Kila mtu atafute sehemu ya ulaji ale. Kula sio dhambi. Ila kuziba ulaji wa wengine ni dhambi na uhalifu

Kila mtu atafute sehemu ya ulaji ale. Kula sio dhambi. Ila kuziba ulaji wa wengine ni dhambi na uhalifu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Mfumo wa Dunia ni kama umbo la vidole vyako vya mkononi. Umbo la pyramid. Watu hawalingani.

Kuna watakaokula zaidi ya wengine. Kuna watakaokula vizuri zaidi ya wengine.
Ulaji.

Kula kwa urefu wa kamba walisema wahenga. Ni kweli. Nature ipo hivyo. Kila mtu ale kwa urefu wa kamba.

Sisi Watibeli tunautambua mfumo wa Kiganja cha mkono, umbo la pyramid kama mfumo wa Haki. Ikiwa kila mtu atatumia uwezo wake bila kuzuiwa au kufanyiwa hujuma au kuzuiwa.

Hata hivyo, ulimwengu umewekwa katika mfumo wa ushindani, kwamba ili uwe bora sharti upitie vikwazo, viunzi. Kwa namna hiyo katika mapambano ya maisha mtu hapaswi kulialia pale anapokutana na vizuizi, kwani ili uvuke hatua inayofuata lazima upitie daraja, kiunzi.

Vijana lazima mhangaike kutafuta ulaji.
Wenye akili zaidi hutengeneza mfumo wa ulaji. Hawaishii tuu kutafuta ulaji bali kutengeneza mfumo wa ulaji.

Kwa miaka sasa nimeandika makala nyingi sana kuhusu maisha kwa ujumla wake. Nikita codes nyingi ambazo walizozifuatilia wengi wamefanikiwa.

Mfumo lazima ukufanye umiliki watu. Hili nilishaeleza kwenye makala yangu isemayo Miliki watu upate utajiri.

Kisha mahitaji na matamanio ya watu,
Imani za watu,
Na hofu za watu.
Huko ndiko mfumo wako wa ulaji uwe.

Sehemu ziko nyingi za kujitengenezea ulaji;
a) Imani za watu.
Kama Dini, anzisha huduma ya kiroho uwe muislam au mkristo lazima upate hela. Nakuhakikishia lazima. Utakachohitaji ni consistency tuu.

Uganga wa jadi, au motivation speaker kote huko ulaji upo.

b) Matamanio na mahitaji ya watu.
Hapa utahitaji ujuzi, huduma, au bidhaa.
Mtibeli sitakuwa mchoyo. Ukitaka kujua matamanio na mahitaji ya watu Angalia
i) kundi gani linaidadi ya watu. Hapa utakuta vijana na wanawake.
ii) Mahitaji yao ya msingi ni yapi?
Chakula, mavazi, makazi, burudani, na usalama.
Usitoke humo

iii) Hofu yao ni ipi?
Hofu ya kwanza ya binadamu ni Kifo.
Hofu ya pili ni Kesho(future),
Wengi wanajiandaa na kesho.
Biashara za hofu zinapesa ndefu na nyingi zipo kitapeli. Yaani unakula pesa kilaini sana.

iv) Madaraka na uongozi.
Binadamu hawezi kuishi bila kiongozi. Uongozi ni moja ya hitaji la muhimu kwa binadamu.
Uongozi maana yake ni hakikisho na dira.
Sio lazima uwe kiongozi ila unaweza kumiliki mfumo wa kutoa viongozi.
Au kudhibiti viongozi kama vyama vya siasa.

Ni muhimu kuweka hii kichwani.
Huwezi kutimiza maono yako kwenye maono ya mtu mwingine.

Kama huwezi kupambana na uovu au waovu. Basi watumie waovu.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwahiyo mkuu unataka kusema hata hizi VITA za wanasiasa ni VITA za mkate and nothing else?
 
"Kula kwa urefu wa kamba" maana yake kula kile unachopaswa kula.

Kama mfanyakazi wa umma, kula iishie kwenye mshahara wako, sio nje ya hapo.

Unaposema kila mtu atafute sehemu ya ulaji ale, maana yake unawataka hawa wafanyakazi watoke nje ya kula yao ya mshahara wao, wakale nje ya hapo, ni kosa.

