Kimbunga Jobo: Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar yawatahadharisha wananchi

Kimbunga Jobo: Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar yawatahadharisha wananchi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mamlaka za hali ya hewa zimeendelea kutaka wananchi wachukue tahadhari dhidi ya kimbunga JOBO ambacho kwa sasa kipo umbali usiozidi km 400 kutoka mwambao wa Bahari ya Hindi.

Kamisheni ya Maafa Zanzibar imetoa tahadhari kwa wavuvi na wamiliki wa vyombo vya usafiri baharini kutokana na uwepo wa kimbunga hicho.

Kamisheni ya Maafa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) wanaendelea kufuatilia kimbunga na wataendelea kutoa taarifa.

1619166317604.png
 
Uzuri kadiri kinavyozidi kukaribia kwetu, kinazidi kupungua nguvu, kwahiyo madhara yatakuwa ni kidogo mnooo, labda watumiaji wa bahari ndo wata feel hizo athari.
 
Utabiri wa hewa umebaini kuwa kuna tropical cyclone iliyoitwa jina la Jobo inayoelekea pwani ya Dar es Salaam na Zanzibar. Kimbunga hiki sasa hivi kiko Madagascar na inakadiriwa kufika Tanzania jumapili tarehe 25 April 2021 kwa utabiri wa watalaamu wa hali ya hewa.

Je wananchi wa Dar es Salaam na Zanzibar wameandaliwa ya kutosha ikiwa kweli gharika hili kama litatokea? Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na ghalika la kimbunga hiki ni pamoja na:

1. Kukosekana kwa umeme kwa kipindi kirefu.
2. Kukosekana kwa huduma mhimu kwa sababu ya mafuriko na mvua kubwa. Chakula sokoni hakitapatikana au hakitafikika. Simu zitaishiwa chaji. Mafuta ya magari hayatapatikana au kufikika. Gesi ya kupikia chakula haitapatikana au kufikika. Vituo vya matibabu havitafikika. Njia za kupata habari kama TV na redio zinaweza kuwa za shida na kadhalika.
3. Wananchi kujeruhiwa au kupoteza maisha.
4. Wananchi kukosa makazi kutokana na nyumba kuezuliwa paa au kubomoka na kusombwa na mafuriko ya mvua kubwa na bahari kufurika.

Tumuombe Mwenyezi Mungu atuepushe na kimbunga hiki kama alivyotuepusha na kile cha Msumbiji mwaka jana.
 
Spidi yake inapungua hivyo madhara yanaweza yasiwe makubwa iwapo kitafika pwani ya Dar-es-Salaam na Zanzibar( madhara ya kimbunga hutegemea zaidi spidi ya upepo( windspeed) itakanayo na kimbunga husika.

Madhara mengine ni kimbunga kusababisha mvua mkubwa inayoweza kuleta madhara( mafuriko, n.k).

Vile vile kinaweza kufa(ku-decay) kabla hata ya kufika pwani ya Dar-es-Salaam na Zanzibar iwapo hakutakuwa na favorable conditions kwa kimbunga kuendelea kuwepo baharini.

But all in all, the risk is still there so we should take necessary precautions kwani kinaweza kuongezeka nguvu iwapo favaroble conditions for it to intesify zitajitokeza.
 
Tuombe Mungu kiendelee kupunguza speed mpaka kinapofika kwenye pwani zetu ya Zanzibar na Daslm...
 
Wabunge wa CCM ndio kwanza wameanza kudanganya umma
1. Serikali haikufungia biashara za MBOWE, je Bilicanas ilivunjwa kwa amri ya Nani?
Tanzania daima ilifungiwa kwa amri ya Nani?
Mashamba kule Hai yaliharibiwa na Nani?

2. Eti ofisi ya Bunge haikupata barua ya kufutwa uanachama wa kina Mzee Halima Mdee
 
Kingekuwa na madhara makubwa wangesema ila kinaweza kusabisha endapo kama wakati kikifika
 
Hizi Serikali za Kiafrika huwa zinasubiri majanga kama haya yauwe maelfu na maelfu ya watu ili watembeze Bakuli wapate fedha za misaada yao waile
 
Wabunge wa CCM ndio kwanza wameanza kudanganya umma
1. Serikali haikufungia biashara za MBOWE, je Bilicanas ilivunjwa kwa amri ya Nani?
Tanzania daima ilifungiwa kwa amri ya Nani?
Mashamba kule Hai yaliharibiwa na Nani?

2. Eti ofisi ya Bunge haikupata barua ya kufutwa uanachama wa kina Mzee Halima Mdee
Kwani hilo ndilo gharika la kimbunga Jobo?
 
Back
Top Bottom