Kila ninapoweka juhudi za kupungua uzito, ndio naongezeka!

Yeah am week physically nalijua hilo sijakualia kwenye kazi ngumu japo kwenye gym nilikua na jitahidi sana kunyanyua vyuma....sasa hayo mazoezi ya Cadio ni yapi mkuu? Fafanua plz.
ruka kamba, kimbia ogelea ukipenda
 
Polee sana kiongozi :
Kuna huu ukweli ambao wengi huona kama uongo na kukomalia yanayoandikwa na influencers. Ukweli ni hivi, mazoezi yanamchango kidogo mnoo kwenye kupungua uzito. Tafiti nyingi zimeonyesha mtu ambaye huwa na Nidhamu kwenye chakula hupungua uzito kwa kilo nyingi sana ikilinganishwa na anayefanya mazoezi.
Mazoezi yanasaidia sana katika kuuweka mwili imara na kuzuia kuwepo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama presha ya kupanda.
Ukitaka kupungua uzito kuwa na nidhamu n chakula. Kama unataka kujua namna gani.. Quote hii reply na uulize How.
How?
 
Iko hivi ndugu mleta maada. Wazungu wanasema Unlearn to Learn. Kuna njia nyingi sana ambazo watu huzishauri zitumike katika kupunguza uzito na njia hizi zinapishana katika ufanisi wa kuleta matokeo tarajiwa. Ili uweze kupungua uzito ni lazima matumizi ya Calories katika mwili wako yawe makubwa zaidi ya kiasi unachoingiza mwilini mwako (Energy consumed
1. Kufunga kula: Njia hii ya kufunga kula kwa masaa 12 hadi 24 imekuwa na uwezo mkubwa sana (40%) wa kuleta matokeo. Katika njia hii Matumizi ya Nishati mwilini huwa ni makubwa zaidi ya kiasi cha Nishati iliyoingizwa mwili hivyo kupelekea mwili kupungua uzito kupitia kuunguza mafuta ya ziada yanayotunzwa katika sehemu mbali mbali za mwili kama vile Chini ya Ngozi na ndani ya viungo. Ukianza kufunga hakikisha pia chakula unachotumia kuvunja funga yako (breakfast) kiwe kisiwebkila chakula chenye Nishati nyingi sana (High caloric value) kama vile ugali mkubwa, sahani iliyojaa wali na mihogo n.k. Kumbuka mtu akiwa katika haki ya kushiba chakula kinchotumika sana ni kile alichotoka kula kilichotunzwa hakivunjwi vunjwi hata kidogo na kama mtu amefunga chakula huvunjwa katika mtiririko huu

Wanga > Mafuta > Protini. Kwahiyo kama haujala mwili hauna wanga, mafuta hutumika kuzalisha nishati na kama mafuta yameisha Protini hutumika (Autolysis). Swali linaweza kuwa ni kufunga kwa namna ganj kwafaa kati ya ile kufunga mfululizo(continuous fasting) au kufunga kwa kurusha siku (intermittent fasting), mimj nakuambia Tumia intermittent fasting. Has been proven effective enough to make your body loose weight.

2. Kupunguza kula wanga(Cutting off carbs) : Wanga umeonekana kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuta mwilini. Hivyo sasa, ili kuzuia mafuta yaliyotunzwa mwilini kuongezeka tunapunguza ulaji wa wanga na kuhamia kula vyakula kama Nyama (Protein) na Mboga za majani. Kufanya hivi hupelekea mwili kuanza kutumia mafuta ya yaliyotunzwa kabla kuzigeukia protini. Hivyo hii nayo inasaidia kupungua uzito. Na kiasi cha wanga unapaswa kula kama unataka kupungua uzito kiwango cha ngumi yako.

3. Kufunga kula huku ukinywa maji tu. Hii njia inaweza kukupa matokeo within 7days unaisha kabisa bila hata kuhangaika sana. Swali je, utaweza kujizuia kula kwa hizo siku zote huku ukiwa unakunywa maji tu? Inawezekana sana ila fanya kwa kuruka siku moja moja (intermittent fasting).

4. Achana na hizi tabia : Acha kunywa pombe usiku na uende kulala, acha kula sana usiku na uende kulala muda huo huo, punguza matumizi ya sukari au vyakula au vinywaji vyenye sukari nyingi, Acha tabia kula usiku muda umeenda sana jizoeze kula chakula chako cha usiku saa moja jioni kama ilivyokuwa boarding schools.

Kama umeisoma hii na unataka niendelee, Quote tena na andika More
More
 
Najaribisha ushauri yako number 3 ntakupa matokeo baada ya siku 7 yaani wiki injao j5. Ningumu ila ebu nijitahidi mimi ni mwanaume hi tabia ya kuongezeka hivi siipendi vitoto vyangu bado vinanihitaji nikiwa na afya njema.....anyway athantee sanaa mkuu[emoji120][emoji120]
 
Kwa siku 45 nilikua silii mchana, nakula tu asubuhi chai ya ragi na skonzi moja na yai moja, mchana napiga ndefu, usiku ndio nakula wanga kidogo na chai ndio nalala. Kila siku kabla ya kuoga nafanya pushup 30 na kuruka ruka kidogo kwa lengo la kupunguza kilo, nitoke Kg 94 nirudi Kg 89 za awali kabla ya holiday.

