Kimei alaani mauaji ya kijana Octavian, ataka haki itendeke na kuwatuliza wananchi

Kwanini tutumie askali wakiba awana uwezo wa kumuoji mtu tunaona barabarani jinsi wana vowaonea wafanya biashara na kuwapiga na kuvunja meza zao wakati kama mtu atii amlii anatakiwa akamatwe jera miedhi 6 au faini shiling 50 awa sisi watatu uwa sana shelia zao zipo mkononi
 
Moyo wangu umeumia sana kupoteza nguvu kazi, yaani kweli mtu anauawa kwa sababu ya kukata majani jamani, ni maumivu sana chombo tunachokiamini kwa ulunzi kudanganya au kutetea mauaji eti amejinyonga yaani katika mambo sitaki kusikia ni kuona mtoto wangu anakuwa askari, bora awe mjeshi kwa kweli
 
Sema wachaga Wana roho mbaya sana hasa wakiwa na madaraka au wakiwa wanataka madaraka
 
Moyo wangu umeumia sana kupoteza nguvu kazi, yaani kweli mtu anauawa kwa sababu ya kukata majani jamani, ni maumivu sana chombo tunachokiamini kwa ulunzi kudanganya au kutetea mauaji eti amejinyonga yaani katika mambo sitaki kusikia ni kuona mtoto wangu anakuwa askari, bora awe mjeshi kwa kweli
Sitetei hili lakini alikuwa anakata ndani ya hifadhi kitu ambacho walishapigwa marufuku kisheria, according tu habari ni katika purukushani za ukamataji sidhan kama askari alidhamiria
 
Kwanini tutumie askali wakiba awana uwezo wa kumuoji mtu tunaona barabarani jinsi wana vowaonea wafanya biashara na kuwapiga na kuvunja meza zao wakati kama mtu atii amlii anatakiwa akamatwe jera miedhi 6 au faini shiling 50 awa sisi watatu uwa sana shelia zao zipo mkononi
Askari wa akiba hawapewi silaha, wanaobeba ni wa hifadhi
 
Ila polisi ni majanga sana sijui Huwa wanasomea nini huko chuoni ni aibu wanajitia yaani wameuchukua mwili wa marehemu wameupeleka na hospital kabisa baadae wanawataarifu ndugu zake kwamba marehemu kajinyonga na ndugu wanapopewa nafasi ya kumkagua mpendwa wao wanakuta ana jeraha la risasi kichwani.

My country people .
CCM siyo janga bali wananchi ndiyo janga. Imaging huyu mbunge anasema alishasikia malalamiko ya kupigwa na wanawake kubakwa lakini hakuchukuwa hatua. Na hili la huyu marehemu amepiga kelele kwa sababu anajua uchaguzi unakaribia. Kila kona ya nchi watu wanalia ila wanshindwa kuungana na kuwaondoa hawa makatili kwenye uongozi.
 
Hiyo kesi ya kubakwa kwa wanachi ilifanyiwa uchunguzi, na result zilikuwa ni false, hakukuwahi kupatikana askari wa huko anaefanya vitendo hivyo . Ila zilikuwa ni speculations za wamama waliokuwa wakidakwa ndani ya hifadhi , in retaliations wakaja na hizo slogan, ndio maana unaona hizo kesi huzisikii tena.

Ila kwenye matukio mengine hapo lazoma wawajibike

All in all wananchi wenyewe hawana umoja, hawawez pressure serikali kufanya reforms, wame sambaratishwa. kwa siasa na nguvu
 
TAARIFA YA KIFO CHA NDG OCTAVIAN HUBERT TEMBA

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei amelaani vikali mauaji ya Ndg Octavian Hubert Temba miaka 25-30 toka kijiji cha Komela, kitongoji cha Komela Kaskazini kata ya Marangu Magharibi ambaye anashukiwa kuuwawa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).

Dkt Kimei amesema kwa muda mrefu sasa mahusiano baina ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro sio mazuri kutokana na namna watumishi wa hifadhi hiyo hususani askari wa uhifadhi wanavyowatendea wananchi kwa madai ya kwamba wanasimamia uhifadhi endelevu jambo ambalo sio sawa.

