Iko hivi ndugu mleta maada. Wazungu wanasema Unlearn to Learn. Kuna njia nyingi sana ambazo watu huzishauri zitumike katika kupunguza uzito na njia hizi zinapishana katika ufanisi wa kuleta matokeo tarajiwa. Ili uweze kupungua uzito ni lazima matumizi ya Calories katika mwili wako yawe makubwa zaidi ya kiasi unachoingiza mwilini mwako (Energy consumed
1. Kufunga kula: Njia hii ya kufunga kula kwa masaa 12 hadi 24 imekuwa na uwezo mkubwa sana (40%) wa kuleta matokeo. Katika njia hii Matumizi ya Nishati mwilini huwa ni makubwa zaidi ya kiasi cha Nishati iliyoingizwa mwili hivyo kupelekea mwili kupungua uzito kupitia kuunguza mafuta ya ziada yanayotunzwa katika sehemu mbali mbali za mwili kama vile Chini ya Ngozi na ndani ya viungo. Ukianza kufunga hakikisha pia chakula unachotumia kuvunja funga yako (breakfast) kiwe kisiwebkila chakula chenye Nishati nyingi sana (High caloric value) kama vile ugali mkubwa, sahani iliyojaa wali na mihogo n.k. Kumbuka mtu akiwa katika haki ya kushiba chakula kinchotumika sana ni kile alichotoka kula kilichotunzwa hakivunjwi vunjwi hata kidogo na kama mtu amefunga chakula huvunjwa katika mtiririko huu
Wanga > Mafuta > Protini. Kwahiyo kama haujala mwili hauna wanga, mafuta hutumika kuzalisha nishati na kama mafuta yameisha Protini hutumika (Autolysis). Swali linaweza kuwa ni kufunga kwa namna ganj kwafaa kati ya ile kufunga mfululizo(continuous fasting) au kufunga kwa kurusha siku (intermittent fasting), mimj nakuambia Tumia intermittent fasting. Has been proven effective enough to make your body loose weight.
2. Kupunguza kula wanga(Cutting off carbs) : Wanga umeonekana kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuta mwilini. Hivyo sasa, ili kuzuia mafuta yaliyotunzwa mwilini kuongezeka tunapunguza ulaji wa wanga na kuhamia kula vyakula kama Nyama (Protein) na Mboga za majani. Kufanya hivi hupelekea mwili kuanza kutumia mafuta ya yaliyotunzwa kabla kuzigeukia protini. Hivyo hii nayo inasaidia kupungua uzito. Na kiasi cha wanga unapaswa kula kama unataka kupungua uzito kiwango cha ngumi yako.
3. Kufunga kula huku ukinywa maji tu. Hii njia inaweza kukupa matokeo within 7days unaisha kabisa bila hata kuhangaika sana. Swali je, utaweza kujizuia kula kwa hizo siku zote huku ukiwa unakunywa maji tu? Inawezekana sana ila fanya kwa kuruka siku moja moja (intermittent fasting).
4. Achana na hizi tabia : Acha kunywa pombe usiku na uende kulala, acha kula sana usiku na uende kulala muda huo huo, punguza matumizi ya sukari au vyakula au vinywaji vyenye sukari nyingi, Acha tabia kula usiku muda umeenda sana jizoeze kula chakula chako cha usiku saa moja jioni kama ilivyokuwa boarding schools.
Kama umeisoma hii na unataka niendelee, Quote tena na andika More