Jana ndio nilienda kupima nione ni mepungua ngapi, to my surprise nimeingia Kg 103! Natimiza hivyo unene ni mwili wa mtu na ni majaliwa na kadari za Mungu. Mke wangu anakula mara mbili yangu milo mitatu hadi minne kwa siku ila anachezea 49kg hadi 55kg ni model kweli kweli ukimuona. Mimi naona nitajiachia tu litakalokuwa na liwe bwana.
Funhga kama wanavyofanya wavaa kobaz,
 
Samahani sana Mkuu Wangu
Mi najuaga wewe ni Demu samahani sana Mkuu Wangu.
 
PIGA DEMU INAYOUZA MWILI KAVU ALAFU PANGA KWENDA KUCHEKI AFYA BAADA YA MIEZI MITATU... NDANI YA MWEZI MMOJA WA MWANZO UTAFANIKIWA KUPNGUZA KG 10 KWA MAWAZO YA JE, KAMA UKIKUTWA NA NGOMA? MATOKEO NI CHAP NA HUNA HAJA YA MAZOEZI ILA ANGALIZO NI KWAMBA "KAMA UKIUKWAA KWELI UTAJUA MWENYEWE" FANYA KAMA UNA-BET TU
😂😂😂😂😂
Bora kubet pesa ya mkopo mechi ya mwenzi ujao
 
kupunguza unene inawezekana hasa has ukifuata , utaratibu ufuatayo

-Kupunguza , vyakula vya wanga, ugari wa sembe,wali, n.k, kupunguza uraji wa nyama hasa hasa nyama choma, na kuku hawa wa kisasa

-Asubuhi inatakia ulee chapati moja, na chai au kuacha kabisa

-Mchan kula matunda, inaweza kua ndizi 2 au parachichi moja

-Usiku unaweza kula ugari kidogo au wali kidogo

utaamua , mchana ule matunda au usiku ndo ule matunda

-UKIFANYA MAZOEZI, LAZIMA UTAKULA SAANA NA UTANENEPA , MAZOEZI HAYAPUNGUZI UZITO MBALI YANAONGEZA

nimefanya hao kwa mda wa miezi 5 nimepungua kutoka 70 to 56,
Mimi hapa siyo mlaji sana ila nimetoka 65kg march 2021 sasa nipo 81kg. Nilikuwa nimeishafikia 86kg mwaka jana nikakata cabs kabisa. Nikawa natumia nyama na samaki, mboga za majani na maharagwe, daar na njegere. Ndo sasa nipo 81.

Shida niliyoambiwa na dr ni kwamba nile sana kidogo kidogo ila nisitumie sukari maana ndo sumu.
Nimeshindwa kuacha sukari. Wewe uliyeongezeka sababu ya mazoezi. Mimi kizee kungwi ninayepanda ngazi kumi nikakaa kwanza inakuwaje.
Washauri wa vyakula njoni huku mtusaidie. Mwenzangu hajasema umri mimi ni 64 she.
 
Push up nipige ngapi ili ziwe na matokeo chanya kama 30 ni ndogo ila jua mwili unachoka nikifanya mazoezi kwa mda mrefu nakuanza kutetemeka.
Unashindwa kutofaurisha mazoezi ya kugain muscles na kupunguza uzito,hayo ni mambo tofauti.

Push up haziondoi uzito bali zitakuomgezea muscles za upper body.

Kimbia,kunywa maji,badili muda wa chakula,usitarget kupoteza kilo nyingi kwa muda mfupi kwani hizo kilo haukuzipata kwa muda mfupi,it takes time.
 
Nikawa natumia nyama na samaki, mboga za majani na maharagwe, daar na njegere. Ndo sasa nipo 81.
Nani kasema samaki hanenepeshi ?
Nani kasema njegere hazinenepeshi ?

Kiufupi falsafa yangu ni kwamba hakuna chakula kibaya wala kizuri inategemea na mlaji mwenyewe.

Kula mara kwa mara ni moja ya propaganda za huu ulimwengu,miili yetu imaweza kuishi kwa kula mlo mmoja ama milo miwili tu kwa siku(milo mepesi)huku muda uliobakia ukinywa maji tu.
 
.
Kuwa na uzito uliopitiliza ni kukosa nidhamu ya kula. No excuses.
.
Wengi wanaotaka kupungua hawapati matokeo kwa sababu hawana nidhamu ya kutulia na diet plan moja kwa muda mrefu. Leo anafanya diet A, kesho karukia diet B, kabla hajaona matokeo kesharukia diet plan nyingine.
.
Choose one diet plan then STICK to it untill you see results...thank me later.
 
Piga intermittent fasting, itafute kwenye Google, mimi hupiga 18/6
Pia epuka chakuka cha usiku.
 
Back
Top Bottom