Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Sijui ni mie ama Niko sensitive sana?
Nnapokutana nao katika maongezi nikipigwa Hilo swali najikuta na-blush huku ndani naumia,mchangayiko na aibu na huzuni.Natoa majibu ya hapana bado.wakiendelea najikuta nashindwa hata kujieleza napata kigugumizi.
Shida sio kupata mchumba,shida ni njia zimetofautiana,njia anayopitia mwingine haiwezi kuwa sawa na anayopitia mwingine.Jambo linaweza kuwa rahisi Kwa mwingine lakini upande wa mwingine likawa tofauti.Jamii yetu imeadapt kama ndio njia sahihi impasayo kupitia Kila mtu Kwa wakati fulani,pale utaposhindwa kuipita kwa wakati inageuka maumivu.
Binti uko over 30 huna hata mchumba,huna mtoto wanabaki eeh🙄
Na je ikiwa mtu ataamua Kwa maamuzi yake kubaki hivyo ni kosa?

Kwa upande wa wengine mapungufu yanachangia,ndio tuna mapungufu ya hapa na pale kama changamoto za kiafya,kimwili zinazopelekea kukosa mwenza.Dhahama na magumu utayokuwa unayapitia mwenyewe na Ile hisia unaipata mwenyewe lakini wengine hawawezi kuuhisi huo mzigo unaoupitia,utasikia "jikubali mbona wapo wengi tu wanaingia kwenye ndoa,Wana familia? Wanakushangaa
Shida ni hawajui ni rejection ngapi unapitia,hawahisi mzigo wa maumivu unaobeba.
Hakuna anaependa kukosa kitu,Kila mtu anatamani kukipata on time,lakini kuweka kama utamaduni mtu kuwa na kitu Fulani katika wakati fulani mi naona ni kuumiza hisia na moyo wa mtu Ambae kwake ni ngumu kupata.

Yangu ni hayo Kwa Leo🥹
Hizo ni pressure za jamii kwa mwana jamii.
Likn usisahau kuwa haya maisha ni yako hautaishi kwa niaba ya wengine
 
Kaka unaijua kondoa? Kwao na marehemu, mkuu kondoa ni watu wa Imani ya kiislamu sana kule dini ipo tena kwa ukubwa, alafu kaka swala la kufa Kila nafasi itaonja mauti fikiria wazazi wake watabaki na Hali Gani, dini yetu ya kiislamu itatuamuru tuombe mwishowema sababu kifo hakizuiwi ila unakufaje hapo ndio tuna shauriwa kuomba mwisho mwema mana siku ya mwisho Kila mtu atafufuliwa alivyo kufa, we unaongelea kwa mtazamo wako mi naongelea uhalisia ulivo sababu na yajua mazongira ya kule mkuu acha tu usirahisishe watu wanajiua kwa kusemwa tu we unachukulia poa, unadhani fujo za oktoba 29 watu kutaka kuwadhuru watoto wa viongozi unadhani chanzo ni nini si maneno tu waliyosemwa watu wakaamini unapuuziaje maneno mkuu, athari zake si ndio hizo kuleta vifo.
Kwanza inasikitisha sana badala ya kusikitika mtu kapoteza maisha umeona jambo kubwa kabisa la kusikitisha hapa ni aibu ya kijijini kwao.

Yani unaishi kwa kujali zaidi watu watakionaje kijiji kuliko kujali mtu kapoteza maisha.

Yani kati ya mtu kupoteza maisha na kijiji kupata aibu umeona kijiji kupata aibu ndiyo tatizo kubwa.

Na hapo hapo hujaona kuwa hoja nzima ya kijiji kupata aibu ni ya kijinga kabisa. Ni hoja ya kijinga kabisa, kwa sababu kama kuna aibu inatakiwa kuwapo hapa, ni kwa mtu aliyefanya kosa, si kijiji chake.

Unakipaje kijiji kizima kosa la mtu mmoja?

Zaidi, umeshindwa kufikiri kimfumo. Hawa watu wana matatizo ya kimfumo ya kukosa elimu, kukosa fursa za kazi, kukosa uongozi bora, kukisa utamaduni bora, kuwa na umasikini wa kurithishana vizazi hata vizazi. Umeshindwa kuangalia mambo ya msingi ya kimfumo yaliyopelekea jambo hili, umefocus kwa mtu mmoja tu kama yeye ana nguvu kushinda mifumo.
 
Hizo ni pressure za jamii kwa mwana jamii.
Line usisahau kuwa haya maisha ni yako hautaishia kwa niaba ya wengine
Ndio ukweli
Mtu anakwambia si angalau uzae umri unaenda,lakini mwisho wa siku malezi ni juu yako na Maisha ni yako hata ukibaki single parent.
Watu wafanye mambo Kwa mipango na utayari na sio presha toka Kwa jamii
 
Ndio ukweli
Mtu anakwambia si angalau uzae umri unaenda,lakini mwisho wa siku malezi ni juu yako na Maisha ni yako hata ukibaki single parent.
Watu wafanye mambo Kwa mipango na utayari na sio presha toka Kwa jamii
" Si uzae umri unaenda" utafikiri huo umri ndo utalipa ada ya mtoto shule au bills za hospital kama mtoto akiumwa.
 
Bwashee umeongea jambo la msingi sana,
Watu watakuuliza haya maswali au kuingilia maisha yoko,kutokana na jinsi ulivyojiweka wewe mwenyewe,

Ukiweka mipaka hakuna kizee kitakacho kusogelea.
Mkuu ukigundua kijana wako ameamuwa kuwa shoga utaheshimu maamuzi yake?
Au ukigundua kuwa binti yako ni muuza k maarufu huko mjini utaheshimu maamuzi yake?
 
Ni ngumu kupunguza watu ndivyo walivyo , kuna watu hata hauwajui kabisa ila wana hadithi zako iwe ni za kweli au za uongo
Zipo jamii nyingine hazina mambo ya kufuatiliana. Kwa hiyo sio kwamba watu ndio wapo hivyo, bali Watanzania ndio wapo hivyo kwa kiasi kikubwa. Bongo kufuatilia maisha ya watu kupo very normalized. Labda uhame nchi
 
Back
Top Bottom