Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Hugs luv 🫂 🤗

Ila watanzania kuna namna inabidi tupunguze kufuatilia maisha binafsi ya wengine na kuuliza maswali yasiyotuhusu!
Acheni upimbi. Mwanamke over 30 upo upo tu unataka jamii isikushangae. Yaani mchumba huna, mme huna, mtoto huna.

Kama kuna shida za kiafya ita-make sense.

Otherwise endeleeni kujifariji na u-feminist huku mkitumika.
 

From Now On Mamii,,Wakikuuliza Tena Waambie Unaye HOLY SKANKA,,Nitawakilisha Na Kukaimu Nafasi Hiyo Ya Mchumba Katika Dipatimenti Ya Moyo Wako,,Mpaka Pale Utakopojaaliwa Kupata Mbadala..
Ukiamua Kunipandisha Cheo Pia, Siwezi Danganya Nitafarijika..
###KamaHutojali###
​
 
Kusema kweli hawa Wakubwa wetu huwa wanakosea sana.

Kuna Baba mdogo ndio lilikuwa swali lake hilo kila akinipigia simu. 😃

Kuna siku nikamwambia MZEE HILI SUALA NINGEOMBA USIRUDIE TENA KUNIULIZA.
Wale wengi ni wa kuwasamehe tu.

Kwa sababu wengi wanaona wanafanya vile kwa upendo.

Ila tatizo hawajui kuwa dunia imebadilika sana kutoka ile ya enzi zao kuilinganisha na hii.

Wengi wanatoka vijijini, kuoa hakukuhitaji kujipanga sana.

Hata waliokuwa mjini, walivyooa wao maisha yalikuwa si ya kujipanga sana kama sasa. Kazi zilikuwa zinapatikana, dunia haikuwa ya kasi ya leo, hata hao wanawake wa kuoa ilikiwa unaweza kupangiwa tu na familia.

Sasa dunia ya leo imebadilika sana, kuna watu wanahoji hata suala zima la kuoa, kifalsafa kabisa, wao bado wako stuck kwenye dunia yao.
 
Kipindi cha nyuma nilipohitimu chuo nikawa nasaka ajira kuna mama alinikalia kooni kila akiniona swala kuolewa halimkauki mdomoni kisa tu ni family friend. Swali ambalo hata familia yangu haikuwa ikiniandama nalo na hata sikuwa over 30. One day nikamtolea uvivu nikamjibu "nasubiri ufe mumeo anioe". Ilikuwa varangati ila hakuwahi kuniuliza hilo swali teeena. Siku ya harusi yangu nikamuuliza umeridhika sasa?

Sijui kwanini binadamu tunapenda kufuatiliana sana.
 
Hili tangazo limekaa kitaalam sana
Mtu anaelezea hisia zake unasema tangazo 🤣🤣🤣 Ufalme wa mbinguni utausikia kwenye redio tu Mkuu

Hili jambo ni mtambuka Mkuu, linatesa sana Wasichana wengi, kuna binti fulani ni graduate wa UDSM tena degree ya Uchumi kaolewa na dogo darasa la saba tu, Mlinzi na bodaboda na yote hayo ni kwa sababu ya mashinikizo.

Binti baada ya kuolewa kapata kazi nzuri tu kwenye taasisi ya serikali na dogo alipata hela kwenye ishu zake kajenganyumba na kapanua biashara kwa kununua na bajaj mbili , Binti hayupo comfortable kabisa na yule dogo maana dogo hata Kiingereza cha kuombea maji hakipo
 
Mfano hauwezi ukasikia familia ya Lady Jay dee au diamond zinalalamika watoto wao kuoa au kuolewa .


Maana yake ukiwa Masikini Kila MTU anahisi ana mamlaka ya kukupangia namna ya wewe kuishi
Nadhani umeelewa vibaya
Na pia umewahi kuingia kwenye familia za hapa watajwa hapo ukasikia wakiwa wanaongea sebuleni labda?
Au unadhani Maisha Yao mitandaoni ndio Kila kitu chao?
 
Acheni upimbi. Mwanamke over 30 upo upo tu unataka jamii isikushangae. Yaani mchumba huna, mme huna, mtoto huna.

Kama kuna shida za kiafya ita-make sense.

Otherwise endeleeni kujifariji na u-feminist huku mkitumika.
Sasa unataka kuwapangia maisha?

Kama mtu kaona ndoa itampotezea muda wa ku focus kutafuta dawa ya cancer, amejitoa maisha yake kutafuta dawa ya cancer, utataka kumpangia asifuate hiyo passion yake, aolewe, kwa sababu wewe ndiyo unavyotaka?

Wewe unayependa watu waoe na kuolewa, mtu akija na kukupiga marufuku usiweze kuoa, utaona sawa?
 
Huwezi kusikia familia za watu kama Lady Jaydee au Diamond Platnumz zikilalamika hadharani kuhusu watoto wao kuoa au kuolewa kwa sababu tu jamii inahisi ina mamlaka ya kuingilia maamuzi yao.

