Mkuu wangu FP,
Leo naomba niwe na Fikira Duni [zama zile za enzi na enzi]. Sidhani kama Tanzania ya leo inahitaji kiongozi aina ya Lowassa. Tanzania ya leo inahitaji kiongozi mwadilifu, asiye na makundi, asiye na mtandao na awe mchapa kazi. Katika hayo yote Lowassa ana sifa moja tu ya uchapa kazi, ambayo kila mtu anaweza kuwa nayo.
Hoja ya UTHUBUTU: Tanzania ina viongozi wengi sana ambao wana UTHUBUTU, lakini je huo uthubutu wanautumia kwa malengo yepi?
Tukumbushane kidogo: Mkapa alishawahi kuonyesha uthubutu pale alipowasemea mbovu wafadhili [specifically UK] pale Mama Clare Short alipojiuzulu kwa kitendo cha BAE kutuuzia radar. Mkapa alionyesha mamlaka na uthubutu wa kufanya maamuzi, kwamba serikali imeridhia kununua radar, lakini ukweli ni kwamba it was a "deal". Wapo waliosema Mkapa ni mwanaume anawakoromea mpaka wafadhili. Leo hii kiko wapi? Radar aliyoitetea imekuja kugundulika ni dili na tena waliogundua ni hao hao aliowatukana. Serikali iko kimya, imepewa details zote za mgao wa fedha, je imefanya nini?
Mkapa alikuwa ni champion wa globalization, watu wakasema Tanzania inaelekea kwenye neema na kwamba ni moja ya top destinations za FDI kwa Sub-Saharan Africa. Kiko wapi? Kumbe hao wawekezaji wote walikuwa ni wapiga dili tu kwenye migodi. Unakumbuka Mkapa alivyokuwa anatetea wawekezaji wa kwenye sekta ya madini? Unakumbuka alivyotumia FFU kuwaingiza NetGroup Solution? Viongozi wetu wengi wana uthubutu na pia huwa wanaonyesha mamlaka, lakini uthubutu wao mara nyingi uthubutu wao na mamlaka waliyonayo huwa wanayatumia kwa faida yao wenyewe, familia zao na marafiki zao. Huo ni uthubutu wa kifisadi wa kuwaambia wananchi wale nyasi na huku yeye anapokea 10%! Huo ni uthubutu wa kifisadi.
Richmond ambayo ndio imekuwa kitanzi cha Lowassa, wengi wamemtetea kwamba hilo halikuwa zigo lake bali la JK. Yeye akiwa Waziri Mkuu ilikuwaje akakubali kutumiwa na huku akiona kabisa kwamba mwelekeo haukuwa mzuri? Kiongozi mwenye uthubutu wa uadilifu angejiweka pembeni. Kama yale maneno ambayo yaliandikwa kwenye magazeti kwamba Lowassa alimpigia simu JK akiwa ughaibuni kwamba wavunje mkataba na Richmond na Rais akasema amepewa ushauri mpya na Kamati ya Makatibu Wakuu, kwanini baada ya hapo Lowassa hakujiweka kando? Huo ndio uthubutu wa uadilifu kwamba umetoa ushauri mzuri na ukaona hausikilizwi, kaa pembeni badala ya kupendekeza kuingizwa mikenge mingine.
Bado watetezi wanasema kwamba baada ya JK kuona Richmond imekwama, JK aliomba ushauri kwa Lowassa. Lowassa akasema kuna mtu mmoja [Rostam Aziz] anaweza kutusaidia, na ndio tukaingizwa mkenge mwingine wa Dowans ambayo bado inawatesa mpaka leo. Kiongozi mwenye uthubutu hawezi kutafuta short cuts kwa kuwatumia marafiki zake ili kutatua matatizo makubwa kama hayo. Kiongozi mwenye uthubutu angependekeza kusitisha mkataba wa Richmond na kushauri mchakato uanze upya badala ya kupendekeza kuuingia mkenge mwingine.
Msimamo wangu siku zote ni huu, ndani ya CCM hakuna ambaye ana afadhali au ambaye anafaa kuwa Rais kwa sasa. Wengi wao wana uthubutu, wanajua mamlaka waliyo nayo lakini huwa wanaishia kutumia uthubutu huo na mamlaka kwa faida yao wenyewe na kulindana within CCM circles.
Sababu zinazonifanya niwaogope viongozi kutoka CCM ni hizi:
Hakuna mwana CCM atakayechaguliwa kuwa Rais ambaye atakuwa tayari kushughulikia maswala yote ya ufisadi kwa kuwa ndani ya CCM wapo ambao ni "untouchables" na ndio wamefanya ufisadi mkubwa sana ndani ya nchi hii. Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alisema tuhuma za ufisadi/rushwa zinatosha sana kumsimamisha kazi kiongozi wa umma. Kipande cha maneno hayo kilikuwa kikirushwa sana na Redio Tumaini, Redio ya Ujirani. Kauli hiyo ilikuwa ni mwiba mchungu wenye ukweli, kwamba mtu aliahidi kupambana na rushwa na ufisadi lakini alipoingia madarakani akawa fisadi namba moja na mla rushwa mkubwa. That was our dearest Mr. Clean!
