Kila mtu amezaliwa akiwa muislamu, ubatizo ndio unaomfanya mtu kuwa mkristu

Kila mtu amezaliwa akiwa muislamu, ubatizo ndio unaomfanya mtu kuwa mkristu

U

Ufuasi wa Dini ni utahira hasa kwa waafrica amka uliko lala acha kuamini hadithi za uongo za mtu mwehu eti mtume bullshit
Wewe ndo hujui lolote kuhusu imani...
Unajua kuwa siku ya mwisho kuna kufufuliwa..
Acha kujimwambafai sawa kuna siku ardhi unayolingia juu yake inakubana kijana
 
Wewe ndo hujui lolote kuhusu imani...
Unajua kuwa siku ya mwisho kuna kufufuliwa..
Acha kujimwambafai sawa kuna siku ardhi unayolingia juu yake inakubana kijana
Mimi siamini dini yeyote bahati nzur, na kuhusu ardhi kunibana hata ww litakutokea hilo japo mi siamini huo upuuzi, ebu acheni uvivu wa kufikiri yaan kisa tu umekuta babaako na mamaako wanafuata hayo ukakuzwa kwenye hayo hata ulipo pata akili zako huwezi changanua mambo kweli uyapime come on
 
Kama yapi ya kuchanganua mkuu..
Hivi wewe huoni hv nyie waja mbona hamna fadhira.. hivi wewe umejiumba... Hv unaweza kuta nyumba imejijenga tu bila kuwepo wahusika...

Ebu grow up mkuu achana na elimu za kizungu za kukupumbaza.. kuna mambo lazima ujiongeze kwanini wanakupotosha mkuu
 
Ni fact na ndo ukweli huo...
Tatizo wengi wamepumbazwa na ilmu
Loh! Ina maana uislam ni dhambi?
Ni kweli kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa na dhambi asili aliyoirithi toka kwa wazazi wake wa mwanzo, Adamu na Eva. Hivyo kusema kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa muislam, basi inamaanisha uislam ni dhambi. Na hiyo dhambi unaiondoa kwa kubatizwa kuwa mkristo.

Waislam, bila shaka mmeupata ujumbe sawia toka kwa sgekhe aliyeongozwa na roho mtakatifu, kuwa kila mwanadamu anazaluwa akiwa mdhambi/muislam. Na hiyo hali utaiondoa kwa kubatizwa.
 
Kama yapi ya kuchanganua mkuu..
Hivi wewe huoni hv nyie waja mbona hamna fadhira.. hivi wewe umejiumba... Hv unaweza kuta nyumba imejijenga tu bila kuwepo wahusika...

Ebu grow up mkuu achana na elimu za kizungu za kukupumbaza.. kuna mambo lazima ujiongeze kwanini wanakupotosha mku
Bro we ndo umepotoshwa coz umeaminishwa tu na umeyabeba jins yalibo without questioning wala reasoning mi japo sjakwambia kua naamini katika elimu za kizungu lakin huku ni facts,reasoning pamoja na kufikiri kwa kina ndo msingi si kuamini amini tu hovyo
 
Loh! Ina maana uislam ni dhambi?
Ni kweli kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa na dhambi asili aliyoirithi toka kwa wazazi wake wa mwanzo, Adamu na Eva. Hivyo kusema kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa muislam, basi inamaanisha uislam ni dhambi. Na hiyo dhambi unaiondoa kwa kubatizwa kuwa mkristo.

Waislam, bila shaka mmeupata ujumbe sawia toka kwa sgekhe aliyeongozwa na roho mtakatifu, kuwa kila mwanadamu anazaluwa akiwa mdhambi/muislam. Na hiyo hali utaiondoa kwa kubatizwa.
Acha ukafiri..
Hakuna tuzo kuwa kafiri...
Hakuna tuzo wewe kuwa kafiri na kutofata maamlisho ya allah mkuu..

Kuna siku moja tu utaamini kwamba Mungu ni mmoja tu na utajuta kwanini hukubaki na dini yako toka ukivyozaliwa...

Utabaki unashangaa wakati mda huo kuna wenzako wanainjoi maisha
 
Bro we ndo umepotoshwa coz umeaminishwa tu na umeyabeba jins yalibo without questioning wala reasoning mi japo sjakwambia kua naamini katika elimu za kizungu lakin huku ni facts,reasoning pamoja na kufikiri kwa kina ndo msingi si kuamini amini tu hovyo
Mi mwenyewe nafanya rezoning..
Hvi unajua unajigamba sana bila kujua kuna siku moja tu ambayo viungo vyako ndo vitaongea yote hayo..

Jaribu kuwaza kesho yako mkuu
 
Madrasa ungekuwa unasoma kwa Kiswahili , ungeielewa zaidi.

Hapa naona Allah na Malaika wake wanamsalia Mohamed.

Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika Wake humsalia Mtume; enyi mlioamini, msalieni (Mtume) na mwombeeni amani” (Quran 33:56)
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Loh! Ina maana uislam ni dhambi?
Ni kweli kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa na dhambi asili aliyoirithi toka kwa wazazi wake wa mwanzo, Adamu na Eva. Hivyo kusema kuwa kila mwanadamu anazaliwa akiwa muislam, basi inamaanisha uislam ni dhambi. Na hiyo dhambi unaiondoa kwa kubatizwa kuwa mkristo.

Waislam, bila shaka mmeupata ujumbe sawia toka kwa sgekhe aliyeongozwa na roho mtakatifu, kuwa kila mwanadamu anazaluwa akiwa mdhambi/muislam. Na hiyo hali utaiondoa kwa kubatizwa.

atuletee ushahidi wa aya
 
Leta ilimu shekh nasubiri

Pata elimu hii bila malipo:-

Dhambi ya Asili Haipo

Msingi wa Ukristo ni dhambi ya asili ambayo kwayo kusulubiwa kwa Yesu kunahalalishwa na kutumika kwa faida ya Wakristo. Ikiwa dhambi ya asili itatupiliwa mbali, basi kusulubiwa kunakufa maana.

Hakuna hata moja kati ya imani hizi mbili zilizotungwa na binadamu ambazo ni za kweli, na dhambi ya asili haipatikani popote katika Biblia nzima.

Mwanzo 3:14
“Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa kuwa umefanya hivi, umelaaniwa kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote wa kondeni; juu ya tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako.”

Hii ni laana juu ya nyoka, na hata hivyo ni ya kidunia tu.

Ezekieli 18:4
“Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba, ndivyo roho ya mwana ni yangu; roho itendayo dhambi, hiyo itakufa.”

Ezekieli 18:20
“Roho itendayo dhambi, hiyo itakufa.”

Kumbukumbu la Torati 24:16

“Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao; kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.”

Biblia iko wazi kabisa kuwa hakuna mtu atakayewajibika kwa dhambi za wengine. Kila mtu anawajibika kwa nafsi yake mwenyewe, na hawezi kumlaumu Adamu na Hawa.

Dhana hii inalingana kabisa na msimamo wa Qur’ani kuhusu suala hili.

(Qur’an 6:164)
“Hakuna mtu yeyote atakayebeba mzigo wa mwingine, wala mtu yeyote hatavuna dhambi isipokuwa ile aliyojitwika mwenyewe.”

Baadhi ya aya zinazopingana zipo katika Biblia ambazo Wakristo huzitumia kutetea dhana hii ya kutungwa ya dhambi ya asili. Lakini tukiziangalia kwa makini, pia hazizungumzi kuhusu dhambi ya asili kama Wakristo wanavyoamini.

Kwa mfano:

Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umesikia sauti ya mkeo, ukala matunda ya mti niliokuamuru usile, ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa taabu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Mwanzo 3:18
Miiba na mibaruti itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;

Mwanzo 3:19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakaporudi katika ardhi, kwa kuwa ulitwaliwa huko; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Aya hizi zinaweza kuonekana kama zinazungumzia dhambi ya asili, lakini tukizisoma kwa makini, zinaelezea tu adhabu za kidunia na si kitu kingine.

Ni wapi katika Biblia imeandikwa kuwa mwanadamu amepangiwa laana ya milele kwa sababu ya dhambi aliyorithi?

Ni wapi Biblia inasema kuwa kusudi la Yesu lilikuwa kufuta alichokifanya Adamu?

Yohana 1:29

Siku ya pili, Yohana akamwona Yesu akimjia, akasema, “Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”

Manabii hutumwa na Mungu kama vielelezo vya ujumbe wanaouleta. Manabii hutumwa kuwaongoza wanadamu katika njia sahihi na kuwaepusha na maisha ya dhambi. Hivyo basi, Yesu anaondoa dhambi kwa kuwaongoza watu na kuwaonyesha njia ya haki. Zaidi ya hayo, Yesu mwenyewe hakusema maneno haya – ni Yohana aliyesema.

Warumi 5:12
“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi—”

Warumi 5:19
“Kwa sababu ya kosa la mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi...”

Aya hizi zinasema kuwa kwa sababu ya dhambi ya Adamu, mauti ilikuwepo. Lakini haizungumzii mauti ya milele bali kifo cha kidunia. Tafsiri hii ndio inayofaa; vinginevyo, kuna mgongano na aya zifuatazo:

Yeremia 31:29–30
“Siku zile hawatasema tena, Baba wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yamekwashwa. Lakini kila mtu atakufa kwa ajili ya uovu wake mwenyewe; kila mtu anayekula zabibu kali, meno yake mwenyewe yatakwashwa.”

Ezekieli 18:4
“Tazama, roho zote ni mali yangu; roho itendayo dhambi, hiyo itakufa.”

Ezekieli 18:20
“Roho itendayo dhambi, hiyo itakufa.”

Kumbukumbu la Torati 24:16
“Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao; kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.”

Kifo kinachozungumziwa ni kifo cha duniani na si adhabu ya kuzimu.

Methali 20:9
“Ni nani awezaye kusema, ‘Nimekisafisha moyo wangu, mimi ni safi kwa dhambi yangu?’”