Ukweli ni kwamba, unapokuwa na uwezo wa kifedha, watu wengi wanaheshimu maamuzi yako hata kama hawakubaliani nayo.

Lakini unapokuwa maskini, kila mtu anahisi ana haki ya kukushauri, kukuhukumu na hata kukupangia namna unavyopaswa kuishi.

Umasikini haupunguzi tu uwezo wako wa kifedha; mara nyingi unapunguza pia uhuru ambao jamii inakupa wa kufanya maamuzi yako mwenyewe.

Ndiyo maana kujenga uwezo wa kifedha si kutafuta pesa pekee, bali pia ni kujenga uwezo wa kuamua maisha yako bila kutegemea idhini ya kila mtu.
 
Sijui ni mie ama Niko sensitive sana?
Nnapokutana nao katika maongezi nikipigwa Hilo swali najikuta na-blush huku ndani naumia,mchangayiko na aibu na huzuni.Natoa majibu ya hapana bado.wakiendelea najikuta nashindwa hata kujieleza napata kigugumizi.
Shida sio kupata mchumba,shida ni njia zimetofautiana,njia anayopitia mwingine haiwezi kuwa sawa na anayopitia mwingine.Jambo linaweza kuwa rahisi Kwa mwingine lakini upande wa mwingine likawa tofauti.Jamii yetu imeadapt kama ndio njia sahihi impasayo kupitia Kila mtu Kwa wakati fulani,pale utaposhindwa kuipita kwa wakati inageuka maumivu.
Binti uko over 30 huna hata mchumba,huna mtoto wanabaki eeh🙄
Na je ikiwa mtu ataamua Kwa maamuzi yake kubaki hivyo ni kosa?

Kwa upande wa wengine mapungufu yanachangia,ndio tuna mapungufu ya hapa na pale kama changamoto za kiafya,kimwili zinazopelekea kukosa mwenza.Dhahama na magumu utayokuwa unayapitia mwenyewe na Ile hisia unaipata mwenyewe lakini wengine hawawezi kuuhisi huo mzigo unaoupitia,utasikia "jikubali mbona wapo wengi tu wanaingia kwenye ndoa,Wana familia? Wanakushangaa
Shida ni hawajui ni rejection ngapi unapitia,hawahisi mzigo wa maumivu unaobeba.
Hakuna anaependa kukosa kitu,Kila mtu anatamani kukipata on time,lakini kuweka kama utamaduni mtu kuwa na kitu Fulani katika wakati fulani mi naona ni kuumiza hisia na moyo wa mtu Ambae kwake ni ngumu kupatanaa.

Yangu ni hayo Kwa Leo🥹
Wanaume ndiyo sisi tatizo tukiwafata mnakataa

Karibu kila week wanaume wanapost uzi

Wanatafuta wake .


Wanawake wengine hawajakaa pia kizembe akimpenda mwanaume ana mtongoza.


Changamka uondokane na hiyo aibu.
 
Huwezi kuvunga kitu ambacho kina kuumiza mpaka kufikia kuanzisha uzi,kusema "Siku inaisha" ni kama kujifariji tu ila tatizo lipo palepale,

Kumbuka haya ni maisha yako,maisha ni mafupi sana,weka mipaka kwenye maisha yako ili usiingilike kirahisi.
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Mfano hauwezi ukasikia familia ya Lady Jay dee au diamond zinalalamika watoto wao kuoa au kuolewa .


Maana yake ukiwa Masikini Kila MTU anahisi ana mamlaka ya kukupangia namna ya wewe kuishi
point.

ila hata kama sio tajiri kiivyo mtu akijileta na kudhani kuwa ana umuhimu kwenye maisha yangu kwa sababu tu sina hela siju sababu sijasoma ama kwa sababu sijui sina gari na yeye ana gari ama kwa sababu anajua kingreza na mimi sijui hata kiswahili yaani tyu ili mradi anadhani anacheo kwenye maisha yangu kiasi cha kutaka riport ya mipango yangu nitampa jibu ambalo lita reset namna anavyonitazama maisha yake yote. na ataenda kuwasimulia na wajinga wenzie mbele ya safari nao natajireset. halafu tunaheshimiana.
 
Sasa unataka kuwapangia maisha?

Kama mtu kaona ndoa itampotezea muda wa ku focus kutafuta dawa ya cancer, amejitoa maisha yake kutafuta dawa ya cancer, utataka kumpangia asifuate hiyo passion yake, aolewe, kwa sababu wewe ndiyo unavyotaka?

Wewe unayependa watu waoe na kuolewa, mtu akija na kukupiga marufuku usiweze kuoa, utaona sawa?
Kaka usitete angalia demu wa ARUSHA kadanganya anauza duka kumbe anauza nyapu kafia gesti hio aibu kijijini kwao wataipeleka wapi?
 
Back
Top Bottom