JK alipoiingia madarakani watu walikuwa na matumaini makubwa sana kwamba ufisadi uliofanyika chini ya Mkapa ungeshughulikiwa na kama unakumbuka watu walikuwa wakisubiri kwa shauku sana outcome ya ziara ya JK pale BoT wakijua kwamba kitendawili cha Twin Towers kingeteguliwa, maana ndio kilichokuwa kikijulikana wakati huo. Dili za EPA zilikuwa bado hazijawa wazi. Siku JK alipoingia BOT waandishi walizuwiliwa na hakuna anayejua kilichoongelewa huko ndani na hakuna kilichotokea baada ya hapo. Serikali imesubiri mpaka Ballali kafa ndo wanakuja kupeleka kesi ya Twin Towers mahakamani wakati shahidi mkuu ameishapotea. JK alisema nyumba za serikali zingerudi, zilirudi? Alisema mikataba ya madini itapitiwa upya na kusitisha kusaini mikataba mipya, je imeishapitiwa? Sana sana tulishuhudia sakata la Mkataba wa Buzwagi ukisainiwa. Hayo yote yanakuonyesha kwamba JK alikuwa na nia au alionyesha uthubutu hata wa kutamka tu kwamba atayashughulikia, leo hii muulize kulikoni hayajashughulikiwa? Hakuna jibu la kueleweka sana sana anajuta kwanini aliahidi hayo na ndio maana 2010 akaja ahadi mpya zaidi ya 80 na kwa kuwa Tanzagiza ni taifa la wadanganyika, tayari walishasahau na kuamini ahadi mpya za kwenye kampeni.
Mfumo wa CCM uliopo ni wa kulindana. Sophia Simba alishasema kwamba ndani ya CCM hakuna msafi, once wakianza kunyoosheana vidole hakuna atakayesalimika. SO, kabla mtu hajawa rais lazima kwanza mafisadi wakuu wajiridhishe kwamba atacheza kwa tune wanayoitaka wao na kwamba hawezi kufunua mfuniko uliofunika uozo wa ufisadi uliofanywa na CCM na serikali yake. Ndo maana unawasikia akina Pinda wanamtetea Mkapa kwamba tumwache apumzike halafu wanasema Kiwira itarudi serikalini, tena bila aibu kabisa. Pinda huyo huyo anaonyesha jazba kwa Jairo na wakurugenzi wengine wa vimiji huko swekeni, lakini ukimtajia jina la Mkapa ananywea na kuanza kujiuma uma, ukitaja Meremeta anasema yuko tayari kusulubiwa lakini hawezi kuongelea hilo swala! Ukisema EPA anasema mafisadi wana nguvu sana, hivi kuna mtu ana nguvu kuliko serikali iliyo madarakani iliyo na vyombo vya dola kila kona?
Kwa hiyo hata kama mwana CCM angekuwa mwadilifu kiasi gani, akishapewa Urais kupitia CCM lazima alinde maslahi ya chama chake na serikali zilizotangulia. Ndio maana Lowassa alisema alikubali kujizulu ili kulinda heshima ya chama chake na serikali. Kama angegoma kujiuzulu basi maana yake ni kwamba serikali yote [hapa ninamaanisha kuanzia JK] ingedondoka! Sidhani kama huo ndio Uthubutu unaousema wewe. Kama kweli Lowassa ana uthubutu, basi angeanzia hapo kwa kusema kila kitu kwa uwazi na baada ya hapo anaweka wazi kwamba alikuwa anatumwa na JK kutekeleza maagizo. Huo ndio uthubutu wa kuwa mkweli kwa wananchi unaowaongoza na pia uthubutu wa kufanya maamuzi ambayo hayawaumizi wananchi au kuwaongezea mzigo. Je, kama Lowassa alijiuzulu ili kumlinda rafiki yake [JK] na chama chao, siku yeye [Lowassa] akipewa urais na akaja kuona kuna watu wa JK au vigogo wa CCM wanahusika na ufisadi, tuna hakika gani kwamba ataonyesha utthubutu kwa kuwashughulikia kwenye vyombo vya sheria?
Uthubutu ndani ya CCM haupo, kwa sababu ya mfumo wa kulindana. Kwa hiyo labda tutafute hoja nyingine na sio uthubutu ambao una dalili zote za kifisadi au kulinda ufisadi. Unakumbuka Sitta alipopelekewa nondo za ufisadi na Dr. Slaa? Alisema Slaa ni mzushi mara sijui anatumia info za kwenye mitandao ambazo hazina ushahidi. Sitta huyo huyo leo kuna watu wanasema ana uthubutu wa kutumia mamlaka ya Spika kumsulubu Zitto na kudanganya umma kwamba Dr. Slaa alighushi documents za ufisadi! Siku Zitto anasulubiwa baadaye Lowassa alitoa hotuba ya kufunga kuahirisha Bunge na kuishia kutishia wabunge kwamba wasicheze na serikali na kwamba kilichotokea kwa Zitto ilikuwa ni mvua za rasha rasha tu. Hiyo pekee inaonyesha wazi kwamba uthubutu wa Lowassa una walakini mkubwa sana. Mtu mwenye uthubutu wenye dhamira nzuri hawezi kutishia wananchi/wabunge kwamba watashughulikiwa. Kama serikali ni safi, kwanini iogope hoja za wabunge?
CCM haiwezi kutoa kiongozi [Rais] ambaye atakuja kubadilisha direction ya airline [kwa kutumia maneno yako] ili Tanzania isiende chini. Tayari tuko chini, na tukipata kiongozi mwingine kutoka CCM atakuwa anachimba ardhi ambayo ndio itakuwa kaburi yetu kama nchi.