Entrepreneur
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 1,087
- 622
Mkuu baraka607, wazo na
ushauri wako ni mzuri sana kwa wanajamii wanaotaka kujishughulisha na
Zao tajwa. hesabu ulizoweka juu ni za kuvutia hasa kwa anayehitaji
changamoto kutoka kwa mtu aliyejaribu biashara hio.
USHAURI WANGU KWAKO
Nadhani ungewavuta wengi sana na kununua mbegu kwa wingi iwapo
ungewaekea takriban za gharama. kwa mfano, kama inaitajika mbolea ni ipi
na kiasi gani, upandaji wake ni vipi, utaalamu wa kutoa vitunguu vingi
na kadhalika nyingine nyingi tu. mimi sio fundi wa haya mambo ila
nadhani umenipata. na kwenye gharama ukitaka mteja wa mbegu arudi
ungepiga kama ulivyosema hapojuu wewe umeuza at minimum price of 85K.
85k *100 gunia = 8500,000/=
Ans - 600,000 za mbegu kutoka kwako=7900,000 Then Gharama za uzalishaji
kwa takriban. kwa hilo mtu anaweza kujikuta faida ni ndogo kuliko
ulivyotaja na hapo akaamua kununua mbegu za eka mbili ama zaidi ili
kufikia malengo. kwa mtindo huu wewe utauza mbegu na mteja lazima
atasambaza sifa za mbegu yako.
Wazo ni zuri sana. Mimi
nalima vitunguu Singida Wilaya mpya ya Mkarama Kata ya Mwanga.
Baraka alichosema kimsingi anapenda watu waweze kupanua mawazo kuelekea
kwenye kilimo kitu ambacho nakiunga mkono sana. Tatizo ambalo hajaweza
kulijua na huende anasikia siyo MKULIMA ekari moja inapandwa kilo tatu
za mbegu. Bei za mbegu ni tofauti sana kulingana na maeneo kwa mfano Red
Bombay ambazo tunazalisha sisi wenyewe huku mashambani debe moja
halizidi laki moja.
Mbegu aina ya Neptune inapatikana Barton Tanzania Ltd inauzwa 120,000/-
kwa nusu kilo, Red Caraoke ya South Afrika inauzwa 80,000/- kilo moja.
Kuhusu bei ya soko huyu ndugu anazungumzia Hapa Dar, hajasema huyo
mkulima kutoka Mang'ora, au Singida Vijijini kwa bei anayosema dalali wa
sokoni hamzungumzii najua huwezi kuleta bidhaa sokoni ukauza mpaka
uwaone madalali.
Nina uzoefu mkubwa mwaka jana nilileta gunia 130 kwa mtu aliyesema
angenunua akaja akaona mzigo akaufungua na kushona upya akatoa gunia 124
kwa bei ya 73,000/- wakati nimevitoa shambani singida akalipa advance
millioni sita na laki tano pesa nyingine mpaka leo hajalipa simu
hapokei.
Mwezi wa tano vitunguu shambani wanunuzi walileta bei ya shilingi
40,000/- hadi 50,000/- kwa gunia la wavu wanapakia viroba vitatu
wanasema ni gunia moja, nikaona ni bora nilete vitunguu soko la misuna
singida mjini, bei yao ilikuwa shilingi 53,000/- kwa gunia moja. Ushuru
ni shs 1000/- kwa gunia, dalali 2,000/- kwa gunia, wanaochmbua shs
1,000/- kwa gunia, mshonaji 1,000/- kwa gunia nilikuwa na gunia 67.
Rafiki bei ya vitunguu haijawa na msimamo inategemea baraka za madalali
na wingi wa mzigo uliopo sokoni.
Nitakupigia Baraka simu ila ukweli ndio huo.
Nna ushahidi wa risiti tokea nimeanza biashara hii miaka minne iliyopita, kama nna gunia nimewahi kuuza chini ya elfu 85 nafuta tangazo hili. Cha zaidi mtu halazimishwi kuchukua opportunity, ni maamuzi binafsi kaka. Next time "Think before you act" Mr
Sasa labda sie wakulima itabidi tuwe na mtandao ili Ndugu yetu Baraka atatusaidia kwenye suala la soko.
Naamini bei inaweza kuwa kubwa kutokana na umoja wa wakulima lakini kila mtu akiuza kivyake matokeo ni bei tofauti.
Mimi naendelea kupanda maana nalima jumla ya eka 23 kila msimu pia nalima eka nne kwa kumwagilia ambazo huwa navuna mwezi wa Novemba.
Madalali yeye hajagusia amewezaje kuwakwepa anapopeleka vitunguu vyake sokoni na wanunuzi amwasiliana nao vipi mpaka wakaweza kufika shambani kwake.
Twaweza kupata namba za wanunuzi nasi tukajaribu bahati zetu?
Nimevutiwa sana na hii ya kulima vitunguu. Vp hapa dar vinaweza kustawi? Namaanisha maeneo kama chanika. Naomba msaada wadau.
Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi kutokana na mtu niliyemuachia maagizo ya kuweka bandiko hili hakutoa ufafanuzi mzuri.
Ufafanuzi huu ntautoa kwa kifupi hapa na ntaambatanisha na excel ambayo ina mchanganuo mzuri zaidi.
Mbegu hii imeandaliwa kisasa na inazalishwa nchini kenya, nimeitumia huu ni mwaka wa nne na sijawahi kukatishwa tamaa na mbegu hii.
Kwa kawaida hutumia lita 10 hadi 15 kwa eneo la ekari moja.
Suala la bei sokoni kwanza kabisa inatokana na ubora wa kitunguu na pia timing ya mavuno yako. Kwa mfano, mimi nalima Kidete na Bagamoyo. Kidete huwa napanda mwezi wa tatu katikati na nakuja kuvuna mwezi wa saba kwenye tarehe 10 na huwa nakutana na bei ya 110,000 hadi 95,000 na kwa bagamoyo nimepanda mwezi huu mwanzo na nategemea kuvuna mwezi wa tatu ambapo bei ya vitunguu huwa juu sana kwasababu shamban tu gunia hufikia hadi 120,000/=
Naomba nieleweke kwamba haya yote nnayoongea sio kwamba navutia biashara ya mbegu ila ni kitu halisi na mtu yoyote anaweza kufika ofisini na nikamuonyesha risiti za mauzo ya sokoni. Kwa fukara kama mimi anayetafuta kujiajiri hii ni nafasi nzuri na tutasaidiana kwa utaalamu bila malipo yoyote.
NB: Naomba muangalie excel niyoiambatanisha hapo chini nimejaribu kutoa mchanganuo wa gharama kamili ya kilimo kwa shamba la ekari moja na mchanganuo kama ukiamua wewe mwenyewe kuleta mzigo mjini na faida ya biashara nzima ndani ya miezi mitatu.
Kama kuna sehemu ntakua nimesahau kutoa maelezo basi tusameheane na ntashukuru ukinitafuta tukaongea zaidi kulikoni kutoa maneno machafu na ya kejeli mtandaoni.
Ahsanteni sana
namba yangu no 0655003510
Nimewahi kupanda vitunguu maeneo ya Mbezi makabe aina ya red bombay vilisitawi sana na nilipata mavuno mengi japo nilitumia kumwagilia maji ya bomba wakati panakituo cha CHILD IN THE SUN