Kila nchi ina haki ya kuwa na silaha za aina zote

Kila nchi ina haki ya kuwa na silaha za aina zote

Marekani iliyovamia Iraq kwa sababu za uongo na kuishia kuivuruga nchi ya watu, yenyewe siyo nchi ya hovyo?

Marekani iliyowatosa Waafghanistan na kukimbia na kuwafanya Taliban warudi madarakani, yenyewe si nchi ya hovyo?

Marekani iliyodondosha mabomu ya nyuklia kule Japan, yenyewe si nchi ya hovyo?

Marekani ambako kuna ubaguzi wa rangi ukiodumu mamia ya miaka, yenyewe si nchi ya hovyo?

Marekani haina mamlaka yoyote yale ya kimaadili ya kuyanyooshea vidole mataifa mengine.

Una akili duni sana kiasi huwezi hata kujenga hoja ambayo ni ngumu kuipangua 🤣.
Nchi zote zilizopata mabadiliko makubwa zilipitia njia ngumu ya jasho na damu, Marekani walipigana vita vya ukombozi, civil war na civili rights movemnt kuleta mabadiliko makubwa, Ufaransa walimkata kichwa mfalme katika French revolution kuleta mabadiliko makubwa, Uingereza walipamba kupata Magna Carta na kufuatia na civil wars nyingi kuleta mabadiliko makubwa.
 
Naunga mkono Iran kuwa na silaha za nyuklia.

Naunga mkono hata Tanzania kuwa nazo.

Namna pekee ya kuheshimiana hapa duniani ni kila nchi ikiwa na silaha za maangamizi makubwa.

Iran ingekuwa nazo hizo silaha za nyuklia, Israel na Marekani zisingethubutu kuishambulia.

Iran haijatenda kosa lolote lile lakini imeshambuliwa na mataifa mawili yenye silaha za nyuklia.

Huo ni uchokozi na uonevu.

Tena hiyo Israel inazo hizo silaha za nyuklia na hakuna anayenyanyuka na kusema kuwa hiyo nchi haipaswi kuwa nazo.

Halafu ni nani huyo ambaye alizipa ruhusa hizo nchi nyingine zenye hizo silaha kuwa nazo?

Nani aliipa Marekani ruhusa ya kuwa na hizo silaha? Na Marekani inatoa wapi mamlaka ya kuamua huyu au yule hapaswi kuwa nazo silaha za nyuklia?

Unafiki wa kiwango cha daraja la kwanza.

Maana kama kuna nchi hapa duniani ambayo haipaswi kabisa kuwa nazo hizo silaha, basi nchi hiyo ni Marekani ikifuatiwa na Israel.

Marekani ndo nchi pekee ambayo imekuwa ikizivamia nchi zingine na kuzilipua bila sababu zozote za msingi.

Wakati mwingine Marekani hutunga hata uongo wa sababu za kuzivamia nchi zingine.

Walijiingiza kwenye vita huko Vietnam. Watu ambao waliipinga hiyo vita ya Vietnam wakati huo, wengine walifungwa jela na wengine walinyanyaswa na kuitwa ni wasaliti.

Mfano Muhammad Ali na Martin Luther King Jr.

Ali alinyang’anywa hadi mkanda wake wa ubingwa wa ndondi na kufungwa jela kwa kukataa kwenda vitani dhidi ya watu ambao hakuwa na tatizo nao.

Sasa hivi Ali ni shujaa anayeheshimika kutokana na misimamo yake thabiti katika kutetea haki za watu.

Mpaka uwanja wa ndege wa mji alipozaliwa umepewa jina lake!


Iran ijitoe kwenye NPT. Na sasa waliunde kikwelikweli hilo bomu la nyuklia na naamini watafanya kweli.

La sivyo wataendelea kunyanyaswa na Israel na Marekani.

Hakuna nchi iliyo na haki pekee ya kuwa na silaha za nyuklia na hakuna nchi isiyo na haki ya kuwa nazo.

Hata Tanzania tuna haki ya kuwa nazo.

Hao walionazo hizo silaha hawakuomba ruhusa yoyote ile kutoka kwa yeyote yule ili kuwa nazo hizo silaha.

