Naunga mkono Iran kuwa na silaha za nyuklia.
Naunga mkono hata Tanzania kuwa nazo.
Namna pekee ya kuheshimiana hapa duniani ni kila nchi ikiwa na silaha za maangamizi makubwa.
Iran ingekuwa nazo hizo silaha za nyuklia, Israel na Marekani zisingethubutu kuishambulia.
Iran haijatenda kosa lolote lile lakini imeshambuliwa na mataifa mawili yenye silaha za nyuklia.
Huo ni uchokozi na uonevu.
Tena hiyo Israel inazo hizo silaha za nyuklia na hakuna anayenyanyuka na kusema kuwa hiyo nchi haipaswi kuwa nazo.
Halafu ni nani huyo ambaye alizipa ruhusa hizo nchi nyingine zenye hizo silaha kuwa nazo?
Nani aliipa Marekani ruhusa ya kuwa na hizo silaha? Na Marekani inatoa wapi mamlaka ya kuamua huyu au yule hapaswi kuwa nazo silaha za nyuklia?
Unafiki wa kiwango cha daraja la kwanza.
Maana kama kuna nchi hapa duniani ambayo haipaswi kabisa kuwa nazo hizo silaha, basi nchi hiyo ni Marekani ikifuatiwa na Israel.
Marekani ndo nchi pekee ambayo imekuwa ikizivamia nchi zingine na kuzilipua bila sababu zozote za msingi.
Wakati mwingine Marekani hutunga hata uongo wa sababu za kuzivamia nchi zingine.
Walijiingiza kwenye vita huko Vietnam. Watu ambao waliipinga hiyo vita ya Vietnam wakati huo, wengine walifungwa jela na wengine walinyanyaswa na kuitwa ni wasaliti.
Mfano Muhammad Ali na Martin Luther King Jr.
Ali alinyang’anywa hadi mkanda wake wa ubingwa wa ndondi na kufungwa jela kwa kukataa kwenda vitani dhidi ya watu ambao hakuwa na tatizo nao.
Sasa hivi Ali ni shujaa anayeheshimika kutokana na misimamo yake thabiti katika kutetea haki za watu.
Mpaka uwanja wa ndege wa mji alipozaliwa umepewa jina lake!
Going somewhere? Louisville Muhammad Ali International Airport makes it easy to get to your favorite places. Let's go!
www.flylouisville.com
Iran ijitoe kwenye NPT. Na sasa waliunde kikwelikweli hilo bomu la nyuklia na naamini watafanya kweli.
La sivyo wataendelea kunyanyaswa na Israel na Marekani.
Hakuna nchi iliyo na haki pekee ya kuwa na silaha za nyuklia na hakuna nchi isiyo na haki ya kuwa nazo.
Hata Tanzania tuna haki ya kuwa nazo.
Hao walionazo hizo silaha hawakuomba ruhusa yoyote ile kutoka kwa yeyote yule ili kuwa nazo hizo silaha.
I say eff them. Go Iran go.