Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Ni fursa pekee nitakayoipigania mwaka 2020.

Iko hivi nilipanda mashimo 2200 ambapo niliweka mbegu 2 kila shimo. Hivyo nilikuwa na mashina kama 4000. Mahindi yalizaa mawili ambapo moja kubwa na lingine dogo. Nilivuna takribani mahindi 5000 na kuyauza kila moja sh 300 na kupata mil 1.5 ndani ya siku 75 na yaliyobakia nilikausha nikapata kama gunia 1. Sasa nimepanda mashimo 6000 na February nitapanda mengine 10,000.

Faida ya Kilimo Cha Mahindi.

1.Hayahitaji dawa nyingi za wadudu zaidi ya dawa moja tu.
2.Gharama zake ni ndogo.Mfano ekari moja unatumia kama laki 4 tu.
3.Wateja wa mahindi mabichi sio issue na hata yakikauka unauza makavu.
4.Hauhitaji kuwa shambani muda mwingi.

Karibuni tulime mahindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa ila usiongelee mashimo , ongele ilikua ekali ngapi ili nikalime kibiti ekali zangu 2 nione matokeo
 
Nimependa ila usiongelee mashimo , ongele ilikua ekali ngapi ili nikalime kibiti ekali zangu 2 nione matokeo
Sawa...kama ekari yako ina ukubwa wa sqm 4900 utapata mashimo 4900 yenye umbali wa mita 1.Hapo utapanda mahindi 3 kila shimo na utapata 14,700 ambayo yatazaa mahindi 29400.Kati ya haya 21050 yatakuwa grade 1 utauza 300 kila moja na kupata 6,615,000/- kwa heka moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa...kama ekari yako ina ukubwa wa sqm 4900 utapata mashimo 4900 yenye umbali wa mita 1.Hapo utapanda mahindi 3 kila shimo na utapata 14,700 ambayo yatazaa mahindi 29400.Kati ya haya 21050 yatakuwa grade 1 utauza 300 kila moja na kupata 6,615,000/- kwa heka moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kifupi naanza kulima masika hii tutapeana mrejesho ila mimi naanza na maharage ya njano
 
Sawa...kama ekari yako ina ukubwa wa sqm 4900 utapata mashimo 4900 yenye umbali wa mita 1.Hapo utapanda mahindi 3 kila shimo na utapata 14,700 ambayo yatazaa mahindi 29400.Kati ya haya 21050 yatakuwa grade 1 utauza 300 kila moja na kupata 6,615,000/- kwa heka moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapo kaka kuna changamoto sana hasa kwenye bei ya mahindi mabichi na mara nyingi bei ni Tshs 150 na ikiwa bei nzuri inafika Tshs 200/= ingawa kwa nadharia unalosema kwa hekari kupata mahindi 29400 hapana mkuu, na sisi wakulima tungekuwa tunapigania huko huko kwenye mahindi mabichi alafu hekari tano tu unatoboa, yaani milioni 30 na ushehe hiyo ingekuwa dhahabu juu ya ardhi isiyokusumbua kichwa.
 
Mimi nimelima season 3 kwa mwaka huu...nilitoa mwezi July, October na December hii nitatoa kuanzia 27,mara zote hizo sijauza chini ya 300.
Shida naiona hapa wakulima wengi hatufuati ushauri wa wataalam.
Mfano aina ya mbegu na kalenda ya mazao.Na ni kweli kwa maeneo ya Pwani ukitoa kuanzia April hadi May utakutana na ya masika hapo bei itakuwa hiyo 150-200.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ushauri ndio tunataka yaani kutoka kwa mtu alielima kweli sio zile hekaya za matikiti
 
Mbolea nzuri ya kupandia ni DAP AU Yaramila otesha, utahitaji almost 24 to 30 kg ya mbegu kwaajili ya ekari Tatu.

Bei ya mbegu kwa sasa 12,000 kwa pakti yenye 2kg
Dar maduka gani tunaweza pata mbegu
 
Msimu huu wa kilimo nimeamua kuingia kwa miguu yote miwili katika shughuli ya kilimo cha mahindi na maharage.

Nimepanda mahindi kwenye eneo la ukubwa wa ekari 9 ambapo nimepanda mbegu kilo 90.

Kwa upande wa maharage nimemwaga mbegu gunia mbili ambapo ukubwa wa eneo ni kama ekari saba hivi.

Hivyo wadau wenye uzoefu na kilimo niombe kupitia uzi huu mtoe ushauri na changamoto za kilimo na mimi nitakuwa ninaleta updates nini kinaendelea huko shambani mpaka mavuno.

Naomba kuwasilisha
 
Ukivuna maharage na ukafanikiwa kuyahifadhi vizuri, kuanzia mwezi wa kumi bei inakuwa nzuri zaidi, Mahindi ni 50/50.
 
Back
Top Bottom