I say eff them. Go Iran go.
Ingekuwa Malawi, Congo inazo sawa tatizo Iran anaongoza kwa ufadhili kwa kuwapa silaha na pesa Wafia DINI kwa lengo la kuharamisha Sheria Haramu na kukuza Uislamu ambayo wengine hatuamini je akiwapa makundi hayo mabomu kama ya nuclear tunaishije hapa Dunian Hilo tatzo
 
Naunga mkono ISRAEL namana sishabikii DINI inayoenezwa kwa upanga mara Mwanamke hatakiwi kusoma mara nini sijui nini sio vyema
 
Waulize wao
Usijali ikitokea Taifa lolote la kiislam linalotengeneza linabidi liangamizwe lakin wakitengeneza WACHINA waachwe namana wao hawana mambo ya kijinga kijinga kufagalia mahadithi ya kimasikin sikin
 
Myahudi alikataa watu wa IAEE kukagua program zake za nyukilia,dunia imejaa unafiki.
Yeye ana kula yake pekee inayomwezesha kujilinda popote alipo mfano inawezekana ukawakuta watalii 50 wa Israel lakin wakiwa na SMG machine ni kitu Cha kawaida Dunian popote
 
Yeye ana kula yake pekee inayomwezesha kujilinda popote alipo mfano inawezekana ukawakuta watalii 50 wa Israel lakin wakiwa na SMG machine ni kitu Cha kawaida Dunian popote
Ndio unafiki wenyewe huo.
Msikilize huyo General wa US ambaye alikuwa ni mkuu wa vikosi vya NATO.

View: https://m.youtube.com/watch?v=Eo6u9DpASp8&pp=ygUpTmF0byBjb21tYW5kZXIgb24gd2FyIHdpdGggc2V2ZW4gY291bnRyeSA%3D
Sasa pata picha mtu anaiongelea hivi nchi yako, wewe utachukua hatua gani kama sio kujilinda? Maaana hata huyo General wakati anapewa maelekezo hakupewa sababu ya kwa nini watazipiga hizo nchi saba. Hizo silaha ya Nuclear ni kisingizio ambacho hakipo kama ,kile kisingizio cha Weapons of Mass Destruction kwa Iraq, ambapo baadae waligundua Iraq hana hizo silaha.IAEE Director wake ambaye aliyeenda kukagua, kasema Iran hawana mpango wa kutengeneza bomu la Nuclear, bali wanatumia Nuclear energy kama source ya kuzalisha umeme.

Plan ya Muyahudi ni kuirudisha nchi ya ahadi, wakishamalizana na hawa. Phase inayo fuatia ni Turkey, Misri na Saudi,kama hujui nusu ya ardhi ya Saudi wanadai ni yao mpaka ile Macca na Madina.
 
Ngabu umetoa boko.

Usifanye masihara na mgonjwa wa akili wa kidini wewe!
 
Ngabu umetoa boko.

Usifanye masihara na mgonjwa wa akili wa kidini wewe!
Sasa kama ni hivyo mkuu si tungekuwa tunaona mashambulizi ya wazi wazi kutoka Iran kwenda Israel kama ilivyo sasa?
 
Kwahiyo Mandela nae alilipua kanisa?
Hujawahi kusikia church street bombing ya 1983 iliyoua watu 20 na kujeruhi wengine zaidi ya 200 kulikofanyawa na Umkhonto we Sizwe (MK)??
 
Hujawahi kusikia church street bombing ya 1983 iliyoua watu 20 na kujeruhi wengine zaidi ya 200 kulikofanyawa na Umkhonto we Sizwe (MK)??
Kwahiyo ndio sababu ya Mandela kuitwa gaidi?
 
Sasa kama ni hivyo mkuu si tungekuwa tunaona mashambulizi ya wazi wazi kutoka Iran kwenda Israel kama ilivyo sasa?
Alikua anajiandaa kufanya hivyo meanwhile akishambulia indirect kwa kufadhili vikundi vya kigaidi Hamas,Hizbolah et al.
 
Nikiona mtu anasimama upande wa haki na ukweli nafarijika.
Hapa umesimama upande wa kweli.
Kwa bahati mbaya watu wengi wanauchukulia huu mgogoro kwa mlengo wa kidini.
Mimi ni mkristo lakini kwa mgogoro huu nasimama upande wa haki wa ukweli wa Iran.
Upande wa haki ndio upo huo?! Ugaidi wa Iran na vibaraka wake dhidi ya Israel ndio upande wa haki.? Nadhani hujui maana ya neno haki
 
Upande wa haki ndio upo huo?! Ugaidi wa Iran na vibaraka wake dhidi ya Israel ndio upande wa haki.? Nadhani hujui maana ya neno haki
Hii mada kubwa sana.
Hapa tutachafua thread ya watu.
Acha tukubaliane unacho sema wewe upo sahihi.
 
Alikua anajiandaa kufanya hivyo meanwhile akishambulia indirect kwa kufadhili vikundi vya kigaidi Hamas,Hizbolah et al.
Miaka yote hii toka atoe hiyo kauli alikuwa bado anajiandaa tu?
 
Back
Top Bottom