Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mkuu ngawia yakupasa ucheze vizuri na msimu wa mvua usijekuambulia patupu. Kitunguu kikikutana na mvua at maturity stage utalia! Fuatilia majira ya mvua za mwaka zinaanza mwezi gani then rudi nyuma atleast miezi minne na nusu ndo utakuwa in a safe period.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umetisha kwa data, kuna haja ya tafiti kabla ya mradi
unaloongea ni kweli mkuu ufuta unalipa sna tatizo ni madalali.embu angalia bei za maeneo haya morogoro gunia laki na themanini hadi laki2.sumbawanga laki2,tanga laki2 pwani laki nathemanini,manyara hawa majamaa walianza na laki5 gunia na sahvi wanauza laki3.hawa wenzetu wa manyara wanafanikiwa kuuza kw bei kubwa sbb wanalima maeneo makubwa nawamezibiti madalali,kuna makampuni ya wahndi toka arusha ndyo wananunua hapo manyara.wakulima wa manyara wako makini kila idara kuanzia uzalishaji wako juu kwa pato kwa eka,mbegu bora napia wanazalisha ufuta wenye kiwango.hayo maeneo yote niliyotaja nimefanya utafiti mm mwenyewe nilianzia morogoro pwani na tanga,sumbawanga nilichukua tarifa kwa wadau sijafika,manyara nawaelewa tangia mwanzo na sahv ndyo naelekea manyara kuchukua data nzuri kwnn wao wamefanikiwa kuliko mikoa mengine
 
Mkuu GEBA2013, tikiti linahela pengine ni usimamizi ndio ulikuangusha. Huwezi kulinganisha pato la ufuta na tikiti hata siku moja. Dunia ya sasa unatakiwa ufanye uzalishaji wenye uhakika wa kutoboa. Mi sifanyi kilimo cha kutegemea mvua hicho walifanya mababu! Ni mara 100 nikalima ekari2 ntakazozimudu na nikawa na uhakika wa mavuno kuliko ekari mia huku nikiumiza kichwa na shingo kila kukicha nikiomba neema ya mvua.

Fanya vzr mahesabu yako na tafakari kwa kina kile nilichokiandika hapo juu kwani nina uhakika wa nisemacho.
Kama huamini kwamba sh milioni3 haiwezi kuzalisha milioni40,basi njoo na hiyo hela shambani kwangu nikupe darasa nakuhakikishia hiyo hela itapatikana ndani ya siku75. Ila sharti utarudi kwenu na sh m15 tu!!

Mkuu Kisima, ni maeneo gani tikiti linastawi, je maene ya Chanika na Mkuranga ni mazao gani yanastawi?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MILCAH28 asante kwa complement, nakuomba ufuatilie nyuzi kuhusu kilimo cha vitunguu maji wadau wamejadili sana kwenye jukwaa hili safu ya ujasiriamali.

Mkuu GEBA2013 atakupa msaada mzuri kuhusu upatikanaji wa mbegu bora za vitunguu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kyenju ukanda wote wa pwani unafaa kwa kilimo cha tikiti. Mhimu uwe ni udongo usiotuamisha maji.

Nakushauri kama unataka kuengage na masuala ya kilimo hasa cha bustani jitahidi usimamie mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
GEBA2013 na Kisima i salute u wadau, Geba ntakutafuta hv karibuni kwa ushauri nataka nilime nyanya za msimu dodoma

KAMA UNATAKA KULIMA NYANYA ANDAA SHAMBA MAPEMA CHUKUA MBEGU BORA AINA YA ANAF1 AU EDEN ANDAA KITALU CHA MBEGU MWEZI 8 TAREHE ZAKATIKATI YANI TAREHE I0 HADI 20 HAPO ILI UPANDE MWEZI WA9 TAREHE 10 HADI 15 NA UANZE KUVUNA MWEZI 12 MWISHONI KIPINDI CHA KRISMAS NA NEW YEAR,HAPO UTAKUTANA NABEI NZURI.mengne ni changamoto tu unaweza kukabiliana nayo km dawa nk
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kyenju ukanda wote wa pwani unafaa kwa kilimo cha tikiti. Mhimu uwe ni udongo usiotuamisha maji.
Nakushauri kama unataka kuengage na masuala ya kilimo hasa cha bustani jitahidi usimamie mwenyewe.

