Kilichofanywa na Iran ni trela tu, ila watazamaji (Israel) wakataka movie nzima wataletewa

Huu ujinga mnaolishana mkiwa tel aviv ya vingunguti ndo tunaoukataa. Tuliwahi kudanganywa kuwa Israel ina intelejensia kali kuliko nchi yoyote duniani, lakini kilichofanyika October 7 kimeiacha uchi na aibu kubwa kuwa haina intelejensia yoyote kama tulivyoaminishwa na waisrael wa bonyokwa.

Imagine kundi la watu linaingia katika ardhi yake na kufanya operation ya kuuwa raia na wanajeshi kadhaa, kisha kuteka na kuondoka na kundi la watu zaidi ya elf 2 bila kukamatwa, kuzuiwa wala kujulikana kuwa wamefanya tukio. Sasa hiyo intelejensia tuliodanganywa ilikuwa iko wapi? Maana watu kuvuka boda kuuwa na kuteka maelf ya watu sio kazi ndogo. Hata Rwanda ambayo ni nchi ndogo isiyokuwa na intelejensia kama ile tuliyoambiwa anayo muisrael, ni vigumu kundi la waasi linaweza kutoka Congo na kuingia katika nchi ile likafanya mauaji na kutoka na kundi la watu kama ilivyofanywa Israel na Hamas vijana wasiokuwa na silaha za maana wala mafunzo yoyote rasmi ya kijeshi.

Pia tulidanganywa kuwa Israel ilikuwa na makomando walioenda kuwaokoa mateka wao huko Intebe Uganda, lakini imekuja kudhihirika kuwa zote hizo zilikuwa ni propaganda uchwara. Maana kama kweli wana makomando wa kweli, basi wangekuwa wameshawaokoa mateka wao kitambo hapo Gaza.

Haiingii akilini makomando waweze kuja kuwaokoa mateka wao hapa Uganda KM zaidi ya elf 6 kutoka Israel alaf washindwe kuwakomboa wale waliopo Gaza ambapo ni KM 200 tu kuwafikia.

Hata hizo silaha unazosema ni porojo tu. Kama kweli ingekuwa na silaha unazosema basi isingelilia msaada wa silaha kutoka Marekani, UK na Ujerumani ili kupambana na kakikundi kadogo tu ka vijana wasiozidi elf 20 tena hawana ndege wala kifaru.

Bob Marley: "you can fool some people some times, but you can't fool all the people all the times"
 
nabana pumbu vita kamili isitokee nahurumia kima wenzangu huko kuzimu ya dunia afirika mtakula nini?

ila jamani tuweke kando ushabiki Israel bila US hawezi vita yoyote. mambo ya 6 days sijui nami zamani nilikua namuona Israel bonge la mbabe ila kumbe ni janja tu zamani hakukua na internet ikawa rahisi kutudanganya. waarabu na wayahudi wote wadwanzi tu.
 
Anaweza asijibu sasa hivi ila siku akijibu lazima apeleke kilio kikubwa Tehran.
Netanyahu huwa hana show ndogo.
Time will tell
Ataishia kuvamia makundi ya vijana anaodai ni washirika wa Iran huko Lebanon au Syria, lakini kui face Iran moja kwa moja hawezi na Biden ashamwambia hivyo Netanyahu kuwa asithubutu. Maana kama yeye Netanyahu ni kichaa, basi Ayatullah ni mwendawazimu kabisa. Kauli yake haijawahi kurudi nyuma, hata Netanyahu na Biden wanalijua hilo. Akisema tutapiga wanapiga kweli.
 
Umeandika ukweli mkuu.
 
Za ndani kabisa, Iran hawakulenga target muhimu ila walitoa salamu tu Kwa Israel kama anaweza ajibu...
 
ushahidi wa nini unaohitaji, unavojua wewe technolojia ya kijeshi ya iran anaipata wapi? kama hujui sema nikupe darasa
Israel inayofikiri ina teknolojia bado inaomba msaada wa kijeshi na silaha toka kwa bwana zake wazungu. Iran inasimama yenyewe bila msada wa yoyote na bado inapambana na mataifa zaidi ya matano peke yake.
 
makombora 99% yametunguliwa syria na jordan hayakufika israel, israel walijua makombora yametumwa kwao na walikua wanaendelea na shughuli zao kama kawaida si dharau hizi?
Kwa kawaida jeshi lolote huwa halitoi taarifa kamili ya madhara waliyopata. Jumlisha vyombo vyote vilivyokupa habari ni vya magharibi. I mean vya kwao na mabwana zao.

