Kimbunga Jobo: Kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar yawatahadharisha wananchi

Ohooo Ka Uzi kamepotea. Ule ujinga uliofanyika October 28 mwaka Jana umeturudisha miaka 80 nyuma.
 
Acheni uoga, upepo utakuwa spidi 60kph tu. Huu upepo hata hauwezi nyanyua bajaji. Ingekuwa vya wenzetu vimbunga vilivyochangamka vinatembea na kasi ya upepo wa 150kph+ si ingekuwa balaa?!
NB:
Nyumba yenye nyufa inayopulia mashine na mabati yaliyoegeshwa jiwe/tofali kwa juu kama mbadala wa msumali usikae tafadhali.
 
Asante Mkuu kwa ushauri
Habari njema ni kuwa kimbunga hakitakuwa kikali Nguvu ya Upepo mkali imepungua isipo MVUA ndio tishio kwa sasa
Waliopo mabondeni bado wanayo nafasi ya kujisogeza
 
Asante Mkuu kwa ushauri
Habari njema ni kuwa kimbunga hakitakuwa kikali Nguvu ya Upepo mkali imepungua isipo MVUA ndio tishio kwa sasa
Waliopo mabondeni bado wanayo nafasi ya kujisogeza

Sote tunachoombea ni salama.

Ila panapo uwezekano tuchukue hadhari za kutosha.

Maisha kwanza mengine yote baadaye.
 
Asante hayati rais Magufuli kwa kutuachia wosia wa kuacha hofu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Kimbunga Jobo na Corona wamekiona cha mtema kuni Tanzania.
 
Asante hayati rais Magufuli kwa kutuachia wosia wa kuacha hofu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Kimbunga Jobo na Corona wamekiona cha mtema kuni Tanzania.

Nakazia, hakuna anayehitaji maafa wala majanga popote. Ila maafa hukabiliwa.

Mzaha mzaha hutumbua usaha. Yalimkuta mzee baba (rip).

Kwamba Corona ichague kuondoka au kuishi kwa adabu? Ngonjera hizi si Pole pole au nduguze wanazoziimba tena.

Kwamba ilikuwa vita vya kiuchumi? Hayupo hata mmoja anayeyaimba hayo tena.

Tuko awamu ya sita sasa kwa roho safi tunasubiria:

1. Ripoti ya CAG kuhusiana na BOT, TPA, tanroads na wajomba zao.
2. Ripoti ya tume ya wataalamu wabobezi kuhusiana na Corona.

Mama Samia atatuvusha unafiki hatutaki.
 
Wasiwasi wako tu.

Ukweli huwa mchungu kuliko shubiri.

Laiti nwendazake angesikiliza tu, mbona bashiri angekuwa KMK na mipango yetu Chatto ingekuwa inakwenda bam bam.

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
Mkuu bado huna Imani? Mungu amesikia maombi yetu watanzania. Mimi nikijichunguza simwoni ndugu wa ukoo wangu aliyekufa kwa korona.Sijasema haipo Ila sio kwa kiwango Cha kuhitaji lockdown.
 
Huko Ufilipino kimbunga cha aina hii miezi 2 iliyopita kiliwafanya hivi:

 
Kikawaida cyclones huwa hazikimbilii towards the equator. Zikifanya hivyo huwa zinakosa nguvu na kutawanyika. Kwa maana hiyo hatari kubwa kwa hii Cyclone ya Jobo ni Lindi na Mtwara (9 degrees S) na sio Dar (6 degrees S).

Ndiyo maana cyclones nyingi zinazoanzia bahari ya Hindi huwa zina gain southwards na kuishia Madagascar au Mozambique. Hii ya ku gain northwards towards the equator kwa kweli ni ajabu

Kikawaida ni vigumu kutokea cyclone/hurricane/typhoon 5 - 7 degrees South or North of the Equator sababu kuna Coriolis Effect ndogo. Dar ni 6 degrees South of Equator kwa hiyo ideally cyclone itadhoofishwa na kutawanyika inapokaribia Dar. Ndiyo maana Lindi na Mtwara (9 degrees S) makes more sense.

Huku kwetu kwenye Southern hemisphere cyclones zote huwa zinaenda clockwise, hata vimbunga n.k......kwenye Northern hemisphere huwa ni anti-clockwise. Sasa tunapo approach Equator huwa hii phenomenon inapungua na tunapoenda mbali na equator inaongezeka....na kwenye equator yenyewe hakuna hii effect......cyclones huwa hazikimbilii equator. Kwa mfano unaweza kufanya practical kidogo.....tukijaza sink maji tukiyafungulia yatazunguka clockwise sababu tupo Southern hemisphere ila kwa wenzetu waliopo northern hemisphere (mfano Uingereza) itakua anti-clockwise....na waliopo equator mfano Kenya au Uganda yataanguka tu straight down! Ndiyo maana inavyosemwa kitaenda northwards hapo ni ajabu sana.

Kinadharia....the worst that can happen kwa Dar ni mvua tu tena kwa kiasi chake. Kitakutana na mengi ya kukiresolve njiani mpaka kifike Dar. Imesahaulika tu kukumbushia oceanic currents,......maana kikiwa njiani kwa upande uliosemwa kutokea kitakutana na Mozambican current hivyo kitapunguzwa nguvu sana.

Vurugu inaweza kuwa kusini hasa Mafia, Rufiji na kwenda Lindi na Mtwara. Dar si rahisi....kikija northwards kuanzia (Dar) na kuendelea maeneo mengine northwards kweli kitakua kimefanya Job kama wanavyokiita Jobo 😅
 

I bet upo kwenye hii field , umeongea kiutalaam sana
 
Tunashukuru sana mama kwa kutuondolea kimbunga. Mitano tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…