Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

1.Nyerere alituachia:-
a.Umoja na Mshikamano
b.Uhuru wa kweli
c.Lugha ya Kiswahili
d.Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
e.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977

2.Mwinyi alituachia
a.Uhuru wa kweli
b.Mfumo wa Vyama vingi vya siasa
c.Deni kubwa la Taifa
d.Ndiyo wakati Watanzania wengi walijenga sana
e.Mitumba na Biashara ya Minada

3.Mkapa alituachia:-
a.Barabara safi zinazounganisha mikoa yote
b.Taasisi mbalimbali imara kama vile TRA,TCRA,TAKUKURU,TASAF nk.
c.Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Dodoma
d.Uwanja mkubwa wa mpira Afrika Mashariki na Kati
e.Alifuta kodi ya Kichwa na kodi mbali mbali za Halmashauri zisizoeleweka.

4.Kikwete alituachia:-
a.Barabara safi zinazounganisha mikoa yote ya Tanzania
b.Vyuo vikuu mbalimbali Tanzania
c.Gharama za maisha zikiwa katika hali nzuri Tanzania kuliko wakati wowote ule.
d.Nidhamu mbovu za Watumishi na viongozi mbalimbali Serikali
e.Bunge lenye nguvu na mvuto

5.Magufuri alituachia:-
a.Ndege
b.Madaraja makubwa kama vile Kigamboni na Busisi
c.Ujenzi wa SGR
d.Ukabila na ukanda
e.Watu wasiojulikana

6.Mama Samiah ametuletea:-
a.Umoja na mshikamano uliopotea awamu ya tano
b.Uzanzibar na Utanganyika
c.DP World
d.Udini
e.Utegemezi
 
Asante sana mtu wa Mungu uko sahihi kabisa.
 
Wewe ni mbumbumbu na mpumbavu.
 
Nani huyo aliyefanya hayo yote?
 
Bila shaka Nyerere alikuacha mjane bila kukurithisha chochote na watoto wako wakaishi kwa shida.
 
Afrika kuna:
1.NKWAME NKRUMAH
2.JULIUS NYERERE
na si vinginevyo.
 
Pamoja na kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo nchini,
Magufuli aliacha alama kwa kujenga misikiti kwa waislamu tulioshindwa kujijengea miskiti yetu wenyewe na kusubiri hisani.
 
Nimeanza kushuhudia awamu kuanzia kwa Jakaya Kikwete, Hizo za Nyerere na Mwinyi sina cha kusema,

Ila Kikwete kwangu ni bora [emoji123]

Kwa Magufuli nadhani ukiwa kama mtumishi ilikuwa ni machungu tu, labda sekta ya ulinzi

Kwa mama Samia sina cha kusema
 
Bibie, " the agony of a dark continent" kwa tafsiri yangu mimi inahusu ukoloni mamboleo wa uongozi wetu wenyewe, weusi na madhila yake yafuatayo katika:
1. Kufeli kwenye utumishi walopewa awamu zote kupunguza makali ya ujinga, umaskini na maradhi ..
aha, kwa njia za KUJITEGEMEA!
2. UFISADI
3. ANASA na GHARAMA zisizofaa kuongoza nchi msikini - midege, migari ya kitajiri kama vitendea kazi, ubadhirifu wa mali za umna n.k
4. Kutokua na SERA zisizo za kitapeli
...... et cetera! bila kusahau
i. Siasa CHAFU
j. UONGOZI usio bora

Tutake pia maendeleo ya watu!
 
Nyerere alituachia Umoja miongoni mwetu ambao upo mpaka leo ila tumeanza kuuwekea upupu !!

Pia alituachia Viwanda visivyopungua 400, nivitaje vichache vilivyokuwa maarufu zaidi
1- Mwatex kiwanda cha nguo za aina tofauti kama vile vitenge khanga nk.
2 - Mutex kiwanda cha nguo pia
3 - Urafiki
4 general Tyre kiwanda cha Matairi
5- Canvas kiwanda cha magunia
6- minjingu Stamico kiwanda cha mbolea
7- Tancut kiwanda cha kukata Almasi
Machine tools Moshi
8- viwanda kibao vya kukamua mafuta huko kanda ya Ziwa
9 - kiwanda cha kutengeneza Sigara
10- Tanganyika Packers viwanda vya kusindika nyama
11 - viwanda vya vileo bia nk,
Bata kiwanda cha viatu
12- huko jeshini vilikuwepo viwanda vikitengeneza baadhi ya silaha
13 - viwanda vya Sukari na sukari guru pia
14 - kiwanda cha Ngozi ,
15- viwanda vya Kahawa
And so on and so on
Wengine wataongezea !!
 
National millings mikoa yote !
 
MJERUMANI
1. Reli ya Kati
2. Ikulu ya Dar Es Salaam
3. Bandari

MWINGEREZA
1. Lugha ya Malkia
2. Mfumo wa Mahakama
3. Mfumo wa Utawala

NYERERE
1. Ujamaa
2. Kiswahili
3. Utanzania

MWINYI
1. Vyama vingi
2. Sekta binafsi
3. "Ruksa"

MKAPA
1.Utandawazi
2. Wawekezaji
3. Hotuba za kila mwezi
4. Mfumo imara wa utawala

KIKWETE
1. Uhuru wa kuongea
2. Barabara nyingi za lami
3. Mchakato wa Katiba mpya
4. Uvumulivu kwa wapinzani
5. Ongezeko la Vyuo Vikuu

MAGUFULI
1. Nidhamu kwenye ofisi za Umma
2. Ndege
3. Jiji la Dodoma
4. Bwawa la Nyerere
5. Daraja la Busisi

SAMIA
Sina uhakika kwa sababu bado hajahitimisha safari yake, lakini huenda akatuachia
1. Katiba ya wananchi
2. Demokrasia ya kupigiwa mfano barani Afrika
3. Tanganyika na Zanzibar zinazoheshimiana
4. Daraja la Dar - Zanzibar
5. Uhuru wa kutoa maoni.
 
Uchambuzi mzuri huu.
 
Mmii Mswahili anakuwaje na Mjomba Muarabu?
I
Hili ni moja ya Ajabu la Dunia.

Sijawahi kusikia Mwarabu anamwita Mjomba mtu mweusi.

Yaani Mwarabu anaonekana kama Mungu kwa hawa watu.
Mimi mweusi tii,lakini babu yangu mmojawapo ni mwarabu pure,nenda tabora na shinyanga ukajifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…