Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Ndugu Lisu kwanza napenda nianze kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Najua hatujuani, lakini hilo haliwezi kuwa sababu ya mimi kuacha kukushauri pale ninapoona inafaa mimi kufanya hivyo.
Bila kupoteza muda na kuchosha wasomaji ukiwemo wewe mwenyewe. Ningependa kukushauri uombe kuongezewa ulinzi ili wale ambao wanapanga kutumia sekeseke hili la uchaguzi kufanya yao wasiweze kukufikia.
Nasema hivyo kwa sababu wewe ni mtu unaeonekana kuwa na maadui wengi kuanzia ndani ya chama chako, na nje ya chama chako, hivyo ni vyema ukatafuta njia ya kujilinda mapema kabla hayajakukuta yale yaliowakuta kina Chacha Wangwe, Ben saa8, mzee Kibao na wengine wengi waliouwawa katika mazingira ya kutatanisha ambayo mpaka leo watu bado hawajapata majibu ya vifo vyao.
Kwa mtu mwenye akili timamu akiunganisha dot atapata jibu kwamba katika chama chenu kuna mtu ambae amekuwa na tabia ya kuwachacha wagwe wale wote wanaoonekana kupingana nae katika mipango yake au kiti chake. Hivyo na wewe ni bora ukachukua tahadhari mapema ili usije kuhamishiwa kuzimu kwa nguvu, tena katika kipindi hiki ambacho wanachama wengi wa chama chenu wanakuhitaji.
Nakumbuka uliwahi kutengenezewa picha juzikati kwa kuletewa taarifa kwamba kuna watu (nje) ya sultani wenu wanakutafuta na kwamba watu hao wanapanga kufanya jambo, halafu jumba bovu wamuangushie sultani. Na wewe bila kufikiri mara mbili ukaliongelea hilo swala mitandao, na kumtoa kabisa sultan wenu kwenye mission hiyo.
Kwa mtazamo wangu naona kuwa watu waliokupa taarifa ni wa team Sultan ndiomaana walikwambia mapema kwamba yeye hausiki ila wanaopanga kufanya hivyo watamuhusisha.
Sasa hapo inamaana kwamba sultan akishaku chacha wangwe, hata ukipona na kujua kwamba sultan ana mkono wake, wewe utakuwa hauna jinsi ya kumnyooshea mkono moja kwa moja, kwani tayari umeshamsafisha mapema kwamba likitokea jambo hata kama uchunguzi utafanyika na kumkuta sultani anahusika, watu watasema mwenyewe ulisema watamdondoshea jumba bovu yeye, hivyo itachukuliwa kwamba kasingiziwa kama ulivyosema kwenye taarifa yako ya awali.