Kama Iddi Amini alikua ni Mtu mwema,Nini chanzo cha Vita ya Kagera!!? Unataka kusema Nyerere ndiyo hakua Mtu mwema hadi akamvamia Amini na kumchapa!!?
Suala la Idd Amini ni gumu sana!!
Anyway, kwamba alikuwa mwema, HAKUWA NA WEMA HUO!! Iddi Amini alikuwa muuaji, PERIOD!! Hana tofauti na Madikteta wengine wengi duniani! Hata hivyo, cha ajabu hata Uganda kwenyewe kuna watu wengi sana ambao wanaona Iddi Amin ni National Hero!
Niliwahi kusoma makala moja ya France24 ambayo walienda Uganda kutengeneza documentary kuhusu 40 Years After Iddi Amin!
France24 wenyewe wanasema walishangaa sana kukuta watu wana mitazamo tofauti! In short, ni Wazee ndio wanamuona Iddi Amin alikuwa mtu mbaya lakini asilimia kubwa ya vijana, Amin kwao ni National Hero!
Tukirudi kwenye Vita ya Kagera... ukweli usemwe, na mara nyingi nimesema kuhusu hilo! Ile vita tulijitakia wenyewe kwa sababu Mwalimu ALIMCHOKOZA KICHAA!!
Sitaeleza kwa undani kwa sababu hapa sio pahala pake!
REMEMBER: Iddi Amin alimpindua Milton Obotte. Mwalimu Nyerere na Obotte walikuwa MARAFIKI WAKUBWA, kwahiyo Mwalimu akampa Obotte hifadhi ya muda jijini Dar es salaam.
Mwalimu hakufanya kosa kumpa Obotte hifadhi. Baada ya Obotte kuja Tanzania, maelfu ya Wafuasi wake nao wakavuka mpaka na kuingia Tanzania.
Alipokuja kukosea Mwalimu ni kuwapeleka Wafuasi wa Obotte kwenye Kambi ya JKT, Handeni. Kule wale Wafuasi wakaanza kuchukua mafunzo ya kijeshi ili baadae warudi Uganda kumpindua Amin.
Hiyo ilikuwa ni Covert Op iliyokuwa inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania, na kweli, mwaka 1971, wale wa Wafuasi wa Obotte wakaondoka TZ hadi Uganda kufanya jaribio la kumpindua Obotte!
Sijui hawakuchanga karata zao vema, jaribio lao dhidi ya Amin lika-fail na wakachakazwa vibaya sana. Wale waliobaki, wakakimbia na kuvuka mpaka tena hadi Tanzania kujiandaa na jaribio lingine.
Hapo ndipo ulipoanza uadui kati ya Mwalimu na Iddi Amini! So, can you blame him?! Ni rais gani anaweza kui-entertain jirani anayefadhili covert op dhidi yake?