Njia ya kujitakasa kutokana na dhambi ni kwa kusafisha moyo, si kwa kuamini kusulubiwa au Utatu.

Zaburi 51:5
“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukua mimba katika dhambi.”

Aya hii inahitaji kusomwa katika muktadha wake ili kueleweka vizuri:

Zaburi 51:1–4

  1. Ee Mungu, unirehemu kwa wema wako; kwa wingi wa huruma zako, uyafute makosa yangu.
  2. Nisafishe kabisa na uovu wangu, unitakase na dhambi yangu.
  3. Kwa maana nakiri makosa yangu; dhambi yangu iko mbele yangu daima.
  4. Nimekutenda dhambi, Ee Mungu, peke yako, nami nimefanya yaliyo mabaya mbele zako...

Zaburi 51:5
“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukua mimba katika dhambi.”

Tukisoma kwa muktadha, tunaona kuwa msemaji wa maneno haya alikuwa mwenye dhambi mwenyewe – angalia aya ya 3 na 5. Hii inaonyesha kuwa anazungumzia dhambi zake binafsi zilizotangulia.

Nathani alitoka kwa mke wa Haruni ambaye alikuwa kizazi cha tano cha mtoto wa haramu wa Yuda. Biblia inasema sheria ya Mungu ilikataza watoto wa haramu kuingia katika kusanyiko la Bwana kwa vizazi kumi (Kumb. 23:2).

Daudi alikuwa kizazi cha tisa cha mtoto wa haramu – mzao wa Peresi, mtoto wa Yuda na Tamari. Nasaba yake ina mawaa: baba yake alitokana na Moabu, uzao wa uzinzi kati ya Lutu na binti yake, hadi kwa Ruthu, Mmoabi aliyebadilika dini.

Daudi alionwa kuwa mtoto wa haramu na baba yake na ndugu zake. Madai haya yametolewa dhidi ya Nabii Daudi.

“Naliumbwa katika uovu” linaweza kumaanisha ama alipokuwa tumboni au katika siku za kukua kwake.

Popote utakapoelekeza maana yake, dhambi inayozungumziwa ni ya kibinafsi, si ya kurithi.

Hata kama “naliumbwa katika uovu” inahusisha siku za kukua, bado hizo ni dhambi binafsi. Mfalme Daudi anatuhumiwa kwa udanganyifu, uzinzi, na uuaji katika Biblia.

Ni ajabu kwamba dhana kubwa namna hii ya Kikristo – "Dhambi ya Asili" – haina ushahidi wowote wa moja kwa moja katika Biblia.

Wabudha, Wahindu, shinto etc ambao hawabatizwi wao walizaliwa wakiwa dini gani? Acheni cheap propaganda
Wote tumezaliwa waislam ni wewe tu kuja duniani na kujifanya mjuaji kumbe hujui lolote kujua Mungu wako
 
Sio mda mkuu

Leta ilimu shekh nasubiri

Ubatizo:
Hii pia ni ibada kuu na ya msingi katika dini ya Kikristo ambayo hata watoto wachanga nao huusishwa nayo pia! Kwa ujumla wake, ibada hii (ya ubatizo) imeshamiri sana katika Ukristo.

Hata hivyo, pamoja na kuwemo katika orodha ya ibada za Kikristo, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Biblia tukufu, asili ya ibada hiyo (ya ubatizo) imetokana na dini ya kipagani (Mithraism). Uthibitisho wa hayo tunaupata katika maelezo ya Biblia yafuatayo:

"Ibada ya (ubatizo) kutosa mwili majini ni mfano wa utakaso au wakujitengeneza upya. Ibada kama hiyo ilijulikana na kutendeka katika dini za kale za kipagani na dini ya Kiyahudi pia...
(kama ubatizo wa waongofu Mdo 2:10; Waesseni)'.

(Tazama Biblia ya Wakatoliki, Imprimatur M. Mihayo Archbishop of Tabora, February, 1967, kwenye maelezo ya Mathayo 3:6 uk. 879).

Maelezo hayo ya Biblia hapo juu yanathibitisha wazi kwamba ibada hiyo ya ubatizo inatokana na dini za kale za kipagani na kamwe haitokani na dini ya Mwenyezi 'Mungu.

Nasema ibada hiyo (ya ubatizo ya kipagani) katu haitokani na M'Mungu, kwa sababu tangu mapema M'Mungu alikwishawakataza na kuwaonya wanadamu kutenda ibada yoyote (kama hiyo ya ubatizo) ya watu wa mataifa (yaani wapagani) kama asemavyo (M'Mungu) katika maandiko yafuatayo:
"Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale".

(Kumbukumbu la Torati 18:19)

Mkristo anaweza kutaka kuutetea ubatizo kuwa ndio ondoleo la dhambi.

Lakini wakrito wote wanakiri kuwa Bw. Yesu hakuwa mwenye dhambi, je iweje asiye na dhambi kama bw. Yesu abatizwe?

Huu kama si uzushi ni kitu gani?
 
Back
Top Bottom