandika sana na hajakanusha? Suala ni kwamba, wakati wa hoja ya kuanzishwa serikali ya Tanganyika iliyopepelekwa na wabunge waliojiita G55 wakiongozwa na mbunge wa Chunya Mhe. Njellu Kassaka, JSM alikuwa waziri mkuu (kiongozi wa shughuli za serikali bungeni). JSM alishindwa kuwakemea wabunge wa chama chake kuacha hoja hiyo, kwa sababu si ilani ya chama chao na wala chama hakikuwatuma kwenda kuianzisha na kuitetea, hivyo walikuwa wanakiuka katiba ya chama. Kukiuka katiba ya chama kilichokuweka madarakanini makosa, hivyo wabunge hawa (G55) walikukua wamekosea sana.
Mantiki ikawa kwamba, kama alipokuwa waziri mkuu, alishindwa kusimamia kufutwa kwa hoja ndogo kama ile kiasi kwamba ikaleta rabsha bungeni na kutaka kugawa nchi, je akiwa raisi si ndo ataua muungano kabisa? Sababu hii ilitosha kabisa kumnyima ugombea. Hakuwa na msimamo. Hakuaminika. Soma kitabu cha 'Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania', kimekuwa-uploaded hapo juu kwenye jukwaa hili.
 

Aliguswa na wizi, ukwapuaji, ufisadi, udini, uuaji na ushirikiana tuu! hana lolote!! his days are numbered! hata kama atakwapua kiasi gani zijui atazitafunia wapi!! ha! ha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…