So usitegemee kupata taarifa za kweli za kilichotokea usiku. Ila maumivu aliyonayo Netanyahu sasa hivi sio ya kawaida.
 
pia iran kila kitu kijeshi anategemea urusi yeye kama yeye bila urusi hakuna anachoweza, silaha zake zote ni modified version ya silaha za urusi, so kama israel anasaidiwa na marekani, iran anasaidiwa na urusi sasa shida hapo iko wapi?
Hivi haukusikia kuwa hata Urusi ilipewa silaha na Iran zikatumika kushambulia Ukraine mpaka raisi wa Ukraine pamoja na nchi za magharibi zikalalamika kuwa Iran inaipa silaha Russia ambazo zinafanya maangamizi makubwa huko Ukraine?

Hizi ni habari ambazo zilitangazwa na vyombo vya habari vya hao hao mabeberu wa magharibi. So kama mrusi anampa silaha mui iran basi na mui ran anampa silaha mrusi.

Alaf pia usiwe mvivu wa kusoma historia ya dunia. Iran ilianza kuwa mbabe na mpaka kuwa na himaya (persia empire) miaka zaidi ya 3000 iliyopita kabla ya utawala wa roma wala Yesu Kristo kuzaliwa. Hivyo Iran ni taifa ambalo linauwezo toka miaka hiyo kabla hata Urusi haijulikani kama itazaliwa.
 

Attachments

  • Screenshot_20240414-215818.jpg
    326.7 KB · Views: 1
kuhusu suala la israel ni wazungu au sio hiyo ni mada ingine nitakupa hilo darasa siku ingine, darasa la leo ni kuhusu makombora
Kwa haya uliyoandika hapa, tayari ishaonesha kuwa wewe ni mweupe unaandika kwa kufuata mkumbo wa wapambe wa Israel, lakini huna lolote unalojua kuhusu Israel, Iran wala kile kinachoendelea mashariki ya kati.
 
Ila Israel ina dharau aiseee. Yaani Iran wamerusha makombora makalio usiku, wakayadungua kisha leo wakaendelea na ligi yao ya soka kama kawaida!

Hiyo ni ishara kwamba kilichofanywa na Iran hakijasababisha madhara yoyote, na kesho Hapoel Beer Sheva atacheza dhidi ya Maccabi Tel Aviv kana kwamba hakuna kilichotokea. Hii ni dharau inayokera zaidi. πŸ˜†πŸ€£
 
Oh kumbe nguvu za Israel zinategemea mataifa mengine ya Marekani na Uingereza? Mimi nilizani taifa la Mungu litasimama lenyewe kujipigania kama wanavyosimama wanaume Iran.

Sasa wewe ukipigana na kundi la watu zaidi ya watatu alaf ukapigwa au ukawapiga kwa pamoja ni nani kati yako wewe uliepigana peke yako na wale waliokuchangia ataonekana ana nguvu. Kiuhalisia utaonekana wewe ndo una nguvu kwa sababu umekubali kuingia mapambanoni na watu zaidi ya watatu bila uoga wala hofu yoyote ya kuomba poo.

Hivyo Iran kupambana na hizo nchi zote ulizotaja peke yake ni ushindi mkubwa kwa Iran labda kama vita hii ingekuwa ni ya Israel peke yake na Iran bila USA na UK kuingilia ndo tungesema kweli Israel iko vizuri.
 
Hawa jamaa huwa hawakubali kushindwa. Yani ukiwagusa, wao wanakusukuma kabisa.. hahahaha
Watamfanyia hivo kibonde wao Palestine sio Iran. Unaijua Iran wewe? Hem kasome tena history. Tafuta Persian Empire.

Hao waisraeli wana historia ya kuvamia hapo palestina kwa fujo kisha wanatawala baadae wanatolewa tena yani ni hivo historia inajirudia kwahiyo hawana jipya watachomoka tu hapo.
 
Umempa historia nzuri sana ambayo wengi wao hawaijui. Hio ni waajemi sio waarab, wayahudi wala wahindi.

Wakiamua kukiwasha wanakiwasha na hakuna wa kuwazuia kufanya wanachotaka kufanya. Wawaulize Marekani kule Iraq walifanywaje na hao jamaa.
 
Israel inayofikiri ina teknolojia bado inaomba msaada wa kijeshi na silaha toka kwa bwana zake wazungu. Iran inasimama yenyewe bila msada wa yoyote na bado inapambana na mataifa zaidi ya matano peke yake.
una uhakika iran inasimama yenyewe? iran silaha zake zote ni za urusi unalijua hilo? ebu nitajie silaha ambazo iran imezigundua yenyewe
 
sio iran tuu..hata egypt hata zipo dola za africa zilizotawala before christ so usilete zilipendwa hapa.

pia kuhusu iran kusuply drone kwa rusia ni kitu cha kawaida mana drone zao ni cheap kuliko drone za urusi, tech ya drone sasa ivi ishasambaa dunia nzima kila mtu anawez kutengeneza
nenda kawachomoe sasa tukuone

hao persin kama ni wakali mbona hawana chochote saa hii? unaleta mambo ya historia hata sisi si tulikua na chief mkwawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…