Kila mwenye ushauri mzuri aje amshauri Lissu. Mimi naanza na ushauri huu

Kila mwenye ushauri mzuri aje amshauri Lissu. Mimi naanza na ushauri huu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu

Ndugu Lisu kwanza napenda nianze kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Najua hatujuani, lakini hilo haliwezi kuwa sababu ya mimi kuacha kukushauri pale ninapoona inafaa mimi kufanya hivyo.

Bila kupoteza muda na kuchosha wasomaji ukiwemo wewe mwenyewe. Ningependa kukushauri uombe kuongezewa ulinzi ili wale ambao wanapanga kutumia sekeseke hili la uchaguzi kufanya yao wasiweze kukufikia.

Nasema hivyo kwa sababu wewe ni mtu unaeonekana kuwa na maadui wengi kuanzia ndani ya chama chako, na nje ya chama chako, hivyo ni vyema ukatafuta njia ya kujilinda mapema kabla hayajakukuta yale yaliowakuta kina Chacha Wangwe, Ben saa8, mzee Kibao na wengine wengi waliouwawa katika mazingira ya kutatanisha ambayo mpaka leo watu bado hawajapata majibu ya vifo vyao.

Kwa mtu mwenye akili timamu akiunganisha dot atapata jibu kwamba katika chama chenu kuna mtu ambae amekuwa na tabia ya kuwachacha wagwe wale wote wanaoonekana kupingana nae katika mipango yake au kiti chake. Hivyo na wewe ni bora ukachukua tahadhari mapema ili usije kuhamishiwa kuzimu kwa nguvu, tena katika kipindi hiki ambacho wanachama wengi wa chama chenu wanakuhitaji.

Nakumbuka uliwahi kutengenezewa picha juzikati kwa kuletewa taarifa kwamba kuna watu (nje) ya sultani wenu wanakutafuta na kwamba watu hao wanapanga kufanya jambo, halafu jumba bovu wamuangushie sultani. Na wewe bila kufikiri mara mbili ukaliongelea hilo swala mitandao, na kumtoa kabisa sultan wenu kwenye mission hiyo.

Kwa mtazamo wangu naona kuwa watu waliokupa taarifa ni wa team Sultan ndiomaana walikwambia mapema kwamba yeye hausiki ila wanaopanga kufanya hivyo watamuhusisha.

Sasa hapo inamaana kwamba sultan akishaku chacha wangwe, hata ukipona na kujua kwamba sultan ana mkono wake, wewe utakuwa hauna jinsi ya kumnyooshea mkono moja kwa moja, kwani tayari umeshamsafisha mapema kwamba likitokea jambo hata kama uchunguzi utafanyika na kumkuta sultani anahusika, watu watasema mwenyewe ulisema watamdondoshea jumba bovu yeye, hivyo itachukuliwa kwamba kasingiziwa kama ulivyosema kwenye taarifa yako ya awali.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu

Ndugu Lisu kwanza napenda nianze kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Najua hatujuani, lakini hilo haliwezi kuwa sababu ya mimi kuacha kukushauri pale ninapoona inafaa mimi kufanya hivyo.

Bila kupoteza muda na kuchosha wasomaji ukiwemo wewe mwenyewe. Ningependa kukushauri uombe kuongezewa ulinzi ili wale ambao wanapanga kutumia sekeseke hili la uchaguzi kufanya yao wasiweze kukufikia.

Nasema hivyo kwa sababu wewe ni mtu unaeonekana kuwa na maadui wengi kuanzia ndani ya chama chako, na nje ya chama chako, hivyo ni vyema ukatafuta njia ya kujilinda mapema kabla hayajakukuta yale yaliowakuta kina Chacha Wangwe, Ben saa8, mzee Kibao na wengine wengi waliouwawa katika mazingira ya kutatanisha ambayo mpaka leo watu bado hawajapata majibu ya vifo vyao.

