Kilicho mpata Heche kimethibitisha mahakama siyo mama yako!

Maana ya Heche kudanganya kuhusu mali, ni kuwa yeye Heche ni muongo na ushahidi wake hauwezi kuaminika kwakuwa anasema uongo hata akiwa chini ya kiapo.
Hili ndilo lilikuwa dhumuni la Katuga kumuuliza hayo maswali.

..Ni kweli Heche alidanganya kuhusu magari yake.

..Je, mambo mengine aliyosema ni ya uongo?

..Kwa mfano, Heche alizungumzia watu kutekwa na kuuwawa jimboni kwake wakati wa uchaguzi.

..Je, madai ya Heche kuhusu watu kutekwa na kuuwawa yanakuwa ni uongo kwasababu amesema uongo kuhusu magari yake?

..Majaji watachambua ushahidi wa uongo, na ushahidi wa kweli. Ndio maana wake pale.
 
In fact,
amedogoshwa mno na Katuga,

In fact,
huenda ana pitia msongo mkali sana wa mawazo hivi sasa, hasa akitafakari alichopitia kizimbani.

hii wiki yote anaweza asibeti kabisa 🐒
Kwamba hayo ndio maswali ya kumtia mtu hatiani kwa kosa la uhaini?.
Nilitegemea ushahidi mzito wa majeshi na zana za kivita alizopanga kutumia Lissu kutekeleza nia yake ya uhaini.
Sasa wanapiga blaablaa tu.
Mungu atawalipa.
Amina.
 
Gentleman,
swali lililomtia hatimae mtuhumiwa wa uhaini ni moja tu,
tena liliulizwa na wakili msomi Ajuaye.

mengine yalikua ni katika kukamilisha ratiba tu kwa mujibu wa sheria za nchi 🐒
 
Hakuna tafsiri yangu hapo, hayo ni maneno ya makamu mwenyekiti wako alipokuwa akijibu maswali ya Katuga kwenye cross examination.
"Adam Francis"?
Utakuwa siyo mzima akilini mwako. Huyo "makamu mwenyekiti" ulininunulia wapi?
Na hayo unayoandika hapa aliyasema "akijibu maswali ya Katuga"; ndio uthibitisho usiokuwa na shaka kuhusu ugonjwa wako wa akili.
 
Sikuelewa kwa nini Lissu na Katuga kila mara walikuwa wanakumbushana kuwa mahakama siyo mama yako mpaka siku Heche alipoanza kufanyiwa cross examination.

Heche huyu huyu aliyetoa ushahidi ulioonekana kuwa na taarifa nyingi za kila uonezi aliodai CHADEMA wanafanyiwa kaishia kudogodeshwa na Katuga mbele ya mahakama kwa kujithibisha yeye mwenyewe kuwa anadanganya kuhusu mali zake na huwa anaingiziwa mapesa kwenye account yake ambayo wenzake wa CHADEMA hawajui!

Kiukweli kwa hiki kilichompata Heche, niko pale nasubiri kuona kama CDF, IGP na DCI wataenda mahakamani. Waswahili husema mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Screenshot_20260803-153325~2.png
 
In fact,
amedogoshwa mno na Katuga,

In fact,
huenda ana pitia msongo mkali sana wa mawazo hivi sasa, hasa akitafakari alichopitia kizimbani.

hii wiki yote anaweza asibeti kabisa 🐒
Screenshot_20260826-114453~2.png
 
Sikuelewa kwa nini Lissu na Katuga kila mara walikuwa wanakumbushana kuwa mahakama siyo mama yako mpaka siku Heche alipoanza kufanyiwa cross examination.

Heche huyu huyu aliyetoa ushahidi ulioonekana kuwa na taarifa nyingi za kila uonezi aliodai CHADEMA wanafanyiwa kaishia kudogodeshwa na Katuga mbele ya mahakama kwa kujithibisha yeye mwenyewe kuwa anadanganya kuhusu mali zake na huwa anaingiziwa mapesa kwenye account yake ambayo wenzake wa CHADEMA hawajui!

Kiukweli kwa hiki kilichompata Heche, niko pale nasubiri kuona kama CDF, IGP na DCI wataenda mahakamani. Waswahili husema mwenzako akinyolewa zako tia maji.

Idadi ya magari ya Heche yanahusika vipi na uhaini!! yaani hamjui hata game. Heche sio mshitakiwa hapa kama ana mali kinyume na sheria kwanini wasimfungulie kesi. Je Heche anadaiwa na TRA?

Yaani ungeonekama wa maana kama ungesema kuhusu Lissu mshitakiwa sasa Heche kimebadilika nini?
 
Hiyo ni tafsiri uliyoitaka wewe, na sasa unataka na wengine tuchukue tafsiri yako ya kipuuzi?

kama wewe unanufaika na hiyo tafsiri, fahamu pia kwamba wengine hawakuona hivyo unavyofikiri wewe.
Jenga hoja wewe acha kulopolopo kila mada
 
Sikuelewa kwa nini Lissu na Katuga kila mara walikuwa wanakumbushana kuwa mahakama siyo mama yako mpaka siku Heche alipoanza kufanyiwa cross examination.