Shukrani mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Habar za asubuh wadau!

Nimepata mashamba maeneo ya kisarawe na ninataka mwaka huu nilime ufuta. Nimesikia ufuta una soko zuri na uhitaji wake ni mkubwa.
Naombeni taarifa sahihi juu ya ulimaji, upatikanaji wa mbegu, soko na msaada wa kitaalamu juu ya kilimo cha ufuta.
Pia ntashukuru kama kunasehemu (kampuni/mtu binafsi anaeweza kunipa msaada wa kitaalamu.
Nawatakia jumatatu njema na swaumu njema kwa wafungaji.
Wenu katika ujenzi wa taifa Bintimzalendo

Ni-pm, niliwahi fanya kazi na mradi ambao unahusika na ufuta naweza kuwa msaada kwako!
 
ni-pm..niliwahi fanya kazi na mradi ambao unahusika na ufuta naweza kuwa msaada kwako!

kwnn usiweke hadharani ili iwe msaada kwa wengne?wenzako wametiririka bila uchoyo,ww pm ya nn?au unataka kumtongoza?acha uchoyo mkuu
 
Maoni yenu ni mazuri sana, binafsi nimelima ufuta huko ilangali dodoma, nilifuata taratibu zote, ufuta ulikubali sana sana, ila kwenye mavuno kilichotokea ilikuwa kama ndoto, mchwa walikuwa wengi sana kwenye ufuta, ila kiufupi kulikuwa na mambo ya kishirikina ambayo ni isue kubwa sana kwenye maeneo mengi yenye mashamba, najua mambo ya kimazingara au ushirikina upo ila siamini katika hilo kama ni kikwazo, ila ilinipelekea kuamini baada ya kuchukua nguvu kazi kutoka sehemu nyingine baada ya wale wa eneo husika kuwa sio waendaji wazuri, hii ilipelekea wao kujenga chuki na kutooa ushirikiano waliokuwa wanatoa mwanzo, maana yangu na lengo langu nikwa wakulima wapya kusoma mazingira ya wanaokuzunguka.
 
Ndugu...ufuta ni zao lenye bei nzuri sana ila linhitaji uangalifu ili ujue ni kipindi gani utakachokuwa unavuna.Masoko ya ufuta yapo India na wahindi wananunua ufuta kwa msimu kwa kuwa huwa wanauhitaji kwa kipindi fulani cha mwaka.Ikiwa ni off season bei inaanguka sana.
 
Mkuu Kyenju ukanda wote wa pwani unafaa kwa kilimo cha tikiti. Mhimu uwe ni udongo usiotuamisha maji.
Nakushauri kama unataka kuengage na masuala ya kilimo hasa cha bustani jitahidi usimamie mwenyewe.

Habari kaka kisima. tafadhali naomba uniPM namba yako nikutafute tuongee zaidi
 
Last edited by a moderator:
Mwaka huuu naingia shambani kulima hiyo ni lazima
 
Ndugu...ufuta ni zao lenye bei nzuri sana ila linhitaji uangalifu ili ujue ni kipindi gani utakachokuwa unavuna.Masoko ya ufuta yapo India na wahindi wananunua ufuta kwa msimu kwa kuwa huwa wanauhitaji kwa kipindi fulani cha mwaka.Ikiwa ni off season bei inaanguka sana.

Kaka kama unalima ufuta Tafadhali naomba uniPM number yako.
 
Wadau naombeni kujua faida ya zao la ufuta kwa ekari moja..je bei ya kilo moja ya ufuta sokoni ni sh ngapi? naweza kupata magunia mangapi kwa ekari moja.
 
Back
Top Bottom