Ifahamike kwamba panapotokea moto mlima Kilimanjaro wananchi wa vijiji vinavyopakana na KINAPA ndio wanaobebwa kwenda kushiriki kuzima moto pamoja na madhila wanayokutana nayo.

Mara zote nilizofanya mikutano katika maeneo hayo wananchi wamekuwa wakieleza kuteswa, wanawake kubakwa, kupigwa na hata kunyang'anywa mali zao kwa kudaiwa wameingia kwenye hifadhi au wamevuna miti ndani ya hifadhi madai ambayo hayatoi uhalali wa matendo ya kinyama na kikatili wanayowatendea wananchi wenzetu.

Familia ya marehemu Octavian ilipofuatilia polisi Himo na Kituo kikuu Moshi Mjini walijulishwa kuna mwili wa mtu anayedaiwa kujinyonga ndani ya hifadhi ya KINAPA ambao polisi wameuchukua na kuupeleka hospital ya KCMC.

Familia ikamjulisha diwani wa kata hiyo Mhe Filbert Shayo ambaye alitushirikisha ofisi ya Mbunge na taarifa zikamfikia Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ambaye alishauri Familia ikautambue Mwili kama ni wa kijana wao pamoja na kuukagua kuona kama una majeraha ya kuashiria kushambuliwa (physical torturing). Familia iliridhia na OCD alitoa ushirikiano kwa Familia na ikafanikiwa kufika mochwari KCMC na kuutambua mwili ni wa kijana wao, katika kuukagua wanadai ulikuwa na jeraha linalodhaniwa alipigwa risasi kichwani na wala shingoni hakukua na alama ya kujinyonga kama walivyoelezwa awali.

Familia ilitoa mrejesho kwa haraka sana mamlaka za kiserikali kwa maana ya mkuu wa wilaya alijulishwa pamoja na Mbunge ambaye alimjulisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Anjela Kariuki ambaye alimhakikishia hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kusababisha mauaji hayo ambayo yanachafua taswira ya uhifadhi pamoja na utalii wa Nchi yetu.

Mpaka sasa zipo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwemo askari wa uhifadhi waliokuwa doria usiku huo kuwekwa chini ya ulinzi huku jeshi la polisi likiendelea na taratibu zake za kiuchunguzi.

Dkt Kimei amesisitiza uhifadhi endelevu hauwezi kujitenga na mahusiano mazuri na jamii. Matukio ya kikatili kama haya ya mauaji, ubakaji na hata kutesa wananchi kwa dhana ya kukabiliana na uvamizi ndani ya maeneo ya hifadhi au kukabiliana na ujangili haukubaliki kwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Wanyamapori na misitu tuliyojaliwa nchini kwetu ni zawadi toka kwa Mungu tuvitumie kwa maendeleo yetu na vikawe neema kwetu badala ya vilio, hofu na mateso kwani hiyo ni laana.

Dkt Kimei ameendelea kuwasihi wananchi wawe watulivu wakati huu ambao serikali inaendelea na taratibu za kisheria pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha haki inatendeka, utaratibu wa uhifadhi endelevu uzingatie mahusiano mazuri na jamii zinazopakana na maeneo yanayohifadhiwa.

Serikali imelipokea jambo hili kwa uzito mkubwa na haki itaonekana kutendeka.

View attachment 2987947
Waliosema kujinyonga wasiachwe na basi tafadhali.
 
Hakuna Kinapa bila Serikali Ukumbuke Hilo
Mnapita njia ndefu Sana.
Hao viongozi wanaoreact Ni Drama tu
Mkizika move imefika mwisho
 
Moyo wangu umeumia sana kupoteza nguvu kazi, yaani kweli mtu anauawa kwa sababu ya kukata majani jamani, ni maumivu sana chombo tunachokiamini kwa ulunzi kudanganya au kutetea mauaji eti amejinyonga yaani katika mambo sitaki kusikia ni kuona mtoto wangu anakuwa askari, bora awe mjeshi kwa kweli
Majani yemyewe mwisho wa siku lazima yaote tena na kua kichaka!!
 
Back
Top Bottom