Heche huyu huyu aliyetoa ushahidi ulioonekana kuwa na taarifa nyingi za kila uonezi aliodai CHADEMA wanafanyiwa kaishia kudogodeshwa na Katuga mbele ya mahakama kwa kujithibisha yeye mwenyewe kuwa anadanganya kuhusu mali zake na huwa anaingiziwa mapesa kwenye account yake ambayo wenzake wa CHADEMA hawajui!

Kiukweli kwa hiki kilichompata Heche, niko pale nasubiri kuona kama CDF, IGP na DCI wataenda mahakamani. Waswahili husema mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Kwanza mimi namshangaa katuga hata kama mimi si lawyers.unawezaje kudukua personal info zangu ambazo si hoja ya uhaini ukapeleka mahakamani kama exhibit.kama hii ndo aina ya wanasheria tulio nao basi ni halali kupambania katiba mpya la sivyo huo uchafu utaendelea kubaki serikalini
 
Kile kinachotokea pale hakiwezi kupelekwa kufungua mashtaka mahakama yoyote, dawa ya kuishinda cross examination hakikisha shahidi wako hana doa kama ilivyokuwa kwa Mnyika, Golugwa na Brenda.
Sasa wewe "doa" umeliona wapi kwa Heche?
Katuga akishatuhumu hata bila ya uthibitisho wowote wa kuaminika tayari hilo wewe unalihesabu kuwa ni "doa"?

Ni muhimu piauelewe kuwa hao akina Katuga walimpania zaidi Heche, kwa sababu ushahidi wake ulikuwa 'extensive' na wa msingi zaidi katika utetezi wa mshtakiwa.
Na hiyo ndiyo sababu aliwekwa kwa mkakati kuwa shahidi wa mwisho wa uhakika wa utetezi.
 
Nijengee hoja gani kwenye mada ya kipumbavu kama hii?

Ni hoja gani ulizoweka wewe katika hayo maneno hapo juu!
Nyie wote vilaza mna piga tu makelele hata hamjui kitu kuhusu ushahidi wa mahakama kuu
Kama wewe ns vilaza wenzako bado hamuelewi hoja ya mleta mada basi nyinyi ni mbulula
 
Sasa wewe "doa" umeliona wapi kwa Heche?
Katuga akishatuhumu hata bila ya uthibitisho wowote wa kuaminika tayari hilo wewe unalihesabu kuwa ni "doa"?

Ni muhimu piauelewe kuwa hao akina Katuga walimpania zaidi Heche, kwa sababu ushahidi wake ulikuwa 'extensive' na wa msingi zaidi katika utetezi wa mshtakiwa.
Na hiyo ndiyo sababu aliwekwa kwa mkakati kuwa shahidi wa mwisho wa uhakika wa utetezi.
Doa nililiona upande wa maelezo yake binafsi.

Kwa mtazamo wangu na kile kilichotokea pale kizimbani, Heche alipwaya zaidi kwa upande wa mashahidi wa Lissu.

Naona unazungumzia ushahidi wa Heche kuwa "extensive" zaidi ya ushahidi wa kina Mnyika na wenzie, sijui umetumia kigezo gani zaidi.

Kama kigezo chako ndio hicho cha Heche kuwekwa mwisho, basi mimi nimeona heri Heche angewekwa mwanzo ili wengine waje kufukia yale mashimo yake.
 
Nyie wote vilaza mna piga tu makelele hata hamjui kitu kuhusu ushahidi wa mahakama kuu
Kama wewe ns vilaza wenzako bado hamuelewi hoja ya mleta mada basi nyinyi ni mbulula
Unajulikana ni nini kinachokuleta humu JF. Huna mchango wowote wa maana kwa taifa hili tokea uingie humu JF; lakini bado unataka nipoteze muda wangu na mtu kama wewe ambaye ajenda yake inajulikana kuwa siyo ya manufaa kwa taifa hili!

Ninakufahamisha tu kwamba hakuna namna ya kujitoa akili itakayowasaidia waovu nyie. Hatma yenu na huyo mhalifu Samia ipo wazi.
 
Doa nililiona upande wa maelezo yake binafsi.

Kwa mtazamo wangu na kile kilichotokea pale kizimbani, Heche alipwaya zaidi kwa upande wa mashahidi wa Lissu.

Naona unazungumzia ushahidi wa Heche kuwa "extensive" zaidi ya ushahidi wa kina Mnyika na wenzie, sijui umetumia kigezo gani zaidi.

Kama kigezo chako ndio hicho cha Heche kuwekwa mwisho, basi mimi nimeona heri Heche angewekwa mwanzo ili wengine waje kufukia yale mashimo yake.
Taarifa za Heche binafsi zilizowasilishwa na Katuga, kama ndizo zinazokufanya uone unavyoona wewe, mimi hizo hazimo kwenye sehemu ya utetezi wa kesi yenyewe.

Aliyozungumzia Heche ni yale yale aliyosema Mnyika katika ushahidi halisi, ila Heche kaingia ndani zaidi na kutoa hadi mifano ya jinsi chaguzi zilivyovurugwa; na hata yeye mwenyewe kuathiriwa.
Ungetaka ushahidi uwe wa namna gani zaidi ya huo.
 
Masuala ya kesi ni sawa, lakini kwa nafasi yake ya kiongozi wa chama na yale mambo ya pesa kwenye akaunti yake asijue zolipotoka - hapana.
 
Back
Top Bottom