Kwa mtu mwenye akili timamu akiunganisha dot atapata jibu kwamba katika chama chenu kuna mtu ambae amekuwa na tabia ya kuwachacha wagwe wale wote wanaoonekana kupingana nae katika mipango yake au kiti chake. Hivyo na wewe ni bora ukachukua tahadhari mapema ili usije kuhamishiwa kuzimu kwa nguvu tena katika kipindi hiki ambacho wanachama wengi wa chama chenu wanakuhitaji.

Nakumbuka uliwahi kutengenezewa picha kuzikati kwa kuletewa taarifa kwamba kuna watu (nje) ya sultani wenu anakutafuta na kwamba watu hao wanapanga kufanya jambo halafu jumba bovu wamuangushie sultani. Na wewe bila kufikiri mara mbili ukaliongelea hilo swala mitandao na kumtoa kabisa sultan wenu kwenye mission hiyo.

Kwa mtazamo wangu naona kuwa watu waliokupa taarifa ni wa team Sultan ndiomaana walikwambia mapema kwamba yeye hausiki ila wanaopanga kufanya hivyo watamuhusisha.

Sasa hapo inamaana kwamba sultan akishaku chacha wangwe hata ukipona na kujua kwamba sultan ana mkono wake, wewe utakuwa hauna jinsi ya kumnyooshea mkono moja kwa moja kwani tayari umeshamsafisha mapema kwamba likitokea jambo hata kama uchunguzi utafanyika na kumkuta sultani anahusika, watu watasema mwenyewe ulisema watamdondishea jumba bovu yeye, hivyo itachukuliwa kwamba kasingiziwa kama ulivyosema kwenye taarifa yako ya awali.
Hapa ndio unaona umecheza mindgame la hatari.
 
Zile Risasi 16 bila Kufa, basi hamna Tena mwanadam wa kumuua LISSU.

Kabla hawajapanga kitu, tayari anakijua.

LISSU ni mwanasiasa anayefaidika na DUNIA, Dunia inampa habari zamoto moto hata kabla hazijaepuliwa.
 
Siasa za Afrika zimejaa uongo, unafiki, wizi, rushwa, kutekana, kuuana, hila, chuki na kila aina ya uovu na uchawi.
Ni hatari sana mkuu, ani mtu yupo tayari kumtoa kafara mwenzake kwa sababu ya madaraka.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ushahuri kwa Lisu kwa aina ya uropokaji wake hawezi kukaa na mtu yoyote na hata akishika madaraka hii nchi kila siku itakuwa ni maandamano tu pengine hata ikazuka vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Zile Risasi 16 bila Kufa, basi hamna Tena mwanadam wa kumuua LISSU.

Kabla hawajapanga kitu, tayari anakijua.

LISSU ni mwanasiasa anayefaidika na DUNIA, Dunia inampa habari zamoto moto hata kabla hazijaepuliwa.
Hata 2pac alipokosa kufa kwa shambulio la kwanza akabweteka akijua kuwa atakuja kufa kwa njia nyingine lkn sio shambulio.

Leo hii ana miaka 28 kaburini baada ya kushambuliwa kwa mara ya pili na baadae kufia hospital. So awe makini na uhai wake. Asibweteke
 
Nani alikuambia kuwa lisu anashaurika?
1. Hana hekima ya kupokea na kukubali ushauri.
2. Anajijua kuwa anajua kila kitu.
3. Anajiamini kuwa anajua kuliko watu wote.
Mtu wa aina hiyo hashauriki hata kidogo.
 
Ushahuri kwa Lisu kwa aina ya uropokaji wake hawezi kukaa na mtu yoyote na hata akishika madaraka hii nchi kila siku itakuwa ni maandamano tu pengine hata ikazuka vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Lengo la Lisu ni kurudisha nidham ndan ya chama, kuepuka hela za chama ikiwemo michango ya join the chain kuliwa na kundi fulan, kurudisha ukomo wa madaraka na kufuta uchawa chamani.

Hayo ya maandamano ni watu wenyewe wataamua kuwa wanafuata kauli zake au wanaacha maana hatokuwa anapiga watu risasi kwa sababu et ya kugoma kuandamana.
 
Back
Top Bottom