Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Palizi eka elfu 10? naona ndogo Sana.
Wenyeji naomba majibu ya maswali yafuatayo, 1.Vibarua wapo?
2.ukitokea Dar unapanda magari ya wapi ili ufike Kiteto?
3.Vijijini gani vina ardhi ya kutosha kwa ajili ya kukodi mashamba?
Vibarua wapo wagogo wapiga iyo kazi sana na wako vizuri

Ukitokea dar unapanda magari ya Kiteto yapo ya kampuni ya kamwana dar to kiteto.

Kuhusu mashamba yako mengi mno niwew tu kuja kujionea na kuchangua unapopenda kulima.
 
Salam!!

Mrejesho wa kutafuta shamba nzuri.

Baada ya ziara ya wiki kadhaa ya kutafuta shamba hapa wilayani kiteto

Hatimae nimepata shamba nzuri kama nilivyotegema nimepata mashamba mawili moja maeneo ya kijungu na jingine maeneo ya lantomomi yote ni mashamba mazuri yapo maeneo mazuri na yenye rutba kedekede japo ilo la kijungu lipo mbali kutokea hapa nilipoweka makazi yangu kiteto mjini lakin sio mbaya kuna boda yangu dar nitaifwata nitakua nikiitumia kuelekea uko maana kutokea hapa town hadi kijungu ni kipande cha 73km.

Mambo ndio yamekaa hivyo wakuu mkisikia ameibuka billionaire kijana mdogo msije kusema nimtakatishaji fedha za umma!

Nukuu ya Baba wa Taifa.
Mnatafuta mali, "mali mtazipata shambani."
 
Ukwel halis mashamba ya rutuba yana umbali sana, kuna eneo linaitwa Irkuishibor (japo kuna hifadhi baadhi ya sehemu) lina rutuba balaaa(84km from kiteto centre)wanlima simsim(Ufuta), mahindi na mazao mengine!!
 
safi kijana mdomdogo mpaka kuwa billionaire
 
Ukiona mwaka kiteto wamevuna mahindi kwa wingi jua gunia itakuwa elf25 nawewe utauza kwa bei iyo,huwezi pata elf60 kwa miezi mitatu labda baada ya miezi 7 kuelekea mwaka unaofuata,sisi ndo ma-settler wa kiteto tuulize,kwanza kwenye mchanganuo wako sijaona gharama ya kupukuchua,makuli,usafiri,stoo.nk. vip unalima kiteto maeneo gani tufahamiane
 
usisahau kupelekwa sehemu pana itwa Njutah na ngaboro nayo ni shida ardhi ni steki tupu
 
Kwa mikoa ya Iringa, Mbeya,Ruvuma, Njombe, Singida, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na Shinyanga ni mwanzo msimu wa kilimo.

Ni vema mkulima wa mahindi akazingatia yafuatayo ili kupata ufanisi:

1.Muda huu ni vema uwe tayari umeandaa au unaandaa shamba.

2. Andaa samadi ya ng'ombe iliyoiva vizuri na isambaze shambani kabla ya kulima hasa maeneo ambao msimu uliopita mazao hayakustawi vizuri. Samadi/ mboji ndio siri kubwa ya ustawi mzuri wa mazao hasa mahindi. Mbolea za viwandani pekee si suluhisho la mavuno mazuri.

Maeneo mengi nchini yana upunguvu mkubwa wa virutubisho vya Nitrogen hivyo ni lazima mkulima arutubishe shamba lake ili kupata tija. Ukiweka samadi mfululizo kwa misimu 3 unaweza usiweke tena mbolea kwa miaka 5 hadi 7 ijayo.

3.Andaa mbegu bora mapema. Kwa mbegu chotara au Hybrids tumia mbegu km DK8053,DK90789,DK777,H614, H625Seedco nk. Waone wataalamu wa kilimo au maduka ya kilimo wakupe ushauri upande mbegu ipi kwa eneo lako, japo Dk. 9089,H625 zinastawi maeneo mengi.

4.Panda mbegu kwa nafasi mfano Sm75xSm30 ambapo ekari moja utapata miche 44,000.

5. Andaa pesa au nguvu kazi ya kutosha kupalilia shamba. Wakulima wengi hukosea hapa. Wengi huchelewa kupalilia shamba. Shamba la mahindi lipaliliwe wiki 3 hadi ya 4 toka kupanda. Ukichelewa mahindi hushindwa kukua vizuri na huenda yakadumaa.

6. Andaa mbolea ya kukuzia hasa kama Urea na CAN ili muda wiki 6 na isizidi wiki 8 uwekee mbolea. Wakulima wengi huchelewa kuweka mbolea kwa sababu huwa hajajiandaa.

7. Shamba lisiwe mbali sana na makazi yako utashindwa kulisimamia. Kwa kifupi haya ndio mambo ya msingi ya kuzingatia katika kilimo cha mahindi.

Mhitimu Chuo cha kilimo Uyole 2010, SUA 2017.

Mungu abariki kazi ya mikono yenu.
 
Asante kwa kutukumbusha, mimi wa Ruvuma napata shiida sana juu ya matumizi ya mbolea. Huku wanachanganya UREA, CAN na SA wengine wanatumia CAN na SA tu je nifanyeje kitaalamu?
 
Kwema mkuu na hiii mbolea ya supergro inafaa kweli
 
Kuna tafiti nmesoma zilifanywa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Ruvuma zinaonyesha maeneo mengi udongo wake umechachuka.Yaani udongo umekua (very Acidic) kwa sababu ya matumizi ya Mbolea za chumvi chumvi kwa mda mrefu hasa SA(Sulphate of Ammonia ) ambayo wakulima wa viazi wamekua wakitumia kwa miaka na mikaka.

Hivyo kitendo cha kuchanganya mbolea ni namna wakulima wanafanya ili kujaribu kupambana na tatzo la kuchachuka kwa udongo japo wao wanafanya bila kujua the reason behind.

Njia bora ya kupunguza na kusawazisha kuchachuka kwa udongo ni pamoja na matumizi ya samadi/mboji km nilivyoshauri hapo juu. Unaweza pia kupunguza kuchachuka kwa udongo kwa kumwaga majivu shambani kabla ya kulima shamba lako.( Yaani unamwaga majivu shambani msimu wote wa kiangazi)

Muhimu jenga tabia ya kurutubisha shamba lako kwa mbolea za asili ili hata unapoongeza mbolea za viwandani iwe kwa kiasi kidogo tu. Nazani utakua umepata kitu.
Asante kwa kutukumbusha, mimi wa Ruvuma napata shiida sana juu ya matumizi ya mbolea.

Huku wanachanganya UREA, CAN na SA wengine wanatumia CAN na SA tu je nifanyeje kitaalamu?
 
Soko la Mahindi Linapatikana wapi ?
Na ni kwa kiasi gani ?
 
Naomba kujua ni mkoa upi hapa Tanzania ambao kilimo cha mahindi kinakuwa vizuri sana na unapata mavuno mazuri.
 
Nimepanga kulima maeneo ya kijingu mkuu pia kuna shamba jingine nimepata maeneo ya lantomoni ila bado sijafanya maamuzi yakulichukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…