Kila nchi ina haki ya kuwa na silaha za aina zote

Mimi nadhani Nyuklia ni kwa ajiri ya ulinzi tu na ndio maana hata North korea anafanya hivyo, hatuoni hata kutishia japo tuliambiwa kiongozi wake ni kichaa hivyo hapaswi kumiliki nyuklia kwa kuhofia ataitumia kwa South korea. Sasa kama Iran ana hasira kiasi hicho kwa Israel na kwamba Iran ni vichaa wa kuweza kutengeneza nyuklia kwa ajiri ya Israel basi tungekuwa tunaona wanaishambulia Israel wenyewe wazi wazi kama wanavyofanya sasa na sio kutumia hivyo vikundi, hapo ndio tungesema moja kwa moja kuwa huyu Iran akipata nyuklia kuna uwezekano mkubwa wa kuitumia kwa Israel.
 
===>> jaribu kupevuka kwanza
 
Iran shobo za kusema eti ataifuta Israel duniani aachane nazo la sivyo kipondo kitaendelea kwa Iran, yeye hajavamiwa na Israel kinachompa kiburi cha kufadhili migaidi ikasumbue Israel ni nini?

Israel kungu'utaaaaa kobaaz mibusha hao
 
Kwa hiyo siyo kosa kwa Iran kufadhili makundi ya magaidi kama Hamas, Hezbollah, Houthi, nk?
Hata Marekani inafadhili kila aina ya uhalifu.

Marekani imewahi kuifadhili Al Qaeda.

Marekani ilifadhili mauaji ya Patrice Lumumba.

Marekani imefadhili na kuunga mkono madikteta lukuki.

Marekani inaifadhili Israel ambayo inafanya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Je, Marekani ni sawa ikifadhili yote hayo?
 
Sio kila mtoto Kisa anataka simu, inampa Je Ina madhara Gani kwake...

Ubaya Wa Iran limekuwa Taifa la hovyo Sio Kwa middle East pekee yake hata Kwa Dunia mzima
Kila Rais wake anapochaguliwa target number moja nikija wamarekani au Israel (death to Israel) waneenda mbali sana Hadi wakatoa matamko kuwa Taifa la Israel lifutwe kwenye ulimwengu Wa Dunia

Pia, iRan ndio Taifa ambalo Ni mfadhili mkuu Wa magaidi wengi walio Middle East ...mfano , Hezbollah,ISIS, HAMAS,Al quida etc ili kuleta sintofahamu ndani YA middle East Na Dunia kWa ujumla Na Jao magaidi target Yao Ni USA Na Israel (raia wao)

Hata kama Ni wewe ungemwacha Iran aendelee kutamba (kama anafadhili magaidi ...ipo siku atawapa silaha ZA maangamizi kama Nuclear hapo ndio maana Zaidi yataonekana
(Kuna misemo unasema prevention is better than cure) Tibu cancer kabla haijasambaa miwili mzima

Note.. Magaidi hawana serikali useme wanapata mode, just imagine Hela zao zinatoka wapi..Iran apigwe n asiruhusiwe kuwa Na vinu vya Nuclear Ni hatari Kwa usalama Wa dunia
 
na tukitoka hapo tunakwenda mbali zaidi kwamba kila raia ana haki ya kumiliki silaha yoyote muhimu awe na hela ya kununulia tu.
 
Naunga mkono hoja zako
 
Kwanini Iran inatumia hivyo vikundi kuishambulia Israel badala wao wenyewe kushambulia moja kwa moja Israel kama wanavyofanya sasa hivi?
 
Si kweli
 
Nikiona mtu anasimama upande wa haki na ukweli nafarijika.
Hapa umesimama upande wa kweli.
Kwa bahati mbaya watu wengi wanauchukulia huu mgogoro kwa mlengo wa kidini.
Mimi ni mkristo lakini kwa mgogoro huu nasimama upande wa haki wa ukweli wa Iran.
 
Myahudi alikataa watu wa IAEE kukagua program zake za nyukilia,dunia imejaa unafiki.
 
Huyo anayetishwa kufutwa,yy kaifuta Palestina hamna maisha,huduma za kijamii ukiwasikiliza madaktari na wafanyakazi wa UN kila anaye simulia hali ya Wapalestina huishia kutoa machozi? dunia imejaa unafiki, mminyaji wa haki akifanyiwa vilevile anaamini anaonewa.

Hiki kitu kilitabiriwa zaidi ya miaka 20, US pamoja na Netanyahu wanasema kabisa ndani ya miaka mitano tutazipiga nchi saba Lebanon, Syria, Sudan, Yemen, Iraq, Libya na watamalizia na Iran, wewe unazani Iran angereact vipi? Huyo Myahudi anaprogram ya Nuclear na amekataa IAEE kukagua program,sasa jiulize kwa nini amekataa. Huu unafiki sijui utaisha lini.

Mpaka sasa hivi Myahudi anampango ya kuirudisha nchi yake ya ahadi, so tegemea vita na Saudi, Turkey, Misri hii ndio next phase, hawa nao watatafutiwa sababu kama ilivyo kwa hao wengine sabab, kama hujui Myahudi anaamini Macca na Madina ni ardhi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…