nimeandika mahala kulitenga hili, au umeona uweke tu!Heche ni kiongozi wa chama cha umma, suala la uadilifu wake sio kati yake binafsi na wale anaowaongoza, unless Chadema wawe hawana mpango wa kushika dola, something which i don't think so.
Kwa hao niliowajumuisha wanaanzia kwenye chama na hadi nje ya chama; sasa wewe unataka nionekane kama nimeweka mipaka?
Kwa wakati wowote, kama atataka kuwa kiongozi katika ngazi yoyote ile, ni lazima akubali na mwanga umwakie katika maswala yake yote.
Na hili halimhusu Heche pekee. Ni ajabu kwamba msisitizo unamhusu yeye wakati tukiona mapapa wanaohitaji kuhojiwa hata hawasemwi.
Na zaidi ya hivyo: hivi ni kitu gani kilichompa Katuga motisha ya kumhusisha Heche katika maswala binafsi na kuyaleta mahakamani wakati siyo mshtakiwa; maswala yale yale yaliyotumiwa na hao akina Lema, umejiuliza hilo?
Kwa hiyo tukubali kwamba Lema na Katuga wanaelewana sana na wanafanya kazi pamoja ya kutaka kumwonyesha kuwa Heche hafai kuwa kiongozi ndani ya CHADEMMA?
haya yote ni upuuzi, unajuwa nilicholenga kueleza.▪ Unapoandika Chadema waachiwe chama chao umenishangaza, kwa member wa aina yako na experience yako humu ndani!.
• Ina maana bado hujui chama cha siasa ni mali ya umma?!
hayo maswala yameanza kuingizwa ndani ya chama toka nje kwa mlango wa akina Lema; ambao kama wangekuwa na lengo zuri kwa chama chao yangeishia huko huko ndani ya chama; lakini wakaona yaenezwe nje ya chama kwa malengo yanayojulikana. Sasa hapa unataka kujifanya huelewi kitu gani.
EEEEEnHEEEEeee!Nashangaa sana chama chenye miaka zaidi ya 30 wafuasi wake kutetemeka pale viongozi wao wanapotakiwa kuwajibika, ajabu kabisa, lazima mbadilike ili kuijenga Tanzania bora mbele ya safari.
Hao "viongozi wanapotakiwa kuwajibika", nani huyo anayetaka viongozi wawajibike, akina Katuga na hawa akina 'Adam francis' matapeli wasiokuwa na uchungu wowote na taifa hili, ili mradi wanajaza matumbo yao?
Mkuu 'denoo' nilijuwa una 'interest' juu ya jambo hili mara ya kwanza kabisa nilipokusoma na tukajibishana.
Heche anatakiwa kuwajibika/kuwajibishwa kama anayo makandokando yake; sipo hapa kumtetea; lakini kwa namna haya yanayoendelea humu kumbini, ni dhahiri kuna la ziada mbali kabisa na shutuma zinazoelekezwa kwake kwa kutumia watu kama Lema; ambaye sasa sina hakika kama doa alilojivisha kuwa upande hasimu wa chama chake ataachana nalo kiurahisi.