Mkuu naona unasema unalima vitunguu bagamoyo naomba kuuliza vitunguu vinakubali katika mazingira ya pwani na kwenye udongo wa Kichanga? Sehemu kama Mkuranga unaweza lima vitunguu?
Ndiyo vinakubali katika mazingira hayo, ila tu kuwepo na maji na udongo wenye rutba nzuri. Usiwe mfinyanzi sana kwasababu huzuia kitunguu kujitanua
Mkuu shamba langu udongo wake ni Kichanga pure lipo Mkuranga naweza lima vitunguu? Mchanga unaweza stawisha vitunguu?
Shukrani wakuu kwa maelezo yenu mwaka 2015 inshallah nataka kuacha kazi rasmi niwe mjasiriamali tu nimechoka kuajiriwa,ngoja nipitie comments zote nijipange kununua hekari hata mbili,kitange na baraka ebu wekeni process from the beginning utayarishaji wa shamba,kupanda,vitalu,umwagiliaji,upaliliaji,umwagiaji dawa ili nipate mwongozo!!
Yan kuchanga kama cha baharini vile?!
Kichanga kama eneo kubwa la Dar lilivyo
Yan kuchanga kama cha baharini vile?!
Kama umeishi Dar au Pwani utanielewa mkuu namaanisha sio udongo mwekundu wala mweusi (Mfinyanzi) bali ni udongo wa kichanga unaopitisha maji kirahisi
We hiyo sehemu ushawah kulima nn?!
Ina mananasi sasahivi na yako poa tu
Mkuu king kong karibu. Process kwa maandishi kidogo ni ngumu kukuelezea ukaelewa. Ila ukiwa na muda tutafutane, utafika ofisin na ntakupa muongozo wote kuanzia mwanzo hadi mwisho.
ofisi zako zipo wapi? number za simu?
Ushauri wa maana sana huu aiseeeMkuu kama uzalishaji wako ni mkubwa mimi nakushauri utengeneze mivuko ya nusu kilo na kilo moja upeki mwenyewe uanzishe stoo ndogo ndogo mitaa ya kariakoo na namanga kama unauwezo kidogo kimfuko.
Utapata wakati mgumu mwanzo hesabia kama miezi mitatu mpaka mitano. Baada ya hapo utapiga bao.
Mfumo huu Tanzania haupo itakuwa wewe ndio muanzilishi nakwakuwa malighafi inatoka shambani kwahiyo itakuwa na bei rahisi kulinganisha na soko la kawaida ambalo linapita kwa madalali zaid ya wawili, ukiwa naufungaji mzuri uanaweza kuza kwene maduka makubwa, wakati huo unatafuta soko la mahoteli ya aina zote ndogo na kubwa jaribu kufanya stad kabla hujaanza
Mkuu ni kweli kabisa unachosema ni kuwa watu hawajajua tu mim nimegusa tu kidogo mwaka jana nimeondoka na mil 3 sasa nataka mwaka huu ndiyo nizame ki kwel kwel, maana kupata gunia 100 kwa kitunguu ni kugusa halafu kuna kipind kama sasa gunia moja laki ×100 una 10milion hapo bado hujatoka tu kimaisha kwa mtaj wa 10 mil wakat wewe garama uliyotumia haizid mil 2 lakin kwa muda mfup unatengeneza faida ya mil 8 Mungu akupe nin tena. Mkuu komaa tu mim ninao mfano kuna watu walianza na mtaj wa laki kadhaa kwenye kilimo cha vitunguu lakin sasa ni matajiri wa kutupwa had unakuja kufikiria kuajiriwa hakuna dili kabisa kwa mtu anaezingatia kilimo
Hongera mkuu,
Umejaribia wapi, na ulifanya cha umwagiliaji au cha kutegemea mvua, na soko lako lilikua lipi kwa hayo majaribio yako?