Mwisho kabisa, naona watibeli mnakosea kuita mfumo wa pyramid kuwa wa haki, haki ni usawa, sasa inakuwaje kwenu pyramid isiyo sawa iwe ya haki!

Hicho ndio chanzo cha wewe kutaka watu wale wapendavyo ilimradi wasizuie kula ya wengine, ni kosa hilo, kula kwa haki kulingana na unachopaswa kulipw kwa kazi uliyofanya.
 
Kaka mtibeli fursa zipo ni sisi tu hatuitambui, Kuna dogo humu juzi kaja anauza akaunti ya TikTok ina wafuasi sijui 84k nikashangaa unauza watu sijui laki mbili dah tuna safari ndefu sana, mi niliona hapo tu ana fursa kubwa sana sijui alijifikiri vipi
 
Vita ya ulaji.
Vita ya kutengeneza mfumo wa ulaji.

Unapozuia vyama vingine visifanye siasa unaviwekea kauzibe kaulaji. Hapo lazima pacharuke.
Aisee,

Swala hili ni nadra kuongelewa kuwa Hawa jamaa wanaojiita wanaharakati na wanasiasa wanapigania mkate na sio kumkomboa mwananchi wa kawaida ili apate maji na umeme na Afya
 
Kaka mtibeli fursa zipo ni sisi tu hatuitambui, Kuna dogo humu juzi kaja anauza akaunti ya TikTok ina wafuasi sijui 84k nikashangaa unauza watu sijui laki mbili dah tuna safari ndefu sana, mi niliona hapo tu ana fursa kubwa sana sijui alijifikiri vipi

Fursa za ulaji zipo kibao wala haihitaji akili mingi.
Kutengeneza mfumo wa ulaji hapo ndipo inahitaji akili ya ziada
 
Aisee,

Swala hili ni nadra kuongelewa kuwa Hawa jamaa wanaojiita wanaharakati na wanasiasa wanapigania mkate na sio kumkomboa mwananchi wa kawaida ili apate maji na umeme na Afya

Mwananchi wa kawaida kumkomboa ni suala kubwa sana. Linaanzia kwenye mindset, kubadili tamaduni hasa Mila potofu, kuwa Wakweli

Kwa mfano kitendo cha kusema serikali au mtu akiwa kiongozi atakukomboa ndio utapeli wenyewe.
Au umkute mchungaji au sheikh anakuambia Mungu au kuna mhusika fulani mwenye nguvu atakuokoa huo ni utapeli. Hakuna kitu kama hicho
 
Nani anapanga mshahara sasa?

Mimi nalipwa 800k nataka mshahara wangu uwe 1.2M. Huoni kama kamba yangu imefupishwa kama sio kukatwa?
Mshahara unalipwa kulingana na qualifiaction, ukifikia qualification unayostahili kulipwa 1.2m utalipwa.

Wewe unachosisitiza kwenye huu uzi, unamtaka wa 800K ale kwa urefu wa kamba yake ili afikie hiyo 1.2m, sio sawa.
 
Ni qualifications ipi Mbunge wa darasa la saba analipwa zaidi ya 12M na Medical Doctor analipwa sio zaidi ya 2M?
 
Kwanini kusiwe na mshahara Mmoja kwa level Moja ya Elimu ?.. nchi nzima
 
Ni qualifications ipi Mbunge wa darasa la saba analipwa zaidi ya 12M na Medical Doctor analipwa sio zaidi ya 2M?
Hapo umetoka nje ya qualifiacation, upo kwenye nafasi, basi kama nawe unataka kulipwa kama mbunge kuwa mbunge, usilazimishe daktari atengeneze mazingira ili avune kama mbunge, atawaumiza wengine.
 
Mwananchi wa kawaida kumkomboa ni suala kubwa sana. Linaanzia kwenye mindset, kubadili tamaduni hasa Mila potofu, kuwa Wakweli

Kwa mfano kitendo cha kusema serikali au mtu akiwa kiongozi atakukomboa ndio utapeli wenyewe.
Au umkute mchungaji au sheikh anakuambia Mungu au kuna mhusika fulani mwenye nguvu atakuokoa huo ni utapeli. Hakuna kitu kama hicho
Hakika
 
